Padri Kitima ashambuliwa na watu wasiojulikana. Inadaiwa hali yake ni mbaya

Padri Kitima ashambuliwa na watu wasiojulikana. Inadaiwa hali yake ni mbaya

Annunaki

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2021
Posts
2,212
Reaction score
4,676
tec_1646942916.jpg

Hofu kubwa imetanda kufuatia tukio la kuvamiwa na kujeruhiwa kwa Katibu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania (TEC) Padri Dkt.Charles Kitima.

Kupitia mitandao ya kijamii, imeripotiwa kuwa watu Wasiojulikana walimvamia Dkt Kitima majira ya saa 3 usiku wa April 30, 2025 na kuanza kumshambulia wakati akiwa kwenye makazi yake yaliyopo Ofisi za Baraza la Maaskofu (TEC) Kurasini, Dar Es salaam.

Mashuhuda wa tukio hilo waliokuwa eneo la tukio lililozungukwa na mgahawa walisema kuwa Padri Dkt Kitima ikiwa ni utamaduni wake wa kupita na kusalimu watu katika mgahawa mmoja eneo hilo, ghafla walitokea watu Wasiojulikana na kuanza kumshambulia kwa sekunde chache na kisha kuondoka.

Padri Kitima alijeruhiwa maeneo mbali mbali ya Mwili maana alikuwa akivuja damu katika sehemu mbalimbali za mwili wake na haijulikani alijeruhiwa na kitu Gani.

Mara baada ya shambulizi hilo, Dkt Kitima amepatiwa matibabu ya awali kwenye Kituo kidogo cha afya cha TEC kilichopo eneo hilo.

=====
UPDATES:

Polisi wadai kumshikilia mmoja: Polisi: Tunamshikilia Mtu mmoja kutokana na tukio la Padri Kitima kushambuliwa

=====
TAARIFA ZA AWALI:

"Tumepokea taarifa muda huu kuwa Father Dr Charles Kitima ameshambuliwa usiku huu nyumbani kwake na kujeruhiwa vibaya - hali yake si nzuri

Tunaendelea kufuatilia hii taarifa ila ieleweke kuwa shambulio kama hii hatuwezi kuchukulia kama bahati mbaya "

Ameandika hivyo Maria Sarungi kupitia mtandao wa X.

Ikumbukwe Padre Charles Kitima ni Katibu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).

Kama hizi ni taarifa za kweli, ni nini hatima ya hali hii inayoendelea nchini?

CCM mnataka kutupeleka wapi kama taifa?

IMG_20250501_003738_467.jpg


Screenshot 2025-05-01 003332.png
 
Hii ni hatari kubwa sana, ni Habari mbaya sana hii.
Endapo kama Habari hii ni ya kweli, basi Serikali inapaswa kufanya kila liwezekanalo ili kuhakikisha kwamba inauthibitishia Umma kwa vitendo kwamba yenyewe Kamwe haihusiki kwa namna yoyote ile na shambulizi hilo.
Serikali inapaswa ifanye hivyo kwa UAMINIFU MKUBWA ili kuondokana na mashaka yoyote yale kutoka kwa Umma.

Ikumbukwe kwamba: Watu bado hawasahau kabisa kuhusiana na suala la Marehemu Mzee Kibao na suala la jaribio la Mauaji dhidi ya Tundu Lisu ambaye yupo mahabusu gerezani sasa hivi.

Hata kama tukio hilo limetekelezwa na Maadui zake binafsi huyo Padre Kitima, bado Serikali ndiyo itakayonyoshewa kidole zaidi. Hii ni kutokana na Ukweli mchungu Sana kwamba Mazingira halisi yaliyopo hivi Sasa hapa Tanzania Kati ya huyo Padre na Watawala yanaonekana kuwa 'yamekorogeka vibaya sana.'
Very bad timing for the execution of such a satanic action!
 
"Tumepokea taarifa muda huu kuwa Father Dr Charles Kitima ameshambuliwa usiku huu nyumbani kwake na kujeruhiwa vibaya - hali yake si nzuri

Tunaendelea kufuatilia hii taarifa ila ieleweke kuwa shambulio kama hii hatuwezi kuchukulia kama bahati mbaya "

Ameandika hivyo Maria Sarungi kupitia mtandao wa X.

Ikumbukwe padre Kitima ni katibu wa TEC kanisa katoliki Tanzania.

Kama hizi ni taarifa za kweli, ni nini hatima ya hali hii inayoendelea nchini?

CCM mnataka kutupeleka wapi kama taifa?

View attachment 3321207
Ningekuwa mimi ni member wa Jesuit hili lisingepita hivi hivi.
 
Jamani c tulikubaliana JPM Ndo alikuwa katili mpaka watu kufurahia kifo chake na kusema mama ameiponya nchi, hii imetoka wapi tena wakuu 😎
Mama ameamua kufuata mkondo ule ule wa Jiwe. Amekuwa, amekomaa na kurithi tabia zile zile mbaya na mbovu.
Usisahau tu, wakati jiwe akiwapoteza wakosoaji wake, mama alikuwa msaidizi wake mkuu.
 
Back
Top Bottom