Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini (TEC) Padri Charles Kitima amewaasa wanasiasa kujirekebisa kwani ipo siku vijana wataleta mapinduzi miaka michache ijayo. Ameyasema haya kwenye mjadala wa maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Demokrasia Septemba 15, 2022.
"Msipo jirekebisha ninyi wanasiasa wa vyama vyote, Vijana watakuja kuleta mapinduzi miaka kumi, ishirini ijayo hamtayakwepa. Hawana kazi, mnawaibia kura, mnawayumbisha. Na wamekuwa wanakaa kimya sababu wanatuheshimu sisi wazazi wao na viongozi wao, lakini hawatavumilia milele.
Ameshauri tabia za kidemokrasia kuanzia ngazi ya familia, ukoo, kijiji, makanisani na misikitini zianze kuonekana ili zilete uhalisia hadi kwenye mazingira ya siasa.
"Mfano hapa Tanzania, sisi wote hapa ni waumini, uwe Mkristo au Muislamu. Tanzania sasa hivi mniambie ninyi Wakristo ni nani anaye mwambia Mwenyezi Mungu nimetenda dhambi kwa kuiba, au kwa kuhonga wajumbe wa kamati? Ni kama tulishasema kwenye siasa hakuna nini? Hakuna dhambi"
Ameongeza kwa kusema kuwa kama watanzania, tuna kazi kubwa sana ya kujenga zile tabia za kidemokrasia ili kuhakikisha kuwa watu wanayapata madaraka na kuwaleta watu haki zao.
"Sasa hizi tabia za kidemokrasia ambazo vilevile zinajengwa na taasisi za kidemokrasia, unaongelea tume ya uchaguzi ni namba moja kwa sababu ni kwa njia ya uchaguzi ndiyo watu wameamua kusalimisha uwezo wao wa kujitawala kwa hiyo tusiwaingilie kwenye dhamiri zao"