Padri wa Kanisa Katoliki aliyefukuzwa afunguka

Padri wa Kanisa Katoliki aliyefukuzwa afunguka

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Wakati Padre Christopher Fosudo aliyefukuzwa na Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam akitarajia kuondoka nchini hivi karibuni, Jeshi la Uhamiaji limesema halina tatizo naye.

Agosti 17, 2022, Katibu wa Askofu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Padri Vicent Mpwaji alituma barua kwa mapadri wote jimboni humo akiwataarifu kufukuzwa kwa Padre Fosudo.

Padri huyo alikuwa paroko msaidizi wa Parokia ya Watakatifu Mashahidi wa Uganda, Magomeni jijini Dar es Salaam.

Kwenye barua hiyo, Askofu Mkuu wa Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi hakueleza sababu za uamuzi huo wa kufukuza.

“Askofu mkuu wa Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi OFMCap anatoa taarifa kwamba Padre Christopher Fosudo kutoka Nigeria ambaye alikuwa anahudumu hapa jimboni kama paroko msaidizi wa Parokia ya Magomeni hatakiwi tena kuwepo jimboni Dar es Salaam. Hivyo, askofu mkuu amemuagiza Padre Fosudo arudi nchini kwake Nigeria,” ilisomeka sehemu ya barua hiyo.

Taarifa za kufukuzwa kwa padre huyo aliyewahi kuhudumu Jimbo Kuu la Dodoma, Kanisa Kuu la Mtatifu Paulo wa Msalaba na parokia tofauti za Jimbo Kuu la Dar es Salaam ikiwamo ya Mtakatifu Padre Pio ya Tabata Kisiniwa, zilisambaa mitandaoni na kuibua mijadala miongoni mwa waumini.

Kati ya maswali yaliyokuwa yakiulizwa ni kwa nini amefukuzwa na kwa sasa yupo wapi hivyo gazeti hili jana lilizungunza na Ofisa Uhamiaji wa Mkoa wa Dar es Saalaam, Peter Mwita na Padri Fosudo na kuhusu suala suala hilo.

Mwita ambaye ni kamisha msaidizi mwandamizi wa Uhamiaji alisema baada ya taarifa za kufukuzwa kusambaa mitandaoni walimtafuta ili wamjue ni mtu huyo.

Baada ya kuzungumza naye, alisema “Tulibaini yupo nchini kihalali na hana kosa lolote wala taarifa yoyote ya uvunjifu wa usalama na kwa sababu hiyo, sisi kama Jeshi la Uhamiaji hatujaona sababu za kushiriki kumfukuza.”

Akifafanua kilichowashawishi kumtafuta, Mwita alisema walitaka kujua kama yupo nchini kihalali na walipojiridhisha walimwacha aendelee na shughuli zake kwani hakuna aliyetoa taarifa mbaya kumhusu.

Alisema padri huyo aliwaeleza kilichotokea kuwa ni masuala ya ndani ya kanisa hilo: “na si uvunjifu wa amani. Tumewaachia wenyewe kama kanisa kuona watafanya nini.”

Aidha, alisema padri huyo “anasoma PhD katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na alifuata taratibu zote za kisheria na kupewa kibali cha ‘student visa.’ Ili upewe kuna taratibu ambazo alizifuata na kupewa na masomo yake bado hajamaliza.”

Mwananchi pia ilizungumza na Padri Fosudo aliyesema alipoiona taarifa ya kutotakiwa jimboni alishituka na alipohojiwa na Uhamiaji aliambiwa aendelee na shughuli zake.

Alipoulizwa ataendelea na masomo au ataondoka, padri huyo alisema “nimeamua nitakwenda nyumbani, kuna mazungumzo na Baba Askofu nyumbani (Nigeria). Katika mazingira haya siwezi kubaki. Nitakwenda kuzungumza na Baba Askofu yeye ndiye ataamua nirudi au niende wapi.”

Akijibu anatarajia kuondoka lini, alisema: “siku chache zijazo kwa sababu katika mazingira haya, si vizuri kuendelea kukaa bila amani. Nitakata tiketi ya kurudi nyumbani.”

Katika mazungumzo yake na gazeti hili, padri huyo hakutaka kuweka wazi sababu za yeye kufukuzwa akisema: “Si vizuri kuyaweka kwenye magazeti yaliyotokea. Lakini, Watanzania ni watu wema sana.”

Padri huyo alikuja nchini kwa mara ya kwanza mwaka 2014 na kufundisha Chuo Kikuu Kishiriki cha Jordan kilichopo mkoani Morogoro hadi mwaka 2016 aliporudi Nigeria kisha akaja tena kwa masomo mwaka 2017/18 anayoendelea nayo mpaka sasa.

Padre huyo alisema atakapozungumza askofu wa jimbo lake ataamua ama kurejea nchini kuendelea na masomo au kusoma kwa njia ya mtandao.

Agosti 18 ikiwa siku moja tangu barua itoke na kusambaa, gazeti hili lilizungumza na Askofu Mkuu Ruwai’chi kutaka kujua sababu za kumfukuza padri huyo ambapo alisema haawezi. “Mimi nimepeleka ujumbe kwa mapadre,” alisema.

Utaratibu wa kisheria
Kwa mujibu wa Sheria za Kanisa Katoliki (Canon Law), kuna makundi tofauti ya mapadre kulingana na karama zao. Wengine ni wa jimbo, watawa wa ndani au wengine ni wamisionarii wanaoishi katika jumuiya za kitawa.

Chini ya sheria hizo, padre anaweza kufanya kazi katika jimbo au eneo lingine kwa mkataba maalumu. Muda wote mapadre huongozwa na nadhiri za utii, useja na ufukara (wale walio watawa), huku wa jimbo wakiongozwa na utii kwa askofu na useja.

Sheria za Kanisa Na. 1341-1356 zinaainisha adhabu zinazoweza kutolewa kwa waumini wote wakiwamo mapadre na walei pindi wakikosea.

Waziri wa Sheria na Katiba amepewa mamlaka kupitia Kifungu cha 14(1) cha Sheria ya Uhamiaji ya mwaka 1995, kumwondoa nchini mtu yeyote ambaye si Mtanzania baada ya kuthibitika kutenda kosa linalovunja sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa kuwa Padre Fosudo hana hatia yoyote ya kisheria, wataalamu wa masuala ya sheria wanasema hawezi kuondolewa nchini (deportation) kwani ametofautiana tu na mwajiri wake.

Source: MWANANCHI
 
Romani Catholic imejengwa katika misingi ya utii wa hali ya juu. Kamwe, si padri Fosudo au askofu atakayefunguka kuhusu sababu za kufukuzwa.

Ila assumptions za kuadhibiwa mapadri wa Roman Catholic huwa ni uzinzi wa wazi wazi, na wizi wa fedha za kanisa uliopindukia. Padri akiwa anachukua fedha kidogo kujihudumia yeye anavumiliwa tu.

Pia, kosa lingine kubwa kabisa ambalo padri wa roman catholic atafukuzwa kutoka kanisani, ni pale atakapoanza kuombea waumini mapepo na kuanguka kama wanavyofanya kina Mwamposa. Sijajua kwa nini roman catholic hawataki kibisa mapadri kuombea watu mapepo.
 
Wanajua kuombea mapepo na kuanguka ni usanii wa Hali ya juu Sana.
 
Romani Catholic imejengwa katika misingi ya utii wa hali ya juu. Kamwe, si padri Fosudo au askofu atakayefunguka kuhusu sababu za kufukuzwa.

Ila assumptions za kuadhibiwa mapadri wa Roman Catholic huwa ni uzinzi wa wazi wazi, na wizi wa fedha za kanisa uliopindukia. Padri akiwa anachukua fedha kidogo kujihudumia yeye anavumiliwa tu.

Pia, kosa lingine kubwa kabisa ambalo padri wa roman catholic atafukuzwa kutoka kanisani, ni pale atakapoanza kuombea waumini mapepo na kuanguka kama wanavyofanya kina Mwamposa. Sijajua kwa nini roman catholic hawataki kibisa mapadri kuombea watu mapepo.
Hujui kitu wewe wapo mapadre wanaombea watu ila lazima apate kibali kutoka kwa askofu wake.

Sent from my Infinix X665B using JamiiForums mobile app
 
Mpaka ukiona Askofu ametoa huo waraka, basi ujue huyo Padre amefanya kosa ambalo halivumiliki kwa mujibu wa sheria na taratibu za Kanisa.

Hivyo arudi tu nchini kwao. Maana hakuna namna. Sisi wengine tuliona bora tuondoke huko mapema. Maisha ya kuishi kama mseja, fukara, mtii kwa Askofu! Nani angeyaweza. Bora nibakie tu kuwa Mlei muaninifu kwa Kanisa.
 
K
Romani Catholic imejengwa katika misingi ya utii wa hali ya juu. Kamwe, si padri Fosudo au askofu atakayefunguka kuhusu sababu za kufukuzwa.

Ila assumptions za kuadhibiwa mapadri wa Roman Catholic huwa ni uzinzi wa wazi wazi, na wizi wa fedha za kanisa uliopindukia. Padri akiwa anachukua fedha kidogo kujihudumia yeye anavumiliwa tu.

Pia, kosa lingine kubwa kabisa ambalo padri wa roman catholic atafukuzwa kutoka kanisani, ni pale atakapoanza kuombea waumini mapepo na kuanguka kama wanavyofanya kina Mwamposa. Sijajua kwa nini roman catholic hawataki kibisa mapadri kuombea watu mapepo.
Ila hawa Roma huwa siwaelewi kuna mapadri wanao adhiniwa kwa makosa ambayo wengine hawaadhiniwi mfano Padri Bayo wa Jimbo la Pwani Bagamoyo ushahidi wa wazi kabisa upo amezaa na mfanyakazi wake watoto 2 lakini anasalisha na hakuna hatua yoyote alichukuliwa
 
Umejuaje alizaa nae, kama una ushahidi tafadhali fika ofisi ya askofu ukiwa na uthibitisho.
 
Back
Top Bottom