TANZIA Padri wetu mpendwa Ernest Donald Boyo wa Jimbo Kuu la Dar, Afariki Dunia

TANZIA Padri wetu mpendwa Ernest Donald Boyo wa Jimbo Kuu la Dar, Afariki Dunia

Roho za waamini wapate rehema kwa MUNGU wapumzike kwa amani!
 
Kwanini wasisitishe Ibada kwa muda kupisha huu upepo, Jumapili zikifika watu nyomi Kanisani mnataka afe nani ili mjue hali mbaya.
Kwakweli adse hali inatisha mnoo
 
13. Naye Mungu akaendelea kumfanya Mfalme wa Wadanganyika awe na shingo ngumu asiweze hata kung'amua hatari iliyoko mbele yake. 14. Hayo yote yalifanyika ili anguko lake litimie kwa wakati, naam nalo anguko hilo liwe anguko kuu. 15. Hata waliokuwa wakimdanganya mfalme watamcheka na kusema hawakuwa pamoja naye katika maamuzi yake yenye kukosa hekima.
Chato 3:13-15
unataka afanyeje!??
 
Kwanini wasisitishe Ibada kwa muda kupisha huu upepo, Jumapili zikifika watu nyomi Kanisani mnataka afe nani ili mjue hali mbaya.
mpaka ufe wewe na baadhi ya Id's hapa jf ndo tutaamini hali ni tete!!!
 
Chanzo cha kifo hakisemwi!
Kitawekwa wazi tu parokia take au siku ya mazishi take. La muhimu Kanisa katoliki walishatoa waraka wao Kama sijasahau baada ya padri mmoja kufariki huko Bukoba.
 
Mimi sitashabikia tena mihemko ya Tanzia. Watawala wasiogope aibu wakubali wameshakosea wasaidie Wananch vifo ni vingi tena vinahepukika tu.

Mungu atujalie uzima, maisha marefu na afya tulio hai. Awarehemu waliotangulia mbele za haki. Na awafariji na kuwapa nguvu waliofiwa ambao wanapitia wakati mgumu wa majonzi kwa kupoteza wapendwa wao.

Tuzidi kuombeana.
Siku hizi unaandika point!
nini kimekupata Mkaldayo!?
 
View attachment 1699505
Wapendwa Mapadri, Mashemasi, Watawa na taifa lote la Mungu, Kristo.

Kwa masikitiko makubwa napenda kuwataarifu juu ya kifo cha Padri wetu mpendwa Ernest Donald Boyo wa Jimbo Kuu la DSM, aliyekuwa Paroko Msaidizi wa Parokia ya Chang'ombe.

Padri Boyo amefariki leo tarehe 10 Februari 2021 saa 1:30 usiku katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili alipokuwa akitibiwa. Taarifa zaidi juu ya taratibu za Mazishi zinapangwa na tutawataarifu. Tumuombee Pumziko la Milele Mbinguni.

ASANTENI.

+ Jude THADDAEUS Ruwa'ichi
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la DSM
View attachment 1699504
Tunaomba kujua chanzo cha kifo tafadhali
 
13. Naye Mungu akaendelea kumfanya Mfalme wa Wadanganyika awe na shingo ngumu asiweze hata kung'amua hatari iliyoko mbele yake. 14. Hayo yote yalifanyika ili anguko lake litimie kwa wakati, naam nalo anguko hilo liwe anguko kuu. 15. Hata waliokuwa wakimdanganya mfalme watamcheka na kusema hawakuwa pamoja naye katika maamuzi yake yenye kukosa hekima.
Chato 3:13-15
Mkuu umepiga nyundo nzuri sn, dikteta atamaliza watu
 
Back
Top Bottom