Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakuna mahusiano bali vinapingana uchawi ni nguvu nje ya ufahamu kwa muktadha huu jicho la tatu kwa kizungu tungesema ni intruder/mvamizi, wakati bangi ni mmea wenye kufungua ufahamu wa ndani kwa muktadha wa post hii.bangi ina uhusiano gani na uchawi?
aisee Mshana katika ubora (SIO UBORA WA USICHANA) wake![]()
Hutaamini utakachogundua hapa kuhusu paji lako la uso...hapa ndio asili ya neno kipaji ilipatikana..hapa napo ni lango hapa ndio penye njia ya kuingilia mlango wa sita baada ya ile mitano. Hili ni jicho la ndani jicho lisioonekana.lango kuu la kiroho.
Tutaenda kwa mitazamo yote ya kidini na kiimani, kisayansi, kihisia na hata kwenye nguvu za giza.
1. Third Eye - Thalamus - Eye of Horus![]()
Hapa ni kwa mtazamo wa kisayansi nafikiri ni kwenye somo la anatomy kuhusu ubongo, jicho la tatu linaonekana katikati ya ubongo (zingatia katikati) vertebrate brain hapo ndio zinapozalishwa homoni za kulaza au kuamsha hisia maono usingizi nk.
2. Mathematics![]()
Katika ulimwengu wa mahesabu na hesabu, wanamahesabu kwenye ishu za ratio cos na tan watatusaidia hapa.
3. Tahjud (Meditation)
![]()
Kwenye tahajudi wale waliosoma chakra na habari za milango nane, ukiangalia vizuri huo mchoro chakra ya sita ndio ya kuingilia mlango wa sita wa fahamu.
4. Baptism & Sijda![]()
![]()
Kiimani katika ukristo, kwenye ubatizo alama ya msalaba kwenye paji la uso ndio hukamilisha tendo na kuwa Mkristo kamili sasa.. Lakini pia ukisoma kitabu cha ufunuo na habari za kutiwa Muhuri katika paji la uso utafahamu zaidi..
Kwenye Uislam tunajua nini maana na umuhimu wa swala tano na kuthibitisha uchaji wako katika swala tano ni sigida kwenye paji la uso.
5. A kiss on the Forehead
![]()
Kwenye mahusiano busu kwenye paji la uso ni tofauti kabisa na mabusu ya sehemu nyingine yoyote.
6. FREEMASONRY
![]()
Kwenye imani za mpinga Kristo freemason satanism nk alama yao kubwa ni jicho la tatu
7. SEVERE PUNISHMENTS (WATERBOARD)![]()
Kwenye adhabu na mateso mbalimbali paji la uso hutumika kuleta adha ya ajabu mwilini... Mateso ya water board ni mfano mmojawapo. Unalazwa chini unafunikwa kitambaa usoni kisha unamwagiwa maji.. Ni aina ya adhabu isiyoumiza mwili bali inayoumiza hisia.
8. Michezoni:
Kwenye mchezo wa ngumi alama za juu ni zile ambazo zinaangukia kwenye paji la uso.
Nimejaribu kwenda na picha kuokoa ufafanuzi wa maneno mengi... Tunaishi kwenye ulimwengu wa ajabu mno.. Tunashiriki kitu hicho hicho lakini kwa maana matumizi na mitizamo tofauti. Tunafundishwa kutolala chali kuepuka ndoto za mauzauza na majinamizi kumbe siri ni jicho la tatu jicho la maono.
Manabii na watenda miujiza hupenda kuwapuliza ama kuwashika watu penye paji la uso na kifuatacho hapo ni mzinga kama si kupiga kelele... Baadhi ya tiba mbadala hutumia paji la uso kama lango la uponyaji.
Wahindi na wahindu kwenye imani zao hujipaka rangi katikati ya macho kama sehemu ya ibada nk.
Jaribu kutafakari kwa hatua hiki kinachoitwa jicho la tatu, paji la uso, imani yako na maisha yako ya kila siku... Mwishowe tunaweza kujikuta tunaabudu paji la uso kwa muktadha tusiojua.
kwahyo ukivuta bangi unawaonaHakuna mahusiano bali vinapingana uchawi ni nguvu nje ya ufahamu kwa muktadha huu jicho la tatu kwa kizungu tungesema ni intruder/mvamizi, wakati bangi ni mmea wenye kufungua ufahamu wa ndani kwa muktadha wa post hii
Mara zote katika ulimwengu wa kiroho mwenyeji huwa anapokea mgeni anayeendana naye na si yule wanayepingana
Tunapozungumzia jicho la tatu ni lile jicho linaloona tofauti na yale mawili yanayo angalia...! Uchawi ni imitation ya jicho la tatu
Inategemea na imani yako na mafundisho yake lakini haya mambo kwenye imani zetu za Mungu mmoja hayapewi kipaumbele, jicho la tatu linapewa nafasi kubwa kwenye imani zisizoamini katika Mungu na practice mahiri ni tahajudihilo jicho linafunguliwaje..?
Kasinde kwanza chuma ulete ni pepo la kimaskini na halina nguvu kivileSwali nje ya topic Mshana Jr. ... unawezaje kujua kama umefanyiwa chuma ulete kwenye chakula au hela?
Unajinasuaje kwenye chuma ulete?
Back to the topic: hii jicho la tatu linahusiana na maono? Hisia kuwa huyu mtu si mzuri au huyu mtu ni mwema? Au zinahusiana na utambuzi wa mambo?
Kuna kipindi huwa inanitokea niko ndotoni napambana na nguvu ambayo nimeitambua kuwa ni nguvu mbaya au za giza. Jinsi ninvyopambana ile nguvu ya upande wa pili inakuwa inanizidi nguvu kwa kupigana inakuwa ni vuta nikuvute kama mieleka au kukabana.
Mara inanijia sauti anza kusali anza kusali na ukemee usipigane hizo nguvu zitakimbia.....
Naanza kusali na kusali nakemea na kukemea zile nguvu zinakuwa kama zinaishiwa nguvu na zinaanza kujiondoa kwangu na kuweka gap kati yetu. Ila mara zinarudi na kunionesha kuwa haziogopi maombi na kama inakuwa inanishiria niachane na hayo maombi maana hayatasaidia mimi kutoka kwenye zile nguvu za giza.
Ila sauti nyingine hainiombei bali inaniambia sali kwanguvu usimsikilize wala usimuangalie wee sali tuu. Nikiendelea kusali woga unaniisha na najiwa na nguvu zaidi na naendelea kusali.
Sasa ishanitokea mara kwa mara nakuwa nasali kwenye ndoto hadi nastuka nakuwa macho na najikuta niko katikati ya sala na nakuwa sina mamlaka au utashi wa kunyamaza. Naendelea kusali hadi ile nguvu iniishe kisha aidha usingizi utakata kabisa au utanipitia baadae.
Waweza nisaidia hapo kuna lolote ambalo nafunuliwa ila sijalitambua. ..... jicho la rohoni linahusika hapo?
Mimi nikilala chali yaani siwezi kulala kwa amani hadi asubuhi, nitaota ndoto za hatari hatari lakini pia kiuhalisia nitakuwa nahisi kushindana na nguvu fulani waziwazi. Yaani kuna wakati ghafla nasikia usingizi wa lazima na nikisinzia japo dk 10 nahisi kuna nguvu nashindana nayo. Hali hiyo nikilala vinginevyo hunitokea mara chache sana lakini nikilala chali ni lazima itokee.Yeah lakini ni intruder kwakuwa nguvu yake sio kutoka ndani ya nafsi bali nje
Kinacholala/lazwa chali ni maiti tu...tofauti na hapo jicho la tatu kupitia roho inatoa nguvu ya uvutano yenye ukinzani na nguvu nyingine ambazo ni hasiMimi nikilala chali yaani siwezi kulala kwa amani hadi asubuhi, nitaota ndoto za hatari hatari lakini pia kiuhalisia nitakuwa nahisi kushindana na nguvu fulani waziwazi. Yaani kuna wakati ghafla nasikia usingizi wa lazima na nikisinzia japo dk 10 nahisi kuna nguvu nashindana nayo. Hali hiyo nikilala vinginevyo hunitokea mara chache sana lakini nikilala chali ni lazima itokee.
Aaah.. ila ulichoongea hata kibaiolojia ni sawa kabisa. Unajua sehemu ya paji la uso ndipo upande ubongo wa mbele ulipo. No ubungo wa mbele ndo unaotawala mambo mengi kwenye maisha yetu[emoji3] [emoji14] [emoji15] nikadhani na mimi Unazungumzia vipaji ile ya vipawa [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Wewe binafsi ulishawahi kupractice na hilo jicho likafunguka..?Inategemea na imani yako na mafundisho yake lakini haya mambo kwenye imani zetu za Mungu mmoja hayapewi kipaumbele, jicho la tatu linapewa nafasi kubwa kwenye imani zisizoamini katika Mungu na practice mahiri ni tahajudi
waweza kunifundisha na mimi..?To some extent yeah...! Hata sasa nayaona mambo mengi tofauti na wengine waonavyo kuna wakati huwa najistukia na kukaa kimya nikiogopa kuonekana tofauti