Paji la uso na siri ya jicho la tatu

bangi ina uhusiano gani na uchawi?
Hakuna mahusiano bali vinapingana uchawi ni nguvu nje ya ufahamu kwa muktadha huu jicho la tatu kwa kizungu tungesema ni intruder/mvamizi, wakati bangi ni mmea wenye kufungua ufahamu wa ndani kwa muktadha wa post hii.

Mara zote katika ulimwengu wa kiroho mwenyeji huwa anapokea mgeni anayeendana naye na si yule wanayepingana. Tunapozungumzia jicho la tatu ni lile jicho linaloona tofauti na yale mawili yanayo angalia...!

Uchawi ni imitation ya jicho la tatu
 
aisee Mshana katika ubora (SIO UBORA WA USICHANA) wake
 
kwahyo ukivuta bangi unawaona
 
Swali nje ya topic Mshana Jr. ... unawezaje kujua kama umefanyiwa chuma ulete kwenye chakula au hela?

Unajinasuaje kwenye chuma ulete?

Back to the topic: hii jicho la tatu linahusiana na maono? Hisia kuwa huyu mtu si mzuri au huyu mtu ni mwema? Au zinahusiana na utambuzi wa mambo?

Kuna kipindi huwa inanitokea niko ndotoni napambana na nguvu ambayo nimeitambua kuwa ni nguvu mbaya au za giza. Jinsi ninvyopambana ile nguvu ya upande wa pili inakuwa inanizidi nguvu kwa kupigana inakuwa ni vuta nikuvute kama mieleka au kukabana.

Mara inanijia sauti anza kusali anza kusali na ukemee usipigane hizo nguvu zitakimbia.....

Naanza kusali na kusali nakemea na kukemea zile nguvu zinakuwa kama zinaishiwa nguvu na zinaanza kujiondoa kwangu na kuweka gap kati yetu. Ila mara zinarudi na kunionesha kuwa haziogopi maombi na kama inakuwa inanishiria niachane na hayo maombi maana hayatasaidia mimi kutoka kwenye zile nguvu za giza.

Ila sauti nyingine hainiombei bali inaniambia sali kwanguvu usimsikilize wala usimuangalie wee sali tuu. Nikiendelea kusali woga unaniisha na najiwa na nguvu zaidi na naendelea kusali.

Sasa ishanitokea mara kwa mara nakuwa nasali kwenye ndoto hadi nastuka nakuwa macho na najikuta niko katikati ya sala na nakuwa sina mamlaka au utashi wa kunyamaza. Naendelea kusali hadi ile nguvu iniishe kisha aidha usingizi utakata kabisa au utanipitia baadae.

Waweza nisaidia hapo kuna lolote ambalo nafunuliwa ila sijalitambua. ..... jicho la rohoni linahusika hapo?
 
Kasinde kwanza chuma ulete ni pepo la kimaskini na halina nguvu kivile
Pili reply yako hii majibu yake ni mengi na yanajibiwa kwenye post kama nne tofauti nitajitahidi kukuwekea link zake na pengine kuna baadhi ni naamini umezisoma
 
Yeah lakini ni intruder kwakuwa nguvu yake sio kutoka ndani ya nafsi bali nje
Mimi nikilala chali yaani siwezi kulala kwa amani hadi asubuhi, nitaota ndoto za hatari hatari lakini pia kiuhalisia nitakuwa nahisi kushindana na nguvu fulani waziwazi. Yaani kuna wakati ghafla nasikia usingizi wa lazima na nikisinzia japo dk 10 nahisi kuna nguvu nashindana nayo. Hali hiyo nikilala vinginevyo hunitokea mara chache sana lakini nikilala chali ni lazima itokee.
 
Kinacholala/lazwa chali ni maiti tu...tofauti na hapo jicho la tatu kupitia roho inatoa nguvu ya uvutano yenye ukinzani na nguvu nyingine ambazo ni hasi
 
Inategemea na imani yako na mafundisho yake lakini haya mambo kwenye imani zetu za Mungu mmoja hayapewi kipaumbele, jicho la tatu linapewa nafasi kubwa kwenye imani zisizoamini katika Mungu na practice mahiri ni tahajudi
Wewe binafsi ulishawahi kupractice na hilo jicho likafunguka..?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…