Paka kuchukuliwa kama mwanafamilia kwa kutengewa bajeti yake, inakubalika?

FANYENI KAZI NYIE
Hahaha Poland hpo nakumbuka kuna mke wa jamaa mmoja mbongo
Ye dili zake kuuza paka anawauza bei kweli
Kwao kuna mipaka kibao wa kila aina
Wako wenye macho meusi,blue,kijani,nyekundu,njano etc
😂😂

Ova
 

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Na akila vya kupikwa si ndio hawezi kuua panya kabisa
 
Alafu unakuta ndugu yako anakuomba pesa ya chakula au mtaji, unamkazia na kumpa paka msosi
 

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Paka wanajiona sana hao wadudu, wana nyodo za kifala sana. Unaweza mwita akakubinulia midomo akakusonya akaendelea kuangalia tv.

Ila yeye akiwa na shida zake mfano njaa au anataka kitu chochote muda wote miguuni kwako anajipitishapitisha na kujiparaza kama anataka kupigwa ukuni. Nyaaaaaau nyaaaaau nyokololo pumbavu zao..... [emoji34][emoji34][emoji34][emoji34]
 

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 

Hayo maringo ndio uzuri wake
 
Weeeee, wale mabwege wameumbwa na GPS tracking system. Kuna paka tulimtia katika kiroba tukatoka nae tabata st. Mary kule tukaenda mtupa kule kwenye daraja la kinyerezi kiroba kikiwa wazi ili aweze kutoka.

Yule fala wiki kadhaa baadae akarejea tena safari hii akiwa na demu na akaja wakazaa watoto.

Paka wapumbavu sana hawa wanyama [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mbwa siku zote hua ana behave Kama mtumwa lakin Paka yeye anajionaga Don.

Ndo maana wanasema hamna rafiki mzuri Kama mbwa lakin sio li Paka

Mzee umenichekesha, yaani paka anajiona kama Don... mimi kuna siku nilienda Bar moja hivi kula nyama, sasa kuna paka wakaja mmoja anaonekana kibonge hivi, si nikamtupia mfupa ambao kwa kweli ulikuwa na nyama kiasi, akaniangalia akanishusha halafu akasonya, huyoo akaondoka zake akijitingisha.. kwa hiyo nimekuelewa kabisa.. hawana maana.
 
Mi haya madudu yananikera usiku yakianza kugombana, yaani usiku wa manane yanalia kwa sauti kali kinoma, ukiyachungulia unakuta ni jike na dume yanataka kumbotana,
Hivi hawa viumbe hua hawawezi kupigana miti kimyakimya kweli au ndio makusudi tu kukarahishana usiku wa manane.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…