Paka! Ni mnafki sana.
Paka anatumika hata na viumbe visivyoonekana kwa macho.
Nakumbuka kuna tajiri mmoja ( sitamtaja ) ana paka na kuku pale kwenye Yard yake masaki.
Huyo paka kwanza ni mkubwa ki umbo, yaani, yule mpuuzi ana Sofa lake na ana kitanda chake, yule paka amewekewa mfanyakazi.
Jengo ni kubwa sana na Tajiri haishi pale bali pale ana ofisi ndogo mle ndani. Wanaoishi pale ni huyo paka, kuku, njiwa na mfanyakazi.
Maisha ya mule ndani ( Boss Paka ) ukiingia kuna Sofa moja kubwa sana la langi ya dhahabu( sofa hili ni la huyo paka, ole wako ukaenda kukaa atakukata jicho hilo alafu haogopi yaan atawaka apo mpaka utainuka, jikoni yamejaa makopo ya chakula chake na cha kuku. Yaani yule paka ( sijui mm mpaka leo siamini kama kuna paka anayeishi kitajiri kama yule mpuuzi na kwanza mpaka hapa siamini kama ni paka ama Power Bank ya yule Tajiri wa mabasi.
Saa asubuhi anakula Samaki wa mchemsho, mchana kuna mavyakula wanachanganya ni vya kopo na maziwa.
Jioni saa kumi, anakula tena Nyama choma na maziwa, kisha anaenda zake kulala chumbani kwake, paka ni kauzu sana kauzu kupitiliza yaani hataki mgeni mle ndani ana jicho baya kinyama yaani mkiangaliana tu unajua huyu hafurahishwi na ujio wangu.
Saa kumi hiyo pia ni Muda wa kuku na njiwa kula.
Hawa wanapewa mikate 10, mbegu za bangi na mtama..huu mtama ni kilo 5. Kila siku..lakini hii si kesi kesi ipo pale kwa Paka Paka ana roho mbaya sana, nilijaribu kudodosa yule mfanyakazi anasema yule paka kwa sikuanatumia 40 kwenye chakula...
Kwa anayemjua Boss yoyote mwenye mabus ambaye ofisi yake ipo Masaki na Profile yake ktk whatsapp kaweka picha ya Boonge la Paka kuubwa, basi ajue huyo paka anakula elfu 40 kwa Siku, kila siku namaanisha. *****