Pakistan, India wana silaha za nyuklia kwanini Iran ikatazwe?

Pakistan, India wana silaha za nyuklia kwanini Iran ikatazwe?

Wakati wote kichaa mkorofi na asiyetabirika hufungwa minyororo, na huyu ndio Iran.

Vichaa wastaarabu wasiodhuru watu wengine wako huru wanadunda mitaani na kujichanganya na watu wazima bila shida, hawa ndio India na Pakstan wakiwa meza moja na US, UK, GERM, SP, POL, CA, CHN kwa uchache.
 
Mbona dunia haina usawa? Kwanini iwe ni Iran tu na sio nchi nyingine?

Kwanini Iran inapangiwa cha kufanya, kwanini sio nchi nyingine?
Hata mnapoenda polisi kuomba vibali vya kumiliki silaha wengine huwa wanakubaliwa na wengine wanakataliwa, wababe ndiyo wanaamua tena hawaamui kwa haki bali kwa matakwa yao binafsi.
Kama anavyofanya Samia anaamua tu mtu apewe kesi ya uhaini au ya ugaidi ukikubali masharti yake kesi inafutwa unaachiwa huru na chawa wanakutetea(kwa maelekezo maalum kama alivyosafishwa anavyosifiwa Mbowe ambaye waliaminishwa ni gaidi).
 
Umiliki wa silaha za moto mara nyingi huwa unaambatana na upimaji wa afya ya akili mkuu
Hahaha... Kwa hiyo Waajemi hawana akili ama?
Hata ungekuwa wewe jirani yako kichaa akimiliki AK-47 utabaki unamtazama tu mpaka akuwahi akumalize!?, kivyovyote vile Irani hapaswi kumiliki silaha za nuclear ana roho ndogo mno.
Boss nimekuelewa
 
Ni ubabe tu.

Ukiwa huru kifikra huo mtafaruku wao utauelewa, sio wa kidini, sio hizo nuclear weapons wala demokrasia.

US anataka kuidominate middle east na Iran ni kikwazo, almost wote washabow kwake kasoro Iran. Iran ni kama "super power " wa middle east ambae hayuko upande wa west.

Uongozi wake ni wa kiislam na hauwakubali kabisa wamarekani na viongozi wao wakuu wa kidini (shia) washatamka mara kadhaa kutaka kuifuta Israel kabisa.
 
Mbona dunia haina usawa? Kwanini iwe ni Iran tu na sio nchi nyingine?

Kwanini Iran inapangiwa cha kufanya, kwanini sio nchi nyingine?
Hilo swali lako aliwahi kuulizwa Obama, naye akajibu kwa kuuliza:

Hivi ukimwona mtu msenye busara ameshika kisu, unakuwa na wasiwasi wowote? Na vipi ukimwona kichaa ameshika kisu?

Maana ya ujumbe huo:
Iran ni kichaa, akiwa na bomu la nuclear, Dunia nzima itaishi kwenye wasiwasi.
Nakubliana na ukweli kuwa Iran inaongozwa na vichaa. Umeona anachofanya sasa hivi? Iran imeshambuliwa na Marekani na Israel, lakini imerusha makombora ya kushambulia mataifa yote jirani yake. Vipi kama ingekuwa na silaha za nuclear.
 
ndio mfadhili mkuu wa makundi mengi ya kigaidi.

Wakiguswa hata kidogo wanashambulia hovyo hovyo hadi majirani zao ambao hawahusiki, kisa tu wana kambi za adui,

Walishaapa wakija kupata nuclear, jambo la kwanza kabisa ni kuilipua Israel.
 
Back
Top Bottom