cupvich
JF-Expert Member
- Aug 2, 2022
- 408
- 247
Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la watoto wa kike hususan wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kunyanyaswa kingoni ikiwa ni pamoja na Kuingiliwa kimwili (KUBAKWA) hadi kupelekea kukatisha masomo yao kutokana na kubeba Mimba na kuathirika kisaikolojia jambo ambalo linahatarisha usalama wao.
Ripoti ya Mwaka ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2021/22 ilibaini kuwa kati ya Mwaka 2015 na 2021 Katika halmashauri 11 zilizofanyiwa ukaguzi wanafunzi 19,945 sawa na asilimia 25 kati ya 78,786 waliosajiliwa mwaka 2015 hawakuhitimu Darasa la saba. Pia ukaguzi ulibaini kuwa Katika mamlaka 19 za Serikali za mitaa; wanafunzi 22,039 sawa na asilimia 28 kati ya 82,236 waliojiunga na kidato Cha kwanza mwaka 2018 hawakufanikiwa kufanya Mtihani wa Kupata cheti Cha kuhitimu kidato Cha nne. huku Sababu mojawapo ikitajwa kuwa ni UJAUZITO kwa watoto wa kike. (Ripoti ya CAG ukurasa wa 119-120).
(Chanzo; Ripoti ya CAG 2021/22)
Mbaya zaidi matendo haya ya ubakaji dhidi ya watoto wa kike yamekuwa yakifanywa na watu wa karibu ambao wangeweza kuwa walinzi juu ya usalama wa mtoto wa kike awapo Nyumbani, Katika nyumba za Ibada, Shuleni hata Mtaani. Hali hii imepekea mtoto wa kike kutokuwa salama. kadri Siku zinavyokwenda ndivyo matukio maovu dhidi ya ukatili wa mtoto wa kike yanaongezeka na Kuhatarisha usalama wake. Je usalama wa mtoto wa kike Uko wapi?
JE, NI NYUMBANI PALIPO SALAMA KWA MTOTO WA KIKE?
Si ajabu Katika Karne hii ya ishirini na Moja kusikia BABA mzazi amembaka mtoto wake wa kumzaa. Ndugu wengine kama vile BABU, MJOMBA na BINAMU wamekuwa wakihusika Katika matukio haya maovu hali inayoleta taswira mbaya Katika Jamii yetu. Matukio haya yameendelea kushika kasi Kila kukicha Kiasi cha Kuhatarisha usalama wa mtoto wa kike awapo Nyumbani. Ni wapi palipo salama Kwa mtoto wa kike?
(Picha kutoka mtandaoni)
JE, NI SHULENI PALIPO SALAMA KWA MTOTO WA KIKE?
Miongoni Mwa sehemu ambazo Jamii inaamini mtoto anaweza akawa salama na kufundishwa maadili mema ni shuleni. Lakini Hali imekuwa tofauti, Kesi nyingi zinazohusisha walimu ambao ni walezi wa watoto kuwabaka hadi kuwapatia ujauzito watoto wa kike zimeripotiwa karibia Katika Kila pembe ya nchi yetu, Tena matukio mengine yamekuwa yakifanyika Katika mazingira ya shuleni. jambo ambalo limechafua taasisi hii muhimu Katika Maendeleo ya nchi yetu. Ni wapi palipo salama kwa mtoto wa kike?
(picha kutoka mtandaoni)
JE, NI KATIKA NYUMBA ZA IBADA PALIPO SALAMA KWA MTOTO WA KIKE?
Hii inaweza kuwa ajabu kidogo lakini ndio uhalisia. Nyumba za Ibada makanisani na misikitini, mahali ambapo tunaamini kuwa ni sehemu takatifu Kwa ajili ya watu kukutana na Mungu wao na kujitakasa imekuwa sio salama tena Kwa mtoto wa kike. Baadhi ya Watumishi wa Mungu wametumia nafasi zao Katika makanisa na Misikiti au madrasa kuwarubuni watoto na kufikia hatua ya kuwabaka na kuwapa ujauzito hali iliyopelekea kukatisha masomo yao. Ni wapi palipo salama Kwa mtoto wa kike?
(picha kutoka mtandaoni)
JE, NI KATIKA MITAA NA MIJI PALIPO SALAMA KWA MTOTO WA KIKE?
Mtoto wa kike hayuko salama hata Katika mitaa na miji anayoishi, anapokuwa njiani akienda shuleni au kutoka, anapokwenda kuchota maji, anapokuwa Katika usafiri, anaenda kutafuta kuni hayuko salama hata kidogo.watu ambao ndio wangekuwa walinzi wake, wamegeuka kuwa katili Katika kumtendea maovu. Kesi za Ubakaji zimekuwa nyingi Kila mahali Kiasi cha Kuhatarisha usalama wa mtoto wa kike. Ni wapi palipo salama Kwa mtoto wa kike?
(picha kutoka mtandaoni)
JE, NI KATIKA VYOMBO VYA SHERIA PALIPO SALAMA KWA MTOTO WA KIKE?
Tunaamini kuwa vyombo vya Sheria ni mahali ambapo haki inaweza kupatikana. Lakini imekuwa tofauti Kwa baadhi ya mamlaka za Sheria kuwaachia huru watuhumiwa wa Ubakaj, kutokana na Baadhi ya Watumishi wa vyombo hivi vyenye Kutoa haki kujihusisha na vitendo vya Rushwa. Hali inayowafanya wananchi kukosa Imani kabisa na vyombo vyao vya Sheria. Tunatarajia Mahakama na vyombo vingine vya sheria kutenda haki Kwa Kutoa adhabu Kali Kwa wale wanao jihusisha na ukatili dhidi ya watoto wa kike Ili iwe fundisho Kwa wengine. Ni wapi palipo salama Kwa mtoto wa kike?
(picha kutoka mtandaoni)
TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO INAVYOWEZA KUINGILIA KATI USALAMA WA MTOTO WA KIKE.
Imefika wakati Sasa teknolojia ya habari na mawasiliano isaidie Katika ulinzi na usalama wa mtoto wa kike Ili Kupunguza vitendo vya ukatili kama vile Ubakaji. Kupitia mradi wa huduma ya simu, mradi unaofadhiliwa na shirika la umoja wa mataifa la idadi ya watu UNFPA Tanzania namba maalumu 116 inayotumiwa Bure Kutoa taarifa za matukio ya unyanyasaji Kwa mtoto ilizinduliwa na hivyo kuwa msaada wa kupambana na ukatili dhidi ya watoto nchini Tanzania.
Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, jinsia, wanawake na makundi maalum chini ya waziri mwenye dhamana mhe Dkt. Dorothy Gwajima haina budi kuboresha njia hii ya matumizi ya Simu maalumu Katika Kutoa taarifa za vitendo vya ukatili dhidi ya watoto wa kike. Namba hiyo ipatikane masaa yote 24, na iwe Bure Katika kupiga au kutuma ujumbe mfupi. Namba hii maalumu ipatikane Katika taasisi zote za Serikali na zisizo za serikali kama vile Mashuleni, Vyuoni, Katika vyombo vya usafiri, Katika nyumba za Ibada, Maofisini, Nyumba za kulala wageni, na Majumbani.
Mwisho, Ili teknolojia hii ya habari na mawasiliano iweze kumlinda mtoto wa kike dhidi ya ukatili wa kijinsia, Serikali haina budi Kutoa elimu ya kutosha juu ya matumizi ya namba maalumu Kwa ajili ya kutolea taarifa, hivyo Kila mwananchi awe na namba hiyo na ashiriki kikamilifu Katika kuripoti matukio ya ukatili pale anapoona Viashiria vya vitendo vya ukatili wa mtoto wa kike mahali popote pale. Vilevile Serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama kuimarisha usalama Kwa mtoa taarifa. Kupitia njia hii ya teknolojia ya habari na mawasiliano sote Kwa pamoja tutaweza kumlinda mtoto wa kike dhidi ya vitendo vya ukatili na kumuwezesha kutimiza ndoto zake.

Attachments
Upvote
10