Pale Nilipoamua kuwanyoosha watu wa kukopesha mtandaoni

H Hii utaona athari yake Kama utaamua kwenda kukopa bank
 
Yes. Kampuni Moja ina app nyingi.
Vipi hawajakuabisha tena kwa kutumia jumbe kwa ndugu kama awali?
 
Acha uongo wako, nadaiwa mpesa 99k zaidi ya miezi sita na tigopesa 145k zaidi ya miezi miwili, mwezi uliopita nimekopa NMB na hawajaniuliza lolote kuhusu hiyo mikopo
 
Hiyo mikopo si huwa ina terms?

Na hizo namba si uliweka wewe?

Usingependa hizo disturbances usingechukua mkopo.

Pengine huo mkopo ungeweza kuupata kwa mtu wako wa karibu na ukawa umeepuka hizo kero.
Mzee mkopo kwangu ni msaada kwao ni biashara,kitu kitakachovunja uhusiano kati ya hivyo viwili ni kwenda kinyume na makubaliano.

Mteja kajaza wadhamini 3 kwa majina na namba zao za simu.

Kachelewa kulipa kama mlivyokuwa mmekubalina ktk term and condition,wanatakiwa wajulishwe wadhamini kwa adabu.

Kampuni inaamua kutuma sms kwa watu 780 wa kwenye contact na call history.yaani mteja kakiuka makubaliano siku moja anafanyiwa unyanyasaji mkubwa hivi,anachotakiwa ni kulalamika au kuacha wajipatie pesa yao kwa hao wati 780πŸ˜†πŸ˜†.

Biashara za mikopo ni taaluma ya watu na ina kanuni zake,isipokuwa wahuni wa kausha damu wameivamia kichwa kichwa,kinachofata ni kuchoma mitaji tu.
 
Sina mda wa kubishana mzee endelea kudanganya mwenzio pengine na wewe unadaiwa unajifariji kwakua umepanga kutokulipa
Nabishana au nakujibu?
Ndiyo nadaiwa na swala la kulipa sio leo au kesho, ila uhalisia ni kwamba nimekopa nmb nikiwa nadaiwa na tigo na voda.
Na hawajawahi kuniuliza hayo madeni zaidi ya kukagua vitu vyao muhimu na mimi kupeleka nyaraka muhimu.
 
Kwani jamaa kapost kuomba ushauri?
 
MKUU Pesa (hadhina) inaongea sauti kubwa sana kuliko chochote kitoacho sauti


MKUU Pesa ambayo Sio Yako na uliyoichukua kwa makubaliano ya kuiludisha hata kama ni 1000 Mkuu hakika Sio nzuri ni hatia Bora hata iwe ya ndugu


Mithali 26:2

"Kama shomoro katika kutanga-tanga kwake, Na kama mbayuwayu katika kuruka kwake; Kadhalika laana isiyo na sababu haimpigi mtu"



Kadhalika laana isiyo na sababu haimpigi mtu πŸ‘‰ sasa wenzako wanayo sababu umechukua hadhina (Pesa) yao na hutaki kuludisha lolote watakalotamka juu Yako
Litakua b'se una hatia(sababu)



"Hadhina ya MTU ilipo na moyo wake ndipo ulipo" πŸ‘‰ pay theirs money n gonna be Free
 
Upo nchi gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…