Pale Nilipoamua kuwanyoosha watu wa kukopesha mtandaoni

Pale Nilipoamua kuwanyoosha watu wa kukopesha mtandaoni

Mzee Mimi sikutishi uliza watu na hii sio Kwa hao tu Hadi kampuni za simu kitendo Cha kukopa halafu ukavunja laini Yako ya simu na umesajili Kwa nida deni lako linabaki milele na riba inapanda siku ukienda kuomba mkopo bank wataangalia record zako kwenye Kila sehemu ndio upewe mkopo na hap jamaa huwa wanapeleka record za watu wasiolipa bank sababa hayo makampuni upande wa mikopo yanadhaminiwa na bank hao sio wajinga mpaka wakopeshe pesa mtandaoni
We jamaa mbona muongo sana? Branch waliniletea za kuleta nikawaacha kuwalipa 150k mwaka 2019! Toka hapo nimekopa CRDB more than 3 time mkopo na top up 2 si chini ya million 40! Wewe hizi stori zako umezitoa wapi nyasubi?
 
Mzee mkopo kwangu ni msaada kwao ni biashara,kitu kitakachovunja uhusiano kati ya hivyo viwili ni kwenda kinyume na makubaliano.

Mteja kajaza wadhamini 3 kwa majina na namba zao za simu.

Kachelewa kulipa kama mlivyokuwa mmekubalina ktk term and condition,wanatakiwa wajulishwe wadhamini kwa adabu.

Kampuni inaamua kutuma sms kwa watu 780 wa kwenye contact na call history.yaani mteja kakiuka makubaliano siku moja anafanyiwa unyanyasaji mkubwa hivi,anachotakiwa ni kulalamika au kuacha wajipatie pesa yao kwa hao wati 780😆😆.

Biashara za mikopo ni taaluma ya watu na ina kanuni zake,isipokuwa wahuni wa kausha damu wameivamia kichwa kichwa,kinachofata ni kuchoma mitaji tu.
Kampuni imekupa mkopo kwa mfumo ambao sio physically kwa maana haukufika ofisini.

HIyo ni njia inayowapa urahisi sana matapeli kutekeleza mipango yao ya kudhulumu pesa.

Kwasababu kampuni haijui background zako kama wewe una rekodi za utapeli au ni mtu muungwana, na pia ukumbuke kampuni haijui wapi unaishi ili pengine waweze kukufuata ili hatua za huo ustaarabu zitumike.

Hivi katika mazingira hayo unadhani njia ipi ilikuwa ni sahihi kama kampuni kuifanya ili kuhakikisha watu wanarejesha pesa bila kampuni kufilisika?

Kwasababu kwenye hiyo option ya kuweka namba 3 kumbuka upo uwezekano wa tapeli kutumia namba za watu ambao hawapatikani hewani au ni namba ambazo kazisajili yeye ili tu afanikishe jambo lake naada ya hapo line zinatiwa kapuni.

Haya sasa jiweke wewe kwenye hiyo nafasi ya huyo anayekudai, umepewa namba 3 halafu zote ukipiga zimefungiwa na kuna namba nyingine unaziona utaacha kuzitumia?
 
Mzee Mimi sikutishi uliza watu na hii sio Kwa hao tu Hadi kampuni za simu kitendo Cha kukopa halafu ukavunja laini Yako ya simu na umesajili Kwa nida deni lako linabaki milele na riba inapanda siku ukienda kuomba mkopo bank wataangalia record zako kwenye Kila sehemu ndio upewe mkopo na hap jamaa huwa wanapeleka record za watu wasiolipa bank sababa hayo makampuni upande wa mikopo yanadhaminiwa na bank hao sio wajinga mpaka wakopeshe pesa mtandaoni
MATANGOPORI
 
Mi sio tapeli tuheshimiane ila ndg Zangu wamedhalilishwa acha waliwe
Wangelipa yasingewakuta hayo yaliyowakuta.

Watu wanapenda hela za kitonga, kwenye mikopo ukiwasetia huo mwanya bila kuweka masharti utadhalilika wewe.

Kulikuwa na kampuni la TALA hapa Tanzania, lilifunga ofisi zao na humu upo uzi ambao watu walikuwa wakipongezana jinsi walivyowatapeli.

Kutapeli hela ya mwingine sio ushujaa. Aliyekupa mkopo ambao ulienda kukusaidia kutatua tatizo lako hakutakiwa kuwa treated namna hiyo.

Kwa kuamua kutolipa mkopo kwasababu umeona njia iliyotumika kupewa mkopo ni rahisi isyokubana unakuwa unawakatili wengine ambao hawana tabia kama yako na wanatumia hiyo mikopo ku solve mambo yao.
 
Sidhani kama unawakomoa, kikawaida huyo anakua na wateja zaidi ya 200 wakuawafanyia kazi mpaka wengine ngumj kawafikia wewe hata ufanye lolote kwake haina shida.

Kuna dada alikuwa anafanya namsadia kutuma sms kwenye PC yangu wateja 800 anawatumia sms ukijibizananae baada ya dakika hata akukumbuki.
Ilishawah nitokea. Baada ya yeye kunipigia akanikosa nikamtafuta akaniuliza ww ni na ni vile
 
😛 😛hao branch..nilikopa 18,000 nilichukua mwaka mzima kuwalipa..looh!, meseji zao zikawa zinanijazia simu tu ...nilipoipata nikawalipa yote, ila wanasumbua haloo...usiombe ukwame uchelewe kuwalipa..utakeleka sana...hadi leo sihitaji kukopa kwa mtu😀🙁
 
Mzee Mimi sikutishi uliza watu na hii sio Kwa hao tu Hadi kampuni za simu kitendo Cha kukopa halafu ukavunja laini Yako ya simu na umesajili Kwa nida deni lako linabaki milele na riba inapanda siku ukienda kuomba mkopo bank wataangalia record zako kwenye Kila sehemu ndio upewe mkopo na hap jamaa huwa wanapeleka record za watu wasiolipa bank sababa hayo makampuni upande wa mikopo yanadhaminiwa na bank hao sio wajinga mpaka wakopeshe pesa mtandaoni
Uongoo me nilisajilia namba ya mama na ni kawa nimepoka tigo Hadi kufikia laki kwa laini zangu mbili. Hapo kati ni kawa mzito kulipa... So line ikawa na Deni kubwa tu mbona mama alienda nmb kukopa wakamkopesha M 10 bila tatizo lolote. Alaf ile line badae sana nikawa nikiiweka hela wala hawakati tena lile deni
 
MKUU Pesa (hadhina) inaongea sauti kubwa sana kuliko chochote kitoacho sauti

MKUU Pesa ambayo Sio Yako na uliyoichukua kwa makubaliano ya kuiludisha hata kama ni 1000 Mkuu hakika Sio nzuri ni hatia Bora hata iwe ya ndugu

Mithali 26:2

"Kama shomoro katika kutanga-tanga kwake, Na kama mbayuwayu katika kuruka kwake; Kadhalika laana isiyo na sababu haimpigi mtu"

Kadhalika laana isiyo na sababu haimpigi mtu 👉 sasa wenzako wanayo sababu umechukua hadhina (Pesa) yao na hutaki kuludisha lolote watakalotamka juu Yako
Litakua b'se una hatia(sababu)

"Hadhina ya MTU ilipo na moyo wake ndipo ulipo" 👉 pay theirs money n gonna be Free
Na wewe haiitwi hadhina ni hazina bwana
Hawa wapare bwana
 
Uongoo me nilisajilia namba ya mama na ni kawa nimepoka tigo Hadi kufikia laki kwa laini zangu mbili. Hapo kati ni kawa mzito kulipa... So line ikawa na Deni kubwa tu mbona mama alienda nmb kukopa wakamkopesha M 10 bila tatizo lolote. Alaf ile line badae sana nikawa nikiiweka hela wala hawakati tena lile deni
Dada dawa ya deni kulipa usijifariji siku ukikanyaga bank ndio utajua najua unajifariji
 
Dada dawa ya deni kulipa usijifariji siku ukikanyaga bank ndio utajua najua unajifariji
We nae Acha kuhemkwa soma uelewe. Namba iliyokopea tigo ilisajiliwa kwa NIDA ya mama. Baada mama alienda bank nmb kukopa na alipewa mkopo.
So Acha kuongea uongo hayo Mambo yako mambeleziii
 
We nae Acha kuhemkwa soma uelewe. Namba iliyokopea tigo ilisajiliwa kwa NIDA ya mama. Baada mama alienda bank nmb kukopa na alipewa mkopo.
So Acha kuongea uongo hayo Mambo yako mambeleziii
Narudia tena dawa ya deni kulipa lipia deni la watu Hilo hamna vya bure duniani yaani unaweka namba ya nida halafu upate mkopo unachekesha wewd
 
Samahani, jifunze matumizi sahihi ya mtandao.

Pori la katavi bado kubwa, huwezi jua unadeal na kina nani na wanaweza kureact vipi, mimi nimesikia tu huruma maana unaweza kuwa ni kijana mdogo ambaye bado una safari ndefu maishani.

Hata hivyo hao watoa mikopo wakatazwe mara 1 kufanya huo uhuni wa kusambaza taarifa ya mkopaji wao.
Kwamba pori la katavi bado kubwa..? Hahahah
 
Back
Top Bottom