Pale Nilipoamua kuwanyoosha watu wa kukopesha mtandaoni

Pale Nilipoamua kuwanyoosha watu wa kukopesha mtandaoni

Binafsi sio tapeli ila nikiri kwamba niliamua kuwanyoosha hawa wakopeshaji wa mtandaoni baada ya mmoja wao kunichafua,

Nilikuwa mkopaji mzuri wa app fulani jina nalihifadhi nikilipa walikuwa wananiomba nikope tena na tena basi kwangu ikawa kama mazoea kopa lipa

Tabu na mateso vilianza pale niliposhindwa rejesha pesa yao kwa wakati tena hata wiki haikufika lakini chamoto nilikiona, nilipokea meseji za watu nnaowaheshimu ikiwemo wazazi kuwa natangazwa mimi tapeli na nimewaweka wao kama wadhamini, nikaja kujua ni wale watu wa app wanatumia namba za watu wangu wakati sikuwapa hizo namba,

Kweli linichukizwa sana na nikaamua sasa kama mbwai iwe mbwai liwalo na liwe siwalipi na nikaamua sasa nilkope app zote niwaonyeshe kazi kuna app walizonipa kuna app walinitosa mana nilichukua hata kama ni buku 7 twende 😁😁.

Usiulize nilikuwa napigiwa simu ngapi kwa siku.
Wajinga sana Hawa watu!
 
Mzee mkopo kwangu ni msaada kwao ni biashara,kitu kitakachovunja uhusiano kati ya hivyo viwili ni kwenda kinyume na makubaliano.

Mteja kajaza wadhamini 3 kwa majina na namba zao za simu.

Kachelewa kulipa kama mlivyokuwa mmekubalina ktk term and condition,wanatakiwa wajulishwe wadhamini kwa adabu.

Kampuni inaamua kutuma sms kwa watu 780 wa kwenye contact na call history.yaani mteja kakiuka makubaliano siku moja anafanyiwa unyanyasaji mkubwa hivi,anachotakiwa ni kulalamika au kuacha wajipatie pesa yao kwa hao wati 780😆😆.

Biashara za mikopo ni taaluma ya watu na ina kanuni zake,isipokuwa wahuni wa kausha damu wameivamia kichwa kichwa,kinachofata ni kuchoma mitaji tu.
Kuna report ya BBC ilikuwa published mwaka jana, vifo vingi vya kujinyonga huko kwao vinasababishwa na hawa watu. Ni takataka.
 
Kama kawaida ya wabongo, uaminifu sifuri kabisa.

Si ulisoma terms and conditions na ukakubaliana nazo, kwanini usiwalipe sasa??

Wabongo uaminifu F, wachina nao unyonyaji A+, kigongo hapoo.

Na wanaokuchafua hivyo ni watoto wa buku 2, ndo wengi wameajiliwa kwa kazi hiyo, hawana uIT wowote.
 
Mzee mkopo kwangu ni msaada kwao ni biashara,kitu kitakachovunja uhusiano kati ya hivyo viwili ni kwenda kinyume na makubaliano.

Mteja kajaza wadhamini 3 kwa majina na namba zao za simu.

Kachelewa kulipa kama mlivyokuwa mmekubalina ktk term and condition,wanatakiwa wajulishwe wadhamini kwa adabu.

Kampuni inaamua kutuma sms kwa watu 780 wa kwenye contact na call history.yaani mteja kakiuka makubaliano siku moja anafanyiwa unyanyasaji mkubwa hivi,anachotakiwa ni kulalamika au kuacha wajipatie pesa yao kwa hao wati 780😆😆.

Biashara za mikopo ni taaluma ya watu na ina kanuni zake,isipokuwa wahuni wa kausha damu wameivamia kichwa kichwa,kinachofata ni kuchoma mitaji tu.
Kaa kitaalamu wewe, ishi kwa codes.

Kopa lipa, kopa lipa, kopa lipa, kopa lipa, kopa lipa, kopa lipa, KOPA SEPA.
 
Sawa kama hutarajii kukopa bank za tanzania maisha Yako yote sawa ila kama utahitaji kukopa Kaa ukijua hao jamaa washapeleka record zako sababu uliweka nida watanzania wengi hawajui hii kitu na hayo madeni yanapanda Kwa riba Kila mda mliokubaliana
Hakuna mikopo ya simu inayopelekwa credit info, inayopelekwa ni Timiza, Songesha
 
Samahani, jifunze matumizi sahihi ya mtandao.

Pori la katavi bado kubwa, huwezi jua unadeal na kina nani na wanaweza kureact vipi, mimi nimesikia tu huruma maana unaweza kuwa ni kijana mdogo ambaye bado una safari ndefu maishani.

Hata hivyo hao watoa mikopo wakatazwe mara 1 kufanya huo uhuni wa kusambaza taarifa ya mkopaji wao.
 
binafsi nimepata hela na hakuna walichofanya nikipiga hesabu nna zaidi ya laki nne nilizokopa hawa fini ndio walikuwa wa mwisho niliwaosha kweli kweli na nilichogundua kampuni moja ina app zaidi ya 3 kudai kukopa ila kudai madeni wanatumia jina kampuni mfano pesa x na cash x ni wale wale tu.
Ungejua kama hizo kampuni kuna Amount ya pesa wameiweka tu just kwa watu wanokopa mara ya kwanza na kulimbia tu usingeona kama umewakomoa.

Maelfu ya watu kama wewe wanakopa na kukimbia mara ya kwanza ila jua kuna Malawi ya watu ambao wanakopa na kulipa. Ni sula la mahesabu zaidi.

wao kukukopesha wanafanya RISK na wanajua kuna wataokimbia na kuna watakao endelea wao target yao wanaoendelea.
 
Back
Top Bottom