Pale Nilipoamua kuwanyoosha watu wa kukopesha mtandaoni

Pale Nilipoamua kuwanyoosha watu wa kukopesha mtandaoni

Wangelipa yasingewakuta hayo yaliyowakuta.

Watu wanapenda hela za kitonga, kwenye mikopo ukiwasetia huo mwanya bila kuweka masharti utadhalilika wewe.

Kulikuwa na kampuni la TALA hapa Tanzania, lilifunga ofisi zao na humu upo uzi ambao watu walikuwa wakipongezana jinsi walivyowatapeli.

Kutapeli hela ya mwingine sio ushujaa. Aliyekupa mkopo ambao ulienda kukusaidia kutatua tatizo lako hakutakiwa kuwa treated namna hiyo.

Kwa kuamua kutolipa mkopo kwasababu umeona njia iliyotumika kupewa mkopo ni rahisi isyokubana unakuwa unawakatili wengine ambao hawana tabia kama yako na wanatumia hiyo mikopo ku solve mambo yao.
Sahihi kabisa Off-sir
 
Sawa kama hutarajii kukopa bank za tanzania maisha Yako yote sawa ila kama utahitaji kukopa Kaa ukijua hao jamaa washapeleka record zako sababu uliweka nida watanzania wengi hawajui hii kitu na hayo madeni yanapanda Kwa riba Kila mda mliokubaliana
Hakuna benki itamnyima mkopo mteja wake kisa hawa wapuuzi. Acha uzwazwa dogo.
 
Binafsi sio tapeli ila nikiri kwamba niliamua kuwanyoosha hawa wakopeshaji wa mtandaoni baada ya mmoja wao kunichafua,

Nilikuwa mkopaji mzuri wa app fulani jina nalihifadhi nikilipa walikuwa wananiomba nikope tena na tena basi kwangu ikawa kama mazoea kopa lipa

Tabu na mateso vilianza pale niliposhindwa rejesha pesa yao kwa wakati tena hata wiki haikufika lakini chamoto nilikiona, nilipokea meseji za watu nnaowaheshimu ikiwemo wazazi kuwa natangazwa mimi tapeli na nimewaweka wao kama wadhamini, nikaja kujua ni wale watu wa app wanatumia namba za watu wangu wakati sikuwapa hizo namba,

Kweli linichukizwa sana na nikaamua sasa kama mbwai iwe mbwai liwalo na liwe siwalipi na nikaamua sasa nilkope app zote niwaonyeshe kazi kuna app walizonipa kuna app walinitosa mana nilichukua hata kama ni buku 7 twende 😁😁.

Usiulize nilikuwa napigiwa simu ngapi kwa siku.
😂😂😂
 
Mkuu nimeona namba moia ninayoifahamu ni rafiki wa karibu kabisa na umeianika
Sio vizuri.Kama umeamua kutokulipa sawa ni wewe na roho yako ila kuweka namba za watu hadharani sio.Wanaodai japo wanatumia njia sizo lakini pia na wewe una makosa kupost namba zao.
Acha wenge. Hizo namba ni za kampuni na zinapigiaga simu kudai madeni. Hata mi zilinipigia hizo so hakuna kuingilia privacy ya mtu hapo.
 
si namba zao za ofisi ukitaka kukopa wacheki
Mi kuna siku niliona tangazo la app ya pesa X. Nikadownload ile app, then nikaingiza namba yangu ya simu alafu nika iunstall baada ya kujua kuwa ni kampuni za kukopesha.

Baada ya muda naona nimepokea 4750 toka Dex nini sijui. Ikabidi niisearch hiyo kampuni, nikawatambua so nikaamua niwatafute kwenye mitandao yao ya kijamii.

Huko nikawaambia naona mmenitumia pesa wakati sijaomba. Niwarudishie pesa yenu wakauchuna. Baada ya wiki simu zikaanza na deni juu. Sijawahi lipa ile pesa yao hadi leo.
 
Hiyo mikopo si huwa ina terms?

Na hizo namba si uliweka wewe?

Usingependa hizo disturbances usingechukua mkopo.

Pengine huo mkopo ungeweza kuupata kwa mtu wako wa karibu na ukawa umeepuka hizo kero.
namba sijawapa na sio za wadhamini niliowaweka
 
Back
Top Bottom