Pale Nilipoamua kuwanyoosha watu wa kukopesha mtandaoni

Pale Nilipoamua kuwanyoosha watu wa kukopesha mtandaoni

H
Binafsi sio tapeli ila nikiri kwamba niliamua kuwanyoosha hawa wakopeshaji wa mtandaoni baada ya mmoja wao kunichafua,
nilikuwa mkopaji mzuri wa app fulani jina nalihifadhi nikilipa walikuwa wananiomba nikope tena na tena basi kwangu ikawa kama mazoea kopa lipa

Tabu na mateso vilianza pale niliposhindwa rejesha pesa yao kwa wakati tena hata wiki haikufika lakini chamoto nilikiona,
nilipokea meseji za watu nnaowaheshimu ikiwemo wazazi kuwa natangazwa mimi tapeli na nimewaweka wao kama wadhamini, nikaja kujua ni wale watu wa app wanatumia namba za watu wangu wakati sikuwapa hizo namba,

kweli linichukizwa sana na nikaamua sasa kama mbwai iwe mbwai liwalo na liwe siwalipi na nikaamua sasa nilkope app zote niwaonyeshe kazi kuna app walizonipa kuna app walinitosa mana nilichukua hata kama ni buku 7 twende 😁😁.

usiulize nilikuwa napigiwa simu ngapi kwa siku.
Hii utaona athari yake Kama utaamua kwenda kukopa bank
 
binafsi nimepata hela na hakuna walichofanya nikipiga hesabu nna zaidi ya laki nne nilizokopa hawa fini ndio walikuwa wa mwisho niliwaosha kweli kweli na nilichogundua kampuni moja ina app zaidi ya 3 kudai kukopa ila kudai madeni wanatumia jina kampuni mfano pesa x na cash x ni wale wale tu.
Yes. Kampuni Moja ina app nyingi.
Vipi hawajakuabisha tena kwa kutumia jumbe kwa ndugu kama awali?
 
Mzee Mimi sikutishi uliza watu na hii sio Kwa hao tu Hadi kampuni za simu kitendo Cha kukopa halafu ukavunja laini Yako ya simu na umesajili Kwa nida deni lako linabaki milele na riba inapanda siku ukienda kuomba mkopo bank wataangalia record zako kwenye Kila sehemu ndio upewe mkopo na hap jamaa huwa wanapeleka record za watu wasiolipa bank sababa hayo makampuni upande wa mikopo yanadhaminiwa na bank hao sio wajinga mpaka wakopeshe pesa mtandaoni
Acha uongo wako, nadaiwa mpesa 99k zaidi ya miezi sita na tigopesa 145k zaidi ya miezi miwili, mwezi uliopita nimekopa NMB na hawajaniuliza lolote kuhusu hiyo mikopo
 
Hiyo mikopo si huwa ina terms?

Na hizo namba si uliweka wewe?

Usingependa hizo disturbances usingechukua mkopo.

Pengine huo mkopo ungeweza kuupata kwa mtu wako wa karibu na ukawa umeepuka hizo kero.
Mzee mkopo kwangu ni msaada kwao ni biashara,kitu kitakachovunja uhusiano kati ya hivyo viwili ni kwenda kinyume na makubaliano.

Mteja kajaza wadhamini 3 kwa majina na namba zao za simu.

Kachelewa kulipa kama mlivyokuwa mmekubalina ktk term and condition,wanatakiwa wajulishwe wadhamini kwa adabu.

Kampuni inaamua kutuma sms kwa watu 780 wa kwenye contact na call history.yaani mteja kakiuka makubaliano siku moja anafanyiwa unyanyasaji mkubwa hivi,anachotakiwa ni kulalamika au kuacha wajipatie pesa yao kwa hao wati 780😆😆.

Biashara za mikopo ni taaluma ya watu na ina kanuni zake,isipokuwa wahuni wa kausha damu wameivamia kichwa kichwa,kinachofata ni kuchoma mitaji tu.
 
Sina mda wa kubishana mzee endelea kudanganya mwenzio pengine na wewe unadaiwa unajifariji kwakua umepanga kutokulipa
Nabishana au nakujibu?
Ndiyo nadaiwa na swala la kulipa sio leo au kesho, ila uhalisia ni kwamba nimekopa nmb nikiwa nadaiwa na tigo na voda.
Na hawajawahi kuniuliza hayo madeni zaidi ya kukagua vitu vyao muhimu na mimi kupeleka nyaraka muhimu.
 
Kudhulumu pesa ya mtu sio ujanja

Wala kupost screenshots za wadai wako ambazo zinaonesha majibu ya kejeli ukiwavimbia wanapokuhimiza ulipe deni lao.

Guys hiyo sio right move kwa mtu ambaye ni smart.

Labda itakuwa ni ishu ya makuzi tu, ila mimi binafsi yangu siwezi kuwa na amani kabisa kudhulumu pesa ya mtu mwingine ambaye alikuwa na intention njema ya kunisaidia kwa kuniazima pesa ili niweze kutatua changamoto zangu.
Kwani jamaa kapost kuomba ushauri?
 
MKUU Pesa (hadhina) inaongea sauti kubwa sana kuliko chochote kitoacho sauti


MKUU Pesa ambayo Sio Yako na uliyoichukua kwa makubaliano ya kuiludisha hata kama ni 1000 Mkuu hakika Sio nzuri ni hatia Bora hata iwe ya ndugu


Mithali 26:2

"Kama shomoro katika kutanga-tanga kwake, Na kama mbayuwayu katika kuruka kwake; Kadhalika laana isiyo na sababu haimpigi mtu"



Kadhalika laana isiyo na sababu haimpigi mtu 👉 sasa wenzako wanayo sababu umechukua hadhina (Pesa) yao na hutaki kuludisha lolote watakalotamka juu Yako
Litakua b'se una hatia(sababu)



"Hadhina ya MTU ilipo na moyo wake ndipo ulipo" 👉 pay theirs money n gonna be Free
 
Mzee Mimi sikutishi uliza watu na hii sio Kwa hao tu Hadi kampuni za simu kitendo Cha kukopa halafu ukavunja laini Yako ya simu na umesajili Kwa nida deni lako linabaki milele na riba inapanda siku ukienda kuomba mkopo bank wataangalia record zako kwenye Kila sehemu ndio upewe mkopo na hap jamaa huwa wanapeleka record za watu wasiolipa bank sababa hayo makampuni upande wa mikopo yanadhaminiwa na bank hao sio wajinga mpaka wakopeshe pesa mtandaoni
Upo nchi gani?
 
Back
Top Bottom