Nabii Issa alipokuja (mazazi yake yalikua ni ya maajabu sana), pia yeye mwenyewe alikua ni mwenye maajabu na miujiza ya hali ya juu. Alipoondoka watu waligawika makundi matano.
1-Kundi la kwanza kabisa walidai kwamba Issa a.s ndiye MUNGU
2-Kundi la pili walidai Issa a.s ni Mtoto wa MUNGU
3-Kundi la tatu walidai kwamba Issa a.s ni Nabii na mtume wa MUNGU (Hili kundi la tatu walikua ni wachache sana) na hawa kwetu sisi ndio tunawaita 'Ahlul-kitaab' kwasababu waliendeleza kuishikilia Injili.
4-Kundi la nne ni mahayudi walioendeleza mila za Nabii Mussa a.s lakini wakamkataa Issa a.s hawa pia tunawaita ni 'Ahlul-kitaab' kwasababu waliendelea kuishikilia Taurati.
5-Kundi la 6 ni Mayahudi yaliyokufuru kabisa ambayo yalipiga vita makundi hayo manne ya juu, walichinja na kuuwa Manabii na kuwakataa hadharani na ndio hawa waliolaaniwa kwa Kauli ya Dawd na Kauli ya Nabii Issa, na hapo ndipo ufalme wa kiungu ukaondolewa kwao na kupelekwa arabuni.