Tupo tunatazama!
Huu mpambano uendeshwe Kwa tahadhari, maana kuna watu wanaanza kuingiza agenda zisizofaa.
Gwajima ni mtu anayependa kushindana na kushinda. Kwa kushindana huchukulia kama mchezo. Na bahati nzuri anaumudu.
Gwajima ni zile type za kina Trump. Njia pekee ya kuwashinda watu aina ya Gwajima ni Kuwapuuza tuu.
Naona kuna baadhi ya viongozi na watu wenye majina wanaanza kuingiza agenda za udini katika kupambana na Gwajiboy. Jambo ambalo ni kosa kiufundi.
Mbaya zaidi wanaofanya hivyo ni dini tofauti jambo ambalo linaweza kubadili mwelekeo wa mapambano.
Ukweli ni kuwa Likija swala la Dini hatumshinda Gwajima. Na Gwajima anajua fika Kabisa kuhusu hilo.
Gwajima ugomvi ukihamia kwenye Dini ni sawa na Umfuate Mamba kwenye kina kirefu Cha Maji.
Dawa ya Gajima ni kumtoa kwenye mfumo unaompa nguvu ambapo inakuwa rahisi kujipigia utakavyo.
Gwajima nje ya Kanisa hawezi kuongea, utamuonea huruma tuu.
Lakini sio Huku baadhi ya watu wanakotaka kulipeleka hili pambano.
Ieleweke, iwe iweje mkiruhusu iende kidini Basi Gwajima hatakuwa pekeake, ataungwa Mkono na Wakristo Kwa madhehebu Yao yote. Na hilo Lipo wazi. Hautakuwa mwelekeo mzuri.
Serikali ipige marufuku matumizi ya udini katika mapambano au kutokuelewano kokote ndani ya nchi.
Haya
Katika posts zako zote ninazosamaga, nadhani hii umeindaa ukiwa mtu mwingine kabisa...
Na hoja yako iliyotia fora ni hii👇
"....Dawa ya Gajima ni kumtoa kwenye mfumo unaompa nguvu ambapo inakuwa rahisi kujipigia utakavyo.Gwajima nje ya Kanisa hawezi kuongea, utamuonea huruma tuu..."
Hapa hujaeleweka unaongelea mfumo upi hasa.
Je una maana asiwe sehemu ya mfumo kiserikali kupitia Bunge na ubunge wake..? Au
Je, una maana atolewe kwenye mfumo kuwa kiongozi mkuu wa huduma ya kikanisa ya uaskofu na uchungaji? How exactly? Kufutia usajili kanisa lake? Kumnyang'anya huduma ya uchungaji? Kumnyang'anya title yake ya uaskofu..?
If this is what you're thinking, then it's too low of you..!
Umeshindwa kutumia umahiri wako wa u - taikoni wa Fasihi Andishi kujenga hoja yako vizuri...
Na jibu la hoja yako hii ni kuwa;
There's no way unaweza kumnyang'anya Askofu Josephat Gwajima jukwaa la kusemea mambo ya nchi hii so long as ni raia halali wa taifa hili...
Tunachopaswa kufanya ni kuwaonya watawala kuzingatia ushauri wa watu muhimu kama Askofu Gwajima Kwa mustakabali mwema wa taifa hili. Kupuuza hoja zake na kuanza kutafuta njia au mbinu za kuziba mdomo wa mtoa hoja haitatua tatizo...!
By the way, hoja za Askofu Gwajima ziko very straight, very genuine na ni hoja za karibu Watanzania wote. Shida iko kwa kundi dogo tu la watawala, watu wasiozidi 20 wanaodhani wana maamuzi ya kila kitu ktk nchi hii...
Hawawezi, na mwisho wao umeshafika...