Pamoja na Dodoma kuwa Katikati ya nchi lakini bado haikupaswa kuwa Makao Makuu

sidhani kama ni chumvi labda chokaa au kitu kingine.....maji ya dodo ni magumu hata kama unaoga ni kama unaoga vumbi la gypsum
 
Kiukweli hali ya hewa dodoma ni mbaya sana
Ni mbaya sababu ya miundombinu bado, pole pole mambo yatakuwa vizuri tu. Hata hali ya hewa Dar si nzuri kabisa sema kwa sababu tayari kushajengwa ndio maana panaonekana pazuri, lakini kama miji yetu ingejengeka vizuri Dar ingekuwa ya mwisho kupendwa sababu ya mazingira yake na hali ya hewa
 
Zamani Dodoma ilikuwa msitu na nchi ya kupendeza sana. Sema ilikuja kuharibiwa na ujio wa garimoshi ambazo zilitumia kuni kama nishati yake. Na sehemu kubwa ya msitu wa Dodoma ilifyekwa wakati huo hadi kupelekea Dodoma kuwa kama ilivyo leo.
 
Tangulini hali ya hewa ikawa kigezo cha kupima ubora wa mji.Kama hali ya hewa ni kigezo nambamoja cha kupima ubora wa mji basi Makete,Lushoto na Njombe zingeshakua na hadhi ya Jiji
 
Wewe mjinga israel imebadilisha jangwa kuwa nchi inayozalisha Hadi akiba ya chakula leo unazingumzia dodoma ambayo inapata mvua karibu miezi mitatu mfululizo kwa mwaka

Mkiambiwa waafrika akili zenu zipo matakoni wewe ndio mfano namba moja
Mkuu kuna watu hawajawahi kukanyaga Dodoma ila wanasimuliwaga tu alafu wanakuja kuandika utoporoo mtupu.Mtu anakwambia eti Dodoma ni jangwa na ukame alafu ukimuuliza kama ni jangwa inakuaje tena wanaongoza Tanzania kwa kilimo cha Alizeti,Zabibu,Karanga,Mtama,Ulezi,Uwele,Tende,Mbaazi,Rosella plus soko la kimataifa la mahindi Kibaigwa anakosa jibu la kuelewekaπŸ˜€πŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…