Pamoja na Dodoma kuwa Katikati ya nchi lakini bado haikupaswa kuwa Makao Makuu

Pamoja na Dodoma kuwa Katikati ya nchi lakini bado haikupaswa kuwa Makao Makuu

Kwan mipango hio si ipo. Jiji hawakup kibal cha ujenz had upande mti.na mabati yasiwe tofaut.au ilikufa hio mipango na kunambi alivoondoka? Dom napenda sana ule mtaa wa vitumbua na mabajia. Kwa stend ya daladala ni vurugu tupu haijulikan yan hapaelewek. Ukiwa mjin pale mazingira saf tu.vumbi lipo tu kila eneo.ila nadhan singida ingekua ndio mji mkuu.singida haina ukame kama wa dodoma.unaweza ukaona utan ila ukabu wa singapoo sio sawa na dom
Singida hapana mkuu doh
 
Ungeliongelea hisia za namna unavyotaka kuendesha maisha yako binafsi, lakini si kwa kukosoa maamuzi sahihi ya Serikali kuhamishia makao makuu pale.

Dodoma imo katika jiografia ya nchi, hauwezi kuitweza ama kuitenga na Tanzania kwa sababu yoyote ile.

Mengi ya sababu ulizoongelea zaweza kurekebishwa kwa kuboreshwa kwa miundo mbinu ya msingi tu na pakawa safi kabisa pa mfano.

Angalia maeneo mengine Duniani yenye jiografia yenye dhiki kuliko jiografia ya Dodoma, kwa mfano Dubai ya leo ama miji mingine iliyomo katika nchi za majangwani namna walivyoboresha miundo mbinu yao na jinsi wanavyo yafurahia maisha!

Ninadhani ungekuja na hoja namna ya kuligeuza Jiji la Dodoma liwe la kijani ili liweze kufaa zaidi kwa maisha ya binadamu.

Uwezekano wa kuvutwa maji baridi toka vyanzo vya kueleweka upo na ulikuwepo.

Maji kutoka Viktoria kuyafikisha pale Igunga, ajenda kuu ilikuwa ni kuyafikisha Makao hadi makao makuu Dodoma ili kulifanya jiji lisitimke vumbi na liwe la kijani.

Uwezekano huo upo, sema labda mipango ndiyo inachelewa tu.

Mkuu mawazo yako siku zote jaribu kuyaweka kutatua tatizo na si kusifia sehemu iliyokwisha boreshwa.

Dar es salaam unapopasifia, bila kuwekwa miundombinu ya maana, pangelifaa nini hapo, kwanza joto lililopo la kushinda na taulo mtu unajifuta, watu wengine hawawezi kupapenda.

Kwa hiyo jiografia ya kila sehemu yoyote hapakosi changamoto zake na uzuri wake pia.
Nani wa kubadilisha dodoma kuwa kama dubai??? Ni hawa hawa majambazi waliojificha kwny V8 zenye full tinted?

Dubai ilikua jangwa lakn leo hii ni full kijani kibich kama beach kwa sababu wana viongozi wenye vision sio hz taka taka zetu
 
Sku ya kwanza kufika dodoma nilipaka lotion,,, nkavaa nguo,,, ile namaliza kuvaa tu najiangalia kwny kioo, ngozi kama ya kenge,,, khaaaaaa
Watu wengi wa Dar,uelewa wao kuhusu hii nchi ni mdogo sana,
Kuna jamaa nilikutana nao temeke Dar,sasa pembeni yetu kulikuwa Kuna watu wanaongea rafudhi kama Kirundi,au waha wakigoma,
Jamaa zangu Hawa wakawa wanabisha kwamba Hawa hawawezi kuwa watz,kwanini wanaongea kama warundi,na wanaonekana kama wanyarwanda,nikawaambia,watu wa Kigoma,ngara,karsgwe,wanafanana sana na watu wa nchi jiraniRwanda,Burundi,na hata lugha zinaingiliana,
Watu wengi wa Dar,wanafikiri mtz,ni yule anayeongea kiswahili kama mzaramo,
Na kwa ufupi,Dar haikutokea tu,imejengwa,miji hujengwa,Arusha hakuna bahari,lakini Kuna hari nzuri kuliko Dar,Njombe Kuna baridi kama ulaya,je tuseme Njombe ni Bora kuliko Dar?
 
Dom pazur ,uende huyo rafikiyo kaachika ndo maana kapauka,au anatembea Juan,jua la Dom hutakiw kuzid nusu saa ukiwa juan ,litakuharibu ngozi ila ni jiji Zuri
 
Wewe mjinga israel imebadilisha jangwa kuwa nchi inayozalisha Hadi akiba ya chakula leo unazingumzia dodoma ambayo inapata mvua karibu miezi mitatu mfululizo kwa mwaka

Mkiambiwa waafrika akili zenu zipo matakoni wewe ndio mfano namba moja
Naunga hoja akili za wengi zimekaa matakoni.
 
Kuhusu jua kali hata ukipanda miti haisaidii ni uongo maybe huipend Dom individual! But hakuna kinashindikana dunia hii hasa suala la upandaji miti na kubadili mazingira na hali ya hewa, jua kweli la Dom ni kali lkn kwa juhud zilizopo za kupanda zaid miti itasaidia san miaka ijayo!! Kuhusu maji yana chumvi kuliko ya bahari huo ni uongoo, maji yapo yenye chumvi lkn sio on that way u claim!! Dar imekua na changamoto nying san za maji saf na salama, jua kali joto kali vitu ambavyo sio comfortable kwa mwanadam lkn ilikua makao makuu kwa miaka na raia walizoea!!
Yaani huyu ni muongo.Hivi hapo dodoma mjini naona huyu tena ni mgeni.Ebu tembelea area c area d na uzunguni kwa miti ilivyopandwa kama utaliona jua.Waambie wakuja wapande miti.
 
Kuna mgogo moja humu jf kutwa yeye kutukana walimu nasikia kwao mpunguzi
 
Dodoma na Tanga zimekuwa majiji Kwa sababu ni ngome za CCM!!! Lakin hazikustahili !!!
 
Nisiwe na Maneno mengi lakini kiukweli hali ya hewa ya Dodoma inaumiza sana na mtu huwezi kuwa comfortable hata kidogo.

Yaani huu mji hata ulazimishe kupanda miti kiasi gani bado ni shida. Hata mwanga wa jua huku ni shida kwa jinsi unavyoumiza macho, yaani kila unayekutana naye kakunja uso na kufinya macho sababu ya jua. Huwezi kuta mtu kanawiri hata kama ana maisha mazuri.

Kuna masela wangu tulikuwa nao Dar wakahamia Dom nimewaona sura zimefubaa sababu ya hali ya hewa. Kipindi cha kiangazi ndio shida zaidi utafikiri watu wapo Sudan jamani. Kitu kingine kinachokera ni Maji mabaya sana, sio machafu lakini ni mabaya na yamejaa chumvi kuliko hata humvi la maji ya bahari.

Kuna jamaa akanishawishi eti nijenge nyumba ya makazi nikamuambia labda nijenge gest lakini si mimi kuja kjishi
Tangu lini Dodoma imekua katikati ya nchi?
Katikati ya nchi ni Manyoni , siyo Dodoma.
 
Kama kweli serikali itaweka dhamiri ya dhati kuhusu kuibadilisha Dodoma,inawezekana ikawa ni mji mzuri sana,na wenye miti kila kona,tatizo naona ni wana siasa wa maigizo ndio wanaokwamisha.Mvua Dodoma inanyesha kwa mwaka karibu miezi 4,sasa kama kutakuwa na kampeni kama zile za kutokomeza mifuko ya plastic ikawezekana, hata ya kupandwa miti kwa lazima inawezekana,kuna mahali ni lazima ubabe utumike,msimu wa mvua unapoanza tu miti inapandwa,ikifika miezi 4 imeshashika na inaendelea kukua,kuna aina ya miti ikishashika hata kama mvua itakaa miezi 6 haidondoshi majani na inakuwa kijani kibichi,hii miti inaitwa Midodoma,inastahimili ukame na ina kivuli kikubwa...
Ila Serikali sijui kwa nini hawako serious
Wakati wanaweza hata kuvuna maji
 
Nisiwe na Maneno mengi lakini kiukweli hali ya hewa ya Dodoma inaumiza sana na mtu huwezi kuwa comfortable hata kidogo.

Yaani huu mji hata ulazimishe kupanda miti kiasi gani bado ni shida. Hata mwanga wa jua huku ni shida kwa jinsi unavyoumiza macho, yaani kila unayekutana naye kakunja uso na kufinya macho sababu ya jua. Huwezi kuta mtu kanawiri hata kama ana maisha mazuri.

Kuna masela wangu tulikuwa nao Dar wakahamia Dom nimewaona sura zimefubaa sababu ya hali ya hewa. Kipindi cha kiangazi ndio shida zaidi utafikiri watu wapo Sudan jamani. Kitu kingine kinachokera ni Maji mabaya sana, sio machafu lakini ni mabaya na yamejaa chumvi kuliko hata humvi la maji ya bahari.

Kuna jamaa akanishawishi eti nijenge nyumba ya makazi nikamuambia labda nijenge gest lakini si mimi kuja kjishi
Komaa wewe acha kujilegeza
 
Komaa wewe acha kujilegeza
Kwamba nikomae tu kwenye jua hata kama kuna kivuli pembeni kisa tu mimi dume. Nyie ndio wale kipindi cha ujana mlikuwa mnajisifia eti "mi mgumu bwana". Mnajinyima starehe kwa kujikomoa wenyewe
 
Back
Top Bottom