Kama kweli serikali itaweka dhamiri ya dhati kuhusu kuibadilisha Dodoma,inawezekana ikawa ni mji mzuri sana,na wenye miti kila kona,tatizo naona ni wana siasa wa maigizo ndio wanaokwamisha.Mvua Dodoma inanyesha kwa mwaka karibu miezi 4,sasa kama kutakuwa na kampeni kama zile za kutokomeza mifuko ya plastic ikawezekana, hata ya kupandwa miti kwa lazima inawezekana,kuna mahali ni lazima ubabe utumike,msimu wa mvua unapoanza tu miti inapandwa,ikifika miezi 4 imeshashika na inaendelea kukua,kuna aina ya miti ikishashika hata kama mvua itakaa miezi 6 haidondoshi majani na inakuwa kijani kibichi,hii miti inaitwa Midodoma,inastahimili ukame na ina kivuli kikubwa...