Ushujaa wa hali ya juuš
Mahakama ya Wilaya ya Geita imemwachia kwa dhamana Mwenyekiti wa CHADEMA Geita Vijijini, Neema Chozaile, baada ya kushikiliwa mahabusu kwa zaidi ya siku 20.
Chozaile anakabiliwa na shtaka la kula njama za kumuua askari polisi, shauri ambalo linaendelea kusikilizwa mahakamani hapo.
Baada ya kusikiliza maombi yaliyowasilishwa, Mahakama ilikubali kumwachia kwa dhamana huku ikimtaka kuendelea kuzingatia masharti yote ya dhamana wakati shauri hilo likiendelea.
Mahakama imeahirisha shauri hilo na kulipangia kutajwa tena Agosti 3, 2026, kwa hatua zaidi za kisheria.
Chozaile ameachiwa huru kwa dhamana huku akitarajiwa kurejea mahakamani tarehe hiyo ya Agosti 3 kwa ajili ya kuendelea na mwenendo wa shauri linalomkabili.
Pia soma:
Mawakili wa Serikali wakwamisha zoezi la kupelekwa mahakamani mwenyekiti wa CHADEMA Geita, Neema Chozaire