Pamoja na madhaifu yao, watu wa Pwani ni watu poa sana

Pamoja na madhaifu yao, watu wa Pwani ni watu poa sana

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Kwema Wakuu!

Kwa ambao hawawajui watu wa Pwani na hawajawahi kufika Pwani naomba kuwajuza tuu, watu wa Pwani ni mikoa ya Tanga, Pwani yenyewe, DAR, Lindi, mtwara, Visiwa vya unguja na pemba,na kidogo Morogoro.

Watu hawa bhana mbali na udhaifu wao lakini wapo poah Sana.

Madhaifu Yao makubwa ni Kama ifuatavyo;

1. Uvivu na ubwanyenye.
2. Hawapendi complication ya mambo katika Mishe zao.
3. Kuridhika mapema.
4. Ngoma na vigodoro ambavyo hata hivyo siku hizi ni Kama wamepunguza kidogo.
5. Dhana kuwa dunia tunapita hivyo masuala ya kupigania maisha hawana.
6. Mdomo na Majungu. N.k
7 ushirikina na Uchawi

Pamoja na udhaifu wao lakini Kwa kweli watu wa Pwani ni watu Bora Sana. Kwa sababu zifuatazo

1. Roho nzuri.
Hawana Roho mbaya kufikia kuua watu.
Ni ngumu Sana kusikia matukio ya vifo kutoka watu wa Pwani.
Roho Mbaya zao nizakawaida tuu lakini sio zilizovuka mipaka.

Ni ngumu kusikia mke au mume kauawa katika jamii za watu wa Pwani. Hiyo huwa nadra Sana. Lakini Sisi wabara tunaongoza. Yaani haiwezi pita wiki bila kusikia tukio la mauaji katika Maeneo yetu.

Ni ngumu Kwa Kiongozi mkubwa wa nchi akitokea Pwani nchi ikabiliwe na matukio ya roho Mbaya.
Kama ni roho mbaya itakuwa Ile ya kawaida.

Watu wa Pwani hata uwaseme vipi, uwaite majina yote mabaya, bado watakukaribisha kwao, watawauzia viwanja na mtajenga, yaani mtaishi maisha ya Raha mustarehe. Kiufupi watu wa Pwani sio wabaguzi.


2. Wanajali maisha ya wengine na wanajua maisha ni nini.
Watu wa Pwani ni watu wakujali maumivu ya watu wengine.
Mtu WA Pwani Kwa mfano Mtoto wako akifanya tukio Baya akakamatwa na kutiwa ndani, watu wa Pwani wapo tayari kuchanga pesa au kukusaidia uondokane na hilo tatizo, kisha baadaye mtamalizana.

Huwezi msikia mtu wa Pwani ati mtoto wako akamatwe mfano na madawa ya kulevya huko nje alafu kiongozi aropoke kuwa atajijua mwenyewe. Hawana roho mbaya ya hivyo.

3. Hawana majigambo; wanyenyekevu.
Ni nadra Sana kumsikia mtu wa Pwani akijitamba na kudharau watu wa makabila mengine.
Licha ya kuwa tukifika miji yao tunawatolea maneno ya shombo lakini wao wala hawana habari na Sisi.

4. Hawana Ubinafsi.
Watu wa Pwani wakiingia uongozini hawaibi wenyewe Mali za nchi hii. Wanaiba na watu wengine.
Hakuna mwanadamu asiyemwizi hilo lipo hivyo Duniani kote. Na Kama yupo basi ni 1 Kwa elfu moja.

Mtu WA Pwani akiingia madarakani basi jua mtakula wote view vya kuchinja au vyakunyonga.

Hawana Ile tabia ya kujifanya wao ni watakatifu Kwa kujipa jina la uzalendo Kwa kuzuia wengine wasiibe(walaji wa nchi) alafu wao wajilimbikizie Mali.

Hutumia kanuni isemayo, Kula kizuri na wenzako lakini kila Mbuzi hula urefu WA kamba yake.

Awamu zao, Ajira zitakuwa nyingi, pesa mtaani zitakwagika lakini haimaanishi watu watakula nje ya urefu WA kamba zao.

Watu wa Pwani sio watu wa kujibana.
Wao unafanya maendeleo huku mnakula maisha Kwa sababu tunaishi leo.

Lakini Sisi wa bara ni watu ambao wengi wetu tunatumia falsafa ya kujibana tufanye maendeleo kisha baadaye ndio tule BATA.

Watu wa Pwani wakiongoza nchi hii, huwezi sikia maumivu ya watu kuuawa, kutekwa, na kufanywa vilema vya maisha.

Watu wa Pwani Kwa mdomo ndio kwao, hawaogopi kusema, kutupiwa maneno na kutukanwa.
Ndio maana wao wanangoma zinaitwa Vigoma Kwa ajili ya kuchambia na kusuta watu. Hivyo wao kusutana na utamaduni.
Ila kuuana ni nadra Sana.

Mwisho niseme,
Hakuna Bora ndani ya nchi hii.
Kila upande unamanufaa makubwa katika nchi hii.
Hivyo ni vyema taasisi nyeti za nchi zipange watu na kuwapa MAJUKUMU kulingana na Asili yake, ili kuleta ufanisi.

Lakini unampa mtu Urais mwenye asili ya watu wenye hasira unategemea nini Kama sio watu kuumia.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Vikindu, Pwani
 
Na roho Mbaya iliyopitiliza.

Ukichunguza ni nadra Sana matukio ya ukatili kutokea ukanda wa Pwani au watu wenye asili ya Pwani kuufanya.

Ila Sisi watu Wabara loooh!
Imagine saizi Rais anasimamia haki Kati ya Zanzibar na Bara ila majitu ya Bara sasa yenye roho za kichawi hayataki hiyo Hali.

Wanasahau kwamba Zanzibar ingekuwa huru ingeshakuwa Dubai au Doha siku nyingi tuu.
 
Back
Top Bottom