Pamoja na madhaifu yao, watu wa Pwani ni watu poa sana

Pamoja na madhaifu yao, watu wa Pwani ni watu poa sana

Kama Mkenya tena wa bara napitia huu uzi kimya kimya, nahisi kuna cha kuiga hapa, labda na sisi tujaribishe nchi iongozwe na Mkenya mwenye asili ya Pwani, labda mambo ya kikatili yanaweza yakapungua, sema sijui kiuchumi kama tutaendelea kwenye kasi ya leo.
 
Waislam wanamapungufu Yao lakini haiondoi sifa zao za Msingi, unyenyekevu na ukarimu

Mapungufu kwa binadamu ni lazima sisi sio malaika na yapo kwa kila binadamu

Ila kuna wengine wamezidi kuanzia ukatili na roho mbaya
Uislam hata kama huna kitu cha kutoa kama sadaka basi unatoa hata tabasamu kwani nayo inahisabika kama Sadaka

Always smile [emoji2]
 
Wakarimu sana watu wa pwani. Unamkuta ameketi kwenye mkeka wake anakula mihogo Ila lazima atakukaribisha japo ukate kipande.

Nikienda shambani unamwambia nipatie Nazi unashangaa anakwea mnazi anaangua na anafua dafu anakupa Nazi hata kumi mpaka inakubidi uone haya japo umpe hata elfu mbili ya sukari.

Sema wambea hao[emoji2][emoji2][emoji2] hawana dogo Wala kubwa. Wanajua kumsuta mtu mpaka unazimia[emoji2][emoji2]

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ukileta za kuleta utasutwa tu [emoji23][emoji23]

Ndio sifa kubwa ila hawana kufichaficha jambo
Atakugongea mlango asubuhi kama akisikia jambo
 
Dini ya kiislam ni Dini ya Haki MKUU.

Uislam Kwa Kiswahili ni unyenyekevu.

Mimi ni Mkristo Hilo nalijua.

Wapwani wanamapungufu ya kibinadamu, ya kawaida Ila ni nadra Sana kiwanja roho za kikatili.
Mbona magaidi wengi wanatoka kwenye hiyo dini.
 
😀😀😀😀

Unataka kusema Sisi bila kusoma ni Kama wanyama??
Watu wa pwani wanazaliw smart ndo maana elimu wanapuuza sipo kukejeli ila nakuambia kama unabisha nenda pwani tafuta mtu ambaye hajasoma kabisa yaani hata la saba hajafika then tafuta mtu wa bara ambaye kafika hata la saba

Then angalia nan anaju kuishi kutokana na hli yake

Ni kwamba hawa wana elimu nyingi mfano za mtaani huko pwani waty wanajua miezi tu kwa kuangalia angani na kujua haya ni maji yanatoja au yanaingia na miezi hyo inatajwa kwa kiarabu

Mfano huko south watu wa pwani hawana elimu ila wanauliwa sana kwa kupigwa risasi coz hawataki unyonge sana ni wajanja japo elimu ni zero
 
Tunapigania haki.

Ila jamani watu wa kanda ya ziwa ni makatili sana;wanauana sana kipindi cha kupanda mazao,kipindi cha mavuno...Kuna watu spesho wanakodiwa kwaajili ya kazi ya kuuwa tu dah kanda ya ziwa(Sukuma/Nyamwezi land)acheni uzamani.
Angalia asili ya utafutaji wao na kazi zao kama kilimo na ufugaji izo jamiu wana ukatili sana na hawapati kabisa

Bara ni kawaida sana huku pwani ukimpiga tu mkeo kibao akienda kwao umemkosa na unaweza kufungwa ila bara huko noma wanapigwa wanavumilia kawaida yao

Mfano niliwai kusikia mauaji kadhaa Tanga na ujambazi wa kutisha miaka ya 2007 ulishamiri ila kila anayekamatwa ni mtu arusha ,mbaya


Kingine watu wa pwani wana vimwili vidogo sana kuliko watu wa bara naona hata vurugu hawawezi
 
Pia umesahau maendeleo yote dunianu yapo pwani mfano New york ipo pwani,Landon ipo pwani, California ipo pwani,Texas ipo pwani,Georgia ipo pwani,Toronto ipo pwani,Shanghai ipo pwani yani pwani ndo mwanzo wa maendeleo
 
Pia umesahau maendeleo yote dunianu yapo pwani mfano New york ipo pwani,Landon ipo pwani, California ipo pwani,Texas ipo pwani,Georgia ipo pwani,Toronto ipo pwani,Shanghai ipo pwani yani pwani ndo mwanzo wa maendeleo


Ati nini
 
Na kwa Sasa watu wa pwani ndiyo wanaongoza nchi,
- Mchengerwa
-Nape >
-Aweso
-Ummy
- Makamba
-Jafo
-Ulega
-Mzee Mkuchika
-Ridhiwani
-Hamis Chilo
-Masauni
-Majaliwa
 
Kwema Wakuu!

Kwa ambao hawawajui watu wa Pwani na hawajawahi kufika Pwani naomba kuwajuza tuu, watu wa Pwani ni mikoa ya Tanga, Pwani yenyewe, DAR, Lindi, mtwara, Visiwa vya unguja na pemba,na kidogo Morogoro.

Watu hawa bhana mbali na udhaifu wao lakini wapo poah Sana.

Madhaifu Yao makubwa ni Kama ifuatavyo;

1. Uvivu na ubwanyenye.
2. Hawapendi complication ya mambo katika Mishe zao.
3. Kuridhika mapema.
4. Ngoma na vigodoro ambavyo hata hivyo siku hizi ni Kama wamepunguza kidogo.
5. Dhana kuwa dunia tunapita hivyo masuala ya kupigania maisha hawana.
6. Mdomo na Majungu. N.k
7 ushirikina na Uchawi

Pamoja na udhaifu wao lakini Kwa kweli watu wa Pwani ni watu Bora Sana. Kwa sababu zifuatazo

1. Roho nzuri.
Hawana Roho mbaya kufikia kuua watu.
Ni ngumu Sana kusikia matukio ya vifo kutoka watu wa Pwani.
Roho Mbaya zao nizakawaida tuu lakini sio zilizovuka mipaka.

Ni ngumu kusikia mke au mume kauawa katika jamii za watu wa Pwani. Hiyo huwa nadra Sana. Lakini Sisi wabara tunaongoza. Yaani haiwezi pita wiki bila kusikia tukio la mauaji katika Maeneo yetu.

Ni ngumu Kwa Kiongozi mkubwa wa nchi akitokea Pwani nchi ikabiliwe na matukio ya roho Mbaya.
Kama ni roho mbaya itakuwa Ile ya kawaida.

Watu wa Pwani hata uwaseme vipi, uwaite majina yote mabaya, bado watakukaribisha kwao, watawauzia viwanja na mtajenga, yaani mtaishi maisha ya Raha mustarehe. Kiufupi watu wa Pwani sio wabaguzi.


2. Wanajali maisha ya wengine na wanajua maisha ni nini.
Watu wa Pwani ni watu wakujali maumivu ya watu wengine.
Mtu WA Pwani Kwa mfano Mtoto wako akifanya tukio Baya akakamatwa na kutiwa ndani, watu wa Pwani wapo tayari kuchanga pesa au kukusaidia uondokane na hilo tatizo, kisha baadaye mtamalizana.

Huwezi msikia mtu wa Pwani ati mtoto wako akamatwe mfano na madawa ya kulevya huko nje alafu kiongozi aropoke kuwa atajijua mwenyewe. Hawana roho mbaya ya hivyo.

3. Hawana majigambo; wanyenyekevu.
Ni nadra Sana kumsikia mtu wa Pwani akijitamba na kudharau watu wa makabila mengine.
Licha ya kuwa tukifika miji yao tunawatolea maneno ya shombo lakini wao wala hawana habari na Sisi.

4. Hawana Ubinafsi.
Watu wa Pwani wakiingia uongozini hawaibi wenyewe Mali za nchi hii. Wanaiba na watu wengine.
Hakuna mwanadamu asiyemwizi hilo lipo hivyo Duniani kote. Na Kama yupo basi ni 1 Kwa elfu moja.

Mtu WA Pwani akiingia madarakani basi jua mtakula wote view vya kuchinja au vyakunyonga.

Hawana Ile tabia ya kujifanya wao ni watakatifu Kwa kujipa jina la uzalendo Kwa kuzuia wengine wasiibe(walaji wa nchi) alafu wao wajilimbikizie Mali.

Hutumia kanuni isemayo, Kula kizuri na wenzako lakini kila Mbuzi hula urefu WA kamba yake.

Awamu zao, Ajira zitakuwa nyingi, pesa mtaani zitakwagika lakini haimaanishi watu watakula nje ya urefu WA kamba zao.

Watu wa Pwani sio watu wa kujibana.
Wao unafanya maendeleo huku mnakula maisha Kwa sababu tunaishi leo.

Lakini Sisi wa bara ni watu ambao wengi wetu tunatumia falsafa ya kujibana tufanye maendeleo kisha baadaye ndio tule BATA.

Watu wa Pwani wakiongoza nchi hii, huwezi sikia maumivu ya watu kuuawa, kutekwa, na kufanywa vilema vya maisha.

Watu wa Pwani Kwa mdomo ndio kwao, hawaogopi kusema, kutupiwa maneno na kutukanwa.
Ndio maana wao wanangoma zinaitwa Vigoma Kwa ajili ya kuchambia na kusuta watu. Hivyo wao kusutana na utamaduni.
Ila kuuana ni nadra Sana.

Mwisho niseme,
Hakuna Bora ndani ya nchi hii.
Kila upande unamanufaa makubwa katika nchi hii.
Hivyo ni vyema taasisi nyeti za nchi zipange watu na kuwapa MAJUKUMU kulingana na Asili yake, ili kuleta ufanisi.

Lakini unampa mtu Urais mwenye asili ya watu wenye hasira unategemea nini Kama sio watu kuumia.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Vikindu, Pwani
Haya uliyoyaandika Bro una uhakika nayo? Mimi niko Pwani mwaka wa 14 sasa najua vizuri tabia na tamaduni za watu wa Pwani.
 
Kusutana kunaondoa sumu ya chuki sana moyoni na ndio maana wakisutana moyo unabaki swaafi huna tena haja ya kutoana roho

Bara wengi wao hawataki kutoa ya moyoni sasa kinachobaki ni kisasi kutoana roho
 
Back
Top Bottom