Pamoja na madhaifu yao, watu wa Pwani ni watu poa sana

Pamoja na madhaifu yao, watu wa Pwani ni watu poa sana

Kuna jamaa yangu mmoja yeye alikuaga mkwere alinifundisha vitu vingi sana yani nilikuaga nakosea wazi wazi jamaa ananiambia mzee usiweke wazi vitu hivyo, wewe nyamaza, usiongee wewe sikiliza...kwenye hekima na kuishi na watu wanajua yani wapo vizuri hata kuishi na adui yake...
 
Sisi watu wa pwani hatujasoma Cha ajabu, tulileta raisi, na kulikuwa na vikao vya malalamiko ......na maongez na yule rais handsome Alisema tatizo ndugu zangu hamjasoma, na Hampend shule, hata nafas ya juu nitamuweka Nani.

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Sisi watu wa pwani ...tuna wanawake warembo pia mkuu ongezea hilo😂😂

Wakipenda wamependa hawa sio kama wale wa sinoni daraja mbili bila pesa si lolote

Halafu jengine waweza pikiwa kisamvu na ukahisi umekula nyama
 
Ni dhana ya hovyo Sana hii,wachaga wanapenda sana kusafiria nyota za matajiri wakichaga,mfukoni hana hata mia halafu utamsikia watu wa tanga bwana masikini sana!
Utawasikia watu wa mikoani jengeni kwenu. Uchaggani tumejenga.

Halafu anaposti jumba la Mengi🤣
 
Umesahau udhaifu wa wanaume wa Dar au umefanya makusudi?
 
Umeandika sifa nyepesi, sifa kuu umeiacha..

Wana "brain" ya kuliongoza taifa?
Mkui TZ imeongozwa na Marais wa4 kutokea PWANI. MWINYI, KIKWETE, MKAPA na sasa ni SAMIA. unataka kusema hao wote hawana brain nzuri kushinda wewe ambaye hata MUTUKURA hupajui?
 
Kuongozwa na watu wenye utamaduni wa umaskini nchi itaendelea kuwa maskini. Mpe nchi mchaga uone mabadiliko changa ya haraka.
Wachaga wameua taasisi na makampuni mengi sana. TTL ni mfano, Benki nyingi ziliuawa na wachaga.Hawajawahi onesha ubora wa kukuza taasisi bali kuua.
Kumbuka wachaga ndio mameneja wa kwanza kwenye taasisi zetu leo zipo wapi?
 
Jukwaa huru hili,nani kakukataza kuandika wewe vitu ulivo na uhakika navyo?
 
Pia umesahau maendeleo yote dunianu yapo pwani mfano New york ipo pwani,Landon ipo pwani, California ipo pwani,Texas ipo pwani,Georgia ipo pwani,Toronto ipo pwani,Shanghai ipo pwani yani pwani ndo mwanzo wa maendeleo
Logical sehemu yenye bahari ni rahisi sana kumove raw materials,kuestablish kiwanda na hata kuestablish makazi na socialization huwa kubwa,.....ni ngumu sana eti mgeni aache kujenga nyumba Bagamoyo aende kujenga nyumba bariadi the same as U.S ni rahisi mgeni anunue apartment New York bay kuliko kwenda North's na south Dakota
 
Na kwa Sasa watu wa pwani ndiyo wanaongoza nchi,
- Mchengerwa
-Nape >
-Aweso
-Ummy
- Makamba
-Jafo
-Ulega
-Mzee Mkuchika
-Ridhiwani
-Hamis Chilo
-Masauni
-Majaliwa
Aiseee,[emoji16] kuna ukweli flani hivi mchungu
 
Madhaifu Yao makubwa ni Kama ifuatavyo;

1. Uvivu na ubwanyenye.
Lini umewahu kusikia watu wa pwani wanakufa njaa na kwahiyo serikali ikalazimika kwenda kuwapa misaada?!

Au kwavile nyie mnachunga ng'ombe ndo mlitarajia kila mtu achunge ng'ombe hata kama sio kazi zao za asili?!

Korosho ambazo zinaliingizia taifa mabilioni ya pesa zinalimwa na nyinyi??

Mbaazi ambazo zilikuwa zinaozeana hadi kwenye maghala kwa kukosa soko mnalima nyie?

Nazi ambazo wengine mnaziona mkishakuja mjin, zinalimwa na nyie?

Acha ujinga!The way mnavyoongea kwa mgeni wa Tanzania anaweza kusema huko kwenu mambo yenu mazuri kweli kweli wakati ni maskini wa kutupwa!!
2. Hawapendi complication ya mambo katika Mishe zao.
Kama yapi? Kuchunga ng'ombe, au?!
3. Kuridhika mapema.
Na nyie msioridhika mapema mna nini cha maana?
4. Ngoma na vigodoro ambavyo hata hivyo siku hizi ni Kama wamepunguza kidogo.
Na ngoma za kipumbavu zinazohitimishwa kwa kukata visimi vya watoto zinachezwa pwani?
5. Dhana kuwa dunia tunapita hivyo masuala ya kupigania maisha hawana.
Yale yale!! Unaweza kukuta hata kwenye ukoo wako weneyewe kuna wengine hawana hata uhakika wa kula halafu hapa unaona wenzako hawapiganii maisha... VERY STUPID!

Kuna watu wangapi kutoka pwani ambao wewe binafsi au familia yako inawalipia kwa chochote?
6. Mdomo na Majungu. N.k
Kuna watu wa majungu kama nyie kenge?!
7 ushirikina na Uchawi
Umeshawahi kufanyiwa huo ushirikina au unasikia tu kwa Waruga ruga wenzako?

Hivi kule walikokua wanaua albino eti ili kupata utajiri ni pwani? Kule wanakoua wazee kisa wana macho mekundu ni pwani? Kule ambako walikuwa wanachuna wenzao ngozi ni pwani?
Pamoja na udhaifu wao lakini Kwa kweli watu wa Pwani ni watu Bora Sana. Kwa sababu zifuatazo

1. Roho nzuri.
Hawana Roho mbaya kufikia kuua watu.
Ni ngumu Sana kusikia matukio ya vifo kutoka watu wa Pwani.
Roho Mbaya zao nizakawaida tuu lakini sio zilizovuka mipaka.

Ni ngumu kusikia mke au mume kauawa katika jamii za watu wa Pwani. Hiyo huwa nadra Sana. Lakini Sisi wabara tunaongoza. Yaani haiwezi pita wiki bila kusikia tukio la mauaji katika Maeneo yetu.

Ni ngumu Kwa Kiongozi mkubwa wa nchi akitokea Pwani nchi ikabiliwe na matukio ya roho Mbaya.
Kama ni roho mbaya itakuwa Ile ya kawaida.

Watu wa Pwani hata uwaseme vipi, uwaite majina yote mabaya, bado watakukaribisha kwao, watawauzia viwanja na mtajenga, yaani mtaishi maisha ya Raha mustarehe. Kiufupi watu wa Pwani sio wabaguzi.

2. Wanajali maisha ya wengine na wanajua maisha ni nini.
Watu wa Pwani ni watu wakujali maumivu ya watu wengine.
Mtu WA Pwani Kwa mfano Mtoto wako akifanya tukio Baya akakamatwa na kutiwa ndani, watu wa Pwani wapo tayari kuchanga pesa au kukusaidia uondokane na hilo tatizo, kisha baadaye mtamalizana.

Huwezi msikia mtu wa Pwani ati mtoto wako akamatwe mfano na madawa ya kulevya huko nje alafu kiongozi aropoke kuwa atajijua mwenyewe. Hawana roho mbaya ya hivyo.

3. Hawana majigambo; wanyenyekevu.
Ni nadra Sana kumsikia mtu wa Pwani akijitamba na kudharau watu wa makabila mengine.
Licha ya kuwa tukifika miji yao tunawatolea maneno ya shombo lakini wao wala hawana habari na Sisi.

4. Hawana Ubinafsi.
Watu wa Pwani wakiingia uongozini hawaibi wenyewe Mali za nchi hii. Wanaiba na watu wengine.
Hakuna mwanadamu asiyemwizi hilo lipo hivyo Duniani kote. Na Kama yupo basi ni 1 Kwa elfu moja.

Mtu WA Pwani akiingia madarakani basi jua mtakula wote view vya kuchinja au vyakunyonga.

Hawana Ile tabia ya kujifanya wao ni watakatifu Kwa kujipa jina la uzalendo Kwa kuzuia wengine wasiibe(walaji wa nchi) alafu wao wajilimbikizie Mali.

Hutumia kanuni isemayo, Kula kizuri na wenzako lakini kila Mbuzi hula urefu WA kamba yake.

Awamu zao, Ajira zitakuwa nyingi, pesa mtaani zitakwagika lakini haimaanishi watu watakula nje ya urefu WA kamba zao.

Watu wa Pwani sio watu wa kujibana.
Wao unafanya maendeleo huku mnakula maisha Kwa sababu tunaishi leo.

Lakini Sisi wa bara ni watu ambao wengi wetu tunatumia falsafa ya kujibana tufanye maendeleo kisha baadaye ndio tule BATA.

Watu wa Pwani wakiongoza nchi hii, huwezi sikia maumivu ya watu kuuawa, kutekwa, na kufanywa vilema vya maisha.

Watu wa Pwani Kwa mdomo ndio kwao, hawaogopi kusema, kutupiwa maneno na kutukanwa.
Ndio maana wao wanangoma zinaitwa Vigoma Kwa ajili ya kuchambia na kusuta watu. Hivyo wao kusutana na utamaduni.
Ila kuuana ni nadra Sana.

Mwisho niseme,
Hakuna Bora ndani ya nchi hii.
Kila upande unamanufaa makubwa katika nchi hii.
Hivyo ni vyema taasisi nyeti za nchi zipange watu na kuwapa MAJUKUMU kulingana na Asili yake, ili kuleta ufanisi.

Lakini unampa mtu Urais mwenye asili ya watu wenye hasira unategemea nini Kama sio watu kuumia.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Vikindu, Pwani
Stop using carrot and stick! Haiwezekani mtu awe mshirikina, mchawi, na full majungu halafu hapo hapo eti useme ana roho mzuri na anajali watu wengine!
 
Kwema Wakuu!

Kwa ambao hawawajui watu wa Pwani na hawajawahi kufika Pwani naomba kuwajuza tuu, watu wa Pwani ni mikoa ya Tanga, Pwani yenyewe, DAR, Lindi, mtwara, Visiwa vya unguja na pemba,na kidogo Morogoro.

Watu hawa bhana mbali na udhaifu wao lakini wapo poah Sana.

Madhaifu Yao makubwa ni Kama ifuatavyo;

1. Uvivu na ubwanyenye.
2. Hawapendi complication ya mambo katika Mishe zao.
3. Kuridhika mapema.
4. Ngoma na vigodoro ambavyo hata hivyo siku hizi ni Kama wamepunguza kidogo.
5. Dhana kuwa dunia tunapita hivyo masuala ya kupigania maisha hawana.
6. Mdomo na Majungu. N.k
7 ushirikina na Uchawi

Pamoja na udhaifu wao lakini Kwa kweli watu wa Pwani ni watu Bora Sana. Kwa sababu zifuatazo

1. Roho nzuri.
Hawana Roho mbaya kufikia kuua watu.
Ni ngumu Sana kusikia matukio ya vifo kutoka watu wa Pwani.
Roho Mbaya zao nizakawaida tuu lakini sio zilizovuka mipaka.

Ni ngumu kusikia mke au mume kauawa katika jamii za watu wa Pwani. Hiyo huwa nadra Sana. Lakini Sisi wabara tunaongoza. Yaani haiwezi pita wiki bila kusikia tukio la mauaji katika Maeneo yetu.

Ni ngumu Kwa Kiongozi mkubwa wa nchi akitokea Pwani nchi ikabiliwe na matukio ya roho Mbaya.
Kama ni roho mbaya itakuwa Ile ya kawaida.

Watu wa Pwani hata uwaseme vipi, uwaite majina yote mabaya, bado watakukaribisha kwao, watawauzia viwanja na mtajenga, yaani mtaishi maisha ya Raha mustarehe. Kiufupi watu wa Pwani sio wabaguzi.

2. Wanajali maisha ya wengine na wanajua maisha ni nini.
Watu wa Pwani ni watu wakujali maumivu ya watu wengine.
Mtu WA Pwani Kwa mfano Mtoto wako akifanya tukio Baya akakamatwa na kutiwa ndani, watu wa Pwani wapo tayari kuchanga pesa au kukusaidia uondokane na hilo tatizo, kisha baadaye mtamalizana.

Huwezi msikia mtu wa Pwani ati mtoto wako akamatwe mfano na madawa ya kulevya huko nje alafu kiongozi aropoke kuwa atajijua mwenyewe. Hawana roho mbaya ya hivyo.

3. Hawana majigambo; wanyenyekevu.
Ni nadra Sana kumsikia mtu wa Pwani akijitamba na kudharau watu wa makabila mengine.
Licha ya kuwa tukifika miji yao tunawatolea maneno ya shombo lakini wao wala hawana habari na Sisi.

4. Hawana Ubinafsi.
Watu wa Pwani wakiingia uongozini hawaibi wenyewe Mali za nchi hii. Wanaiba na watu wengine.
Hakuna mwanadamu asiyemwizi hilo lipo hivyo Duniani kote. Na Kama yupo basi ni 1 Kwa elfu moja.

Mtu WA Pwani akiingia madarakani basi jua mtakula wote view vya kuchinja au vyakunyonga.

Hawana Ile tabia ya kujifanya wao ni watakatifu Kwa kujipa jina la uzalendo Kwa kuzuia wengine wasiibe(walaji wa nchi) alafu wao wajilimbikizie Mali.

Hutumia kanuni isemayo, Kula kizuri na wenzako lakini kila Mbuzi hula urefu WA kamba yake.

Awamu zao, Ajira zitakuwa nyingi, pesa mtaani zitakwagika lakini haimaanishi watu watakula nje ya urefu WA kamba zao.

Watu wa Pwani sio watu wa kujibana.
Wao unafanya maendeleo huku mnakula maisha Kwa sababu tunaishi leo.

Lakini Sisi wa bara ni watu ambao wengi wetu tunatumia falsafa ya kujibana tufanye maendeleo kisha baadaye ndio tule BATA.

Watu wa Pwani wakiongoza nchi hii, huwezi sikia maumivu ya watu kuuawa, kutekwa, na kufanywa vilema vya maisha.

Watu wa Pwani Kwa mdomo ndio kwao, hawaogopi kusema, kutupiwa maneno na kutukanwa.
Ndio maana wao wanangoma zinaitwa Vigoma Kwa ajili ya kuchambia na kusuta watu. Hivyo wao kusutana na utamaduni.
Ila kuuana ni nadra Sana.

Mwisho niseme,
Hakuna Bora ndani ya nchi hii.
Kila upande unamanufaa makubwa katika nchi hii.
Hivyo ni vyema taasisi nyeti za nchi zipange watu na kuwapa MAJUKUMU kulingana na Asili yake, ili kuleta ufanisi.

Lakini unampa mtu Urais mwenye asili ya watu wenye hasira unategemea nini Kama sio watu kuumia.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Vikindu, Pwani
Karibu TANGA taycoon wa fasihi
 
Hahahah
Wakarimu sana watu wa pwani. Unamkuta ameketi kwenye mkeka wake anakula mihogo Ila lazima atakukaribisha japo ukate kipande.

Nikienda shambani unamwambia nipatie Nazi unashangaa anakwea mnazi anaangua na anafua dafu anakupa Nazi hata kumi mpaka inakubidi uone haya japo umpe hata elfu mbili ya sukari.

Sema wambea hao[emoji2][emoji2][emoji2] hawana dogo Wala kubwa. Wanajua kumsuta mtu mpaka unazimia[emoji2][emoji2]
 
Back
Top Bottom