Pamoja na mbwembwe zote LATRA hawajafikia ubora wa Scandinavia Bus sekta ya usafiri wa abiria!

Pamoja na mbwembwe zote LATRA hawajafikia ubora wa Scandinavia Bus sekta ya usafiri wa abiria!

Scandnavia mie sioni kama ni mfano bora wa uendeshaji wa kampuni za mabasi - kwa kule kushindwa kwake kuwa endelevu.
 
Scandinavia ilifanya vizuri sababu allikuwa na meneja uendeshaji mzungu mwenye uzoefu toka ulaya .
[emoji867]
Kwahiyo ambao sio wazungu hawana uwezo wa kuendesha makampuni
Bado tutatawaliwa na wazungu saana kwa fikra hizi
Suala la ufanisi katika Uongozi na kuendesha mashirika ya biashara halihusiani kabisa na kutawaliwa,
hii ni habari ya uchumi na uongozi. Huyo mzungu unaweza kumleta kama expert tuu yaliyobaki chini yake tuwepo sisi wenyewe Africans.
Hwa jamaa kitu DISCIPLINE katika utendaji wa kazi zao ndio priority yao
 
Kwamba huo mfumo wa online ticketing scandnavia wakishakuwa nao miaka yake 2000 huko ... Leo LATRA ndio wanauintroduce miaka 21 mbele!!?? Hauoni hoja yake bado !!???
Ndio nasema,hiyo ni kampuni ya basi na nyingine ni mamlaka!Kulinganisha kampuni ya mabasi na mamlaka ni vitu viwili tofauti!
Ilichokifanya LATRA ni kuweka ulazima wa mabasi kuwa na online ticketing,lakini huko mwanzo Sumatra walifanya jambo hilo kuwa optional!
Sasa kuja hapa kufananisha Mamlaka ambayo ni msimamizi na kampuni ya mabasi unaona ni sawa?Doesnt make any sense!
 
Hoja yake ni kwamba LATRA ndiye regulator wa usafiri wa ardhini; je, itaweza ku-regulate usafiri wa mabasi ufikie kiwango japo cha Scandinavia?
Msimamizi ameweka viwango vyake, mtoa huduma anatakiwa avitimize mamlaka inayosimamia kuondoka na kufika kwa mabasi siyo jukumu la LATRA ni jukumu la Trafiki kwani sheria za mwendo haziko LATRA ila wao wanaweza kusimamia haki za abiria ndani ya mabasi endapo abiria watatoa taarifa kuwa vitu vilivyoorodheshwa kwenye daraja la basi hawavipati, ujue si rahisi LATRA kusimamisha basi njiani na kuwauliza abiria kama wamekunywa soda.
Hiyo Scandinavia ninaifahamu sana tangu ikiwa na njia moja tu ya Iringa kituo chake kikiwa hoteli ya Prinsesi Mnazimmoja na kuongeza njia ya Dodoma na Kyela, nayo ilikuwa na mapungufu mengi sana kuliko mnavyodhani.
 
Hili halikuwa na mpinzani

View attachment 1669602
lakini hata uda enzi za Ikarus nayo yalipeta
View attachment 1669603
Hilo basi IKARUS viongozi wengi wa sasa wa CCM hawalijui ndiyo maana wanashabikia ya mchina ambayo hayakawii kuungua, lakini miaka ya sitini kulikuwa mabasi ya ghorofa kama ya Landani ambayo aliyaacha mkoloni! Sijui hawa wa mwendokasi wanaringia nini! Usingizi wa pono wa watanzania?
 
Jamaa unapenda kuanzisha nyuzi sana!Wakati mwingine ni hoja nyepesi kabisa!Sasa kweli unafananisha mamlaka ya usimamizi wa usafiri wa ardhini na Kampuni moja ya basi,kweli?
Sijui hata ulitaka kusemaje hapa?Ndio madhara ya kutaka uandike wewe kila mara,unaishia kutoa mvuke tu!

Nimekuelewa Mr!Mchango mzuri saana
 
Kuna watu mnashuka point hadi raha. Wapuuzi wamejaribu kuleta siasa wamepotezewa.

Raha ya majadiliano ni point zilizoshiba
 
Tatizo la usimamizi mbovu ni janga kwa Waafrika kwa ujumla...

Ni kitu cha kawaida sana sasa hivi kitu kipya kilichoanzishwa kuharibika au uendeshaji wake kuyumba yumba

Scandinavia ilifanya vizuri sababu allikuwa na meneja uendeshaji mzungu mwenye uzoefu toka ulaya .Mkataba ulipoisha akaondoka akapewa mswahili kampuni ikaanza kuyumba

Tatizo la kampuni zetu sio wamiliki hasa. Wamiliki wanajitahidi mno kutafuta mitaji lakini menejimenti zinawangusha haziko competent nafikiri kuboresha serikali iwe inaruhusu tu na kushauri private sector wakiona wanakwama waajiri toka nje
 
Ndio nasema,hiyo ni kampuni ya basi na nyingine ni mamlaka!Kulinganisha kampuni ya mabasi na mamlaka ni vitu viwili tofauti!
Ilichokifanya LATRA ni kuweka ulazima wa mabasi kuwa na online ticketing,lakini huko mwanzo Sumatra walifanya jambo hilo kuwa optional!
Sasa kuja hapa kufananisha Mamlaka ambayo ni msimamizi na kampuni ya mabasi unaona ni sawa?Doesnt make any sense!
Ndio maana wenye akili wamelinganisha menejimenti ya mzungu pale Scandinavia na Latra.

Wewe endelea kukariri bwashee!
 
Jamaa unapenda kuanzisha nyuzi sana!Wakati mwingine ni hoja nyepesi kabisa!Sasa kweli unafananisha mamlaka ya usimamizi wa usafiri wa ardhini na Kampuni moja ya basi, kweli?

Sijui hata ulitaka kusemaje hapa? Ndio madhara ya kutaka uandike wewe kila mara,unaishia kutoa mvuke tu!
Kweli kabisa, nilizani ni kampuni mpya ya mabasi.

Sent from my SM-A415F using JamiiForums mobile app
 
Msimamizi ameweka viwango vyake, mtoa huduma anatakiwa avitimize mamlaka inayosimamia kuondoka na kufika kwa mabasi siyo jukumu la LATRA ni jukumu la Trafiki kwani sheria za mwendo haziko LATRA ila wao wanaweza kusimamia haki za abiria ndani ya mabasi endapo abiria watatoa taarifa kuwa vitu vilivyoorodheshwa kwenye daraja la basi hawavipati, ujue si rahisi LATRA kusimamisha basi njiani na kuwauliza abiria kama wamekunywa soda.
Hiyo Scandinavia ninaifahamu sana yangu ikiwa na njia moja tu ya Iringa kituo chake kikiwa hoteli ya Prinsesi Mnazimmoja na kuongeza njia ya Dodoma na Kyela, nayo ilikuwa na mapungufu mengi sana kuliko mnavyodhani.
Uliposema Latra haisimamii ratiba za mabasi ndio nimechoka kabisa maana yake hata hujui kwa sasa kidhibiti mwendo cha mabasi kinasomewa wapi.

Stendi ya kwanza ya Scandinavia ilikuwa mtaa Congo nyuma ya DDC Kariakoo baadae ikahamia mnazi mmoja jirani na Juwata sasa mnaita Tucta na mwisho ikahamia Kamata.

Bus ya kwanza ilikuwa TZ 42604

Maendeleo hayana vyama!
 
Ccm ni lichama la kigaidi hawana wanachokifikiria cha kumnufaisha mwananchi wao wanawaz kuwakamua wanaojitutumua
 
Sijachanganya madesa hapa, Mwaka 2012 Kuna gari ilikuja ilikuwa unapiga route ya Mbeya Dsm iliitwa green star, ulitumia ofisi za Scandinavia hapo Morogoro. Na ilikufa mapema Sana, saiz haipo .

Sent using Jamii Forums mobile app
Hao walikuwa ni watu wengine walichukua hata ofisi zilizoachwa na Scandinavia pale Ubungo
 
Back
Top Bottom