Pamoja na mbwembwe zote LATRA hawajafikia ubora wa Scandinavia Bus sekta ya usafiri wa abiria!

Pamoja na mbwembwe zote LATRA hawajafikia ubora wa Scandinavia Bus sekta ya usafiri wa abiria!

Scandinavia ilifanya vizuri sababu allikuwa na meneja uendeshaji mzungu mwenye uzoefu toka ulaya .Mkataba ulipoisha akaondoka akapewa mswahili kampuni ikaanza kuyumba.

Tatizo la kampuni zetu sio wamiliki hasa. Wamiliki wanajitahidi mno kutafuta mitaji lakini menejimenti zinawangusha haziko competent nafikiri kuboresha serikali iwe inaruhusu tu na kushauri private sector wakiona wanakwama waajiri toka nje.
Kumbe mabeberu yana tija kwa taifa noma sana
 
Scandinavia vs latra??

Latra hawa tawi la Sumatra?? Aka regulators?

Itakua hainihusu ndo maana sijaelewa.
Mkuu huyu jamaa kachemsha ila kaamua kufa kisabuni!Anapambana mpaka anatoka nje ya mada yake mwenyewe,sasa wachangiaji wengine sijui wafanyeje?
 
Tokea umeanza kuitaja hiyo mbege,inaonekana ni kinywaji chako pendwa!
Uko nje sana ya mada yako mwenyewe,what a shame!
Mimi nakunywa mbege na ni kinywaji pendwa kabisa ndio maana nakusisitiza meku mwenzangu endelea kushushia na kisusio ile Konyagi tuwaachie wasioanguka!
 
Mimi nakunywa mbege na ni kinywaji pendwa kabisa ndio maana nakusisitiza meku mwenzangu endelea kushushia na kisusio ile Konyagi tuwaachie wasioanguka!
Nje kabisa ya mada yako mwenyewe!Siku nyingine andika vitu vyenye logic kuepuka kuikimbia mada yako mwenyewe na kujikita kwenye utopolo kama huu unaoandika!
Ujumbe umefika,naishia hapo!
 
Alaaniwe aliyeshiriki kuiua Scandinavia kwa zile huduma za miaka ile sijaona kampuni yoyote kwa sasa ambayo inafikia
Hakuna kampuni pale stand ilikuwa kama airport kabisa ikiwa na maelfu ya ajira kiukweli mtu alikuwa huwezi na tofauti ya kupanda ndege na basi tofauti ilikuwa labda muda tu gari inaochukua njiani

Hadi sasa hakuna kampuni imefikia viwango vile Afrika Mashariki na Kati yote hakuna ambaye kaifikia ile standard
 
Sekta ya usafirishaji huduma sio rafiki kabisa.

Magari mengi ni mabovu mno, naona kama imeamuliwa yawepo tu ili kupunguza uhaba lakini kwa mtazamo wangu hayafai kubeba abiria kabisa.

Unakuta viti vimechakaa, AC hazifanyi kazi, ndani kuna wadudu kama mende kwakweli hali ni mbaya,

Trafiki nao wanasema wanafanya ukaguzi sijui wanafanya ukaguzi gani maana unakuta gari ni bovu lakini linabeba abiria na lipo bara barani.

Kuna haja ya wamiliki kuboresha usafiri jamani,

Abiria akilipa nauli ana haki ya kupata huduma bora na si bora huduma.
 
Hakuna kampuni pale stand ilikuwa kama airport kabisa ikiwa na maelfu ya ajira kiukweli mtu alikuwa huwezi na tofauti ya kupanda ndege na basi tofauti ilikuwa labda muda tu gari inaochukua njiani

Hadi sasa hakuna kampuni imefikia viwango vile Afrika Mashariki na Kati yote hakuna ambaye kaifikia ile standard
Unaijua Afrika ya Kati ina nchi ngapi! Mbona stesheni za Relwe Kyela, Mbeya, Iringa, Itigi na nyinginezo zilikuwa na mgahawa na chumba cha kulala wasafiri huku wakilindwa na ndio walioanza kuwa na mabasi yenye vyoo. Wakati mnaisifu Scandinavia Buffalo alikuwa na mabasi yenye choo.
 
Unaijua Afrika ya Kati ina nchi ngapi! Mbona stesheni za Relwe Kyela, Mbeya, Iringa, Itigi na nyinginezo zilikuwa na mgahawa na chumba cha kulala wasafiri huku wakilindwa na ndio walioanza kuwa na mabasi yenye vyoo. Wakati mnaisifu Scandinavia Buffalo alikuwa na mabasi yenye choo.
Relwe waliokuwa wakikata zile tiketi ngumu za mabox ya viatu sio za karatasi? Hiyo stand ilikuwa na viti vizuri na A.C. vya abiria kama scandinavia?
 
Katika suala la uongozi na usimamizi wa mambo, mzungu ni best.
Sisi waafrika tunawezakufanya kazi nyuma yao vizuri tuu
Hata Uongozi wa nchi, kama tutampa Uraisi Mzungu leo na Magu awe chiniyake basi utaona mabadiliko makubwa na ukata utaondoka na Tanzania itageuka kuwa nchi ya dunia ya kwanza mara moja.

Sisi Afrika suala la Utawala si letu.

Nakumbuka miaka ile kuna siku Rais Mwinyi alikuwa akihutubia watendaji wa bandari kuhusu huduma mbovu; akatoa hadithi kuhusu kikao chake kimoja na Rais wa Malawi wa wakati huo, Kamuzu Banda. Akasema:

“Banda akaniambia ‘unajua bwana mdogo, bandari yako (DSM) ndiyo nafuu sana kwetu; ipo karibu na usafiri (access) sio tatizo. TATIZO ni kuwa mizigo yetu ikifika pale clearance inachukua wiki tatu hata mwezi. Malipo kibao pamoja na rushwa. Mwishowe, mzigo ukiupata basi umepungua, vitu vimeshachomolewa. Tokea hapo hadi kuvuka mpaka ni usumbufu njia nzima.

Ndio maana tumeamua kutumia bandari ya Durban iliyo mbali zaidi ya mara mbili ya DSM. Kule, clearance ni siku 3 maximum na mzigo unaupata kamili kisha unavuka boda bila mikwaruzo. Gharama inakuwa chini ya DSM.

Siri ya Durban ni kuwa pale kuna MZUNGU! Ukiwa tayari niarifu nikuletee mzungu hapo DSM. Nakuhakikishia akikaa mzungu pale, majirani wote hata wa mbali wanahamia hapo!’

Kufikia hapo, Rais Mwinyi akawageikia mabosi wa serikali na bandari akawauliza: “ndugu zangu, kweli mnataka nikuleteeni mzungu wa Banda akusimamieni? Semeni. Mimi Niliona haya sana kwa fedheha hii. Nilimjibu mzee Kamuzu kuwa bado hatujaharibikiwa kiasi hicho; nikamhakikishia kuwa tutajirekebisha”. Watu walicheka sana.
 
Hawa Green star walikuwa ni wale wale

Sent using Jamii Forums mobile app
Scandinavia ilikabiliwa na madeni toka Benki ya Maendeleo Africa, kuna wakati benki hiyo ilikamata mabasi yao na kuyafungia Temeke kwenye yadi ya serikali. Siasa ukiingia kichwakichwa ni mbaya, yule mzee alijifanya kada tajiri wa CCM, akachukua mabasi kupeleka watu bure kwenye ufunguzi wa daraja la Mkapa! Benki ilipoona hivyo huku akitoa visingizio kushindwa kulipa deni, wakashikilia mabasi na CCM haikuikataza benki hiyo kwani ni ya nje, huo ukawa mwisho wa Scandinavia.
 
Nimejaribu kufuatilia kwa karibu maboresho yanayofanywa na LATRA kwenye sekta ya usafiri wa abiria lakini sijaona Jipya.

Nikikumbuka kampuni yangu pendwa ya mabasi ya Scandinavia naona viwango walivyovifikia wakati wanafunga kampuni bado havijafikiwa na hawa Latra.

Mambo ya online booking na ticketing walishakuwa nayo achilia mbali vikorombwezo vingine kedekede safarini ikiwemo viburudisho na magazeti.

Bus ziliondoka kwa muda sahihi na hapakuwepo usumbufu wowote safarini.

Maendeleo hayana vyama!
hiyo SCANDNAVIA kwanini ilifilisika?
 
Back
Top Bottom