Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 21,490
- 38,302
Tunajua kwamba Mch Msigwa alichukua kozi ya week tatu kusomea uchungaji.
Tunafahamu tena pasipo shaka elimu ya Msigwa juu ya theology ni ndogo sana na ikitokea akaenda katika makanisa ya kueleweka labda atapewa nafasi ya kufundisha watoto wadogo kuimba na kucheza.
Kwa hakika Mch Msigwa hawezi kwenda Catholic,Lutheran au Anglican.
Mch Msigwa hajawahi kubeba MSALABA alama kuu katika Ukristo.
Mch Msigwa kabeba picha ya Rais Samia kwa heshima na ishara kuu ya imani yake.Msigwa kafanya yote lakini bado CCM wametafuna kichwa chake.
Nimeamini linapokuja swala la maslahi CCM hawana mswalie Mtume.
Tunamsubiri Msigwa katika teuzi za ukuu wa Wilaya au uDED.
Ngongo kwasasa Siha.