Nina rafiki zangu identical twins,walizaliwa wanafanana kila kitu,
Ilikuwa ngumu kuwatofautisha
Kupanga ni kuchagua,Kurwa aliamua kusoma sasa yupo TRA
Doto ni dalali tu mtaani
Sasa tofauti yao iko bayana Kurwa anangara maana hapigwi jua maisha yake ni full kiyoyozi
Doto kapauka
Hawafanani tena
Diamond zamani alikuwa na mdomo kama chai jaba
Mdomo ulipotea ghafla baada ya kupata pesa
Harmonise sura yake imeendelea kufanana na harmorapa hakuna tofauti
Sura imegomea pesa.
Mimi mzee wenu kwa sasa sipendi kujiangalia kwenye kioo,nimepauka mbaya tofauti na enzi zangu nilivyokuwa sina majukum
Hapa chini ni mwamba wa Lusaka tripple C kabla hajapata hela.kapauka kama kibaka wa Kariakoo.pesa sabuni,sasa anawaka