Mr Antidote
JF-Expert Member
- Jan 11, 2015
- 953
- 1,304
- Thread starter
- #121
Kimsingi nafasi ya Simba kuwa bingwa imepungua sana kutokana na kutokuwa makini kwenye kumaliza mchezo.
Ktk project kuna kazi zinaitwa critical activities. Simba pamoja na kuwa timu bora kuliko zote ktk ligi ya mwaka huu wanashindwa kumaliza mchezo mapema hasa baada ya kuchungulia ratiba ilivyokaa ovyo.
Baada ya kufanya kazi nzuri kwa kumgonga Yanga, hawakupaswa kuziacha pointi 2 za Mbeya City wala hizi za Kagera.
Kazi imekuwa ngumu sana japo lolote linaweza kutokea
Kweli kabisa, Simba wanakosa focus, unawezaje kumfunga Yanga halafu mechi inayofuatia badala matokeo hayo yawe kichocheo cha ushindi nyie ndio mnaharibu.
Jambo lingine ni kucheza mpira kipindi cha pili na kurelax cha kwanza, hiyo ni strategy mbovu sana ndio maana mara nyingi Simba wanahaha kurudisha mabao yanayofungwa kipindi cha kwanza.
Cha mwisho pia kipa wetu awe makini na baadhi ya mipira inayopigwa toka mbali, anakuwa anajiposition vibaya sana. Kipa wetu bado hajaonekana kuwa ni match saver mara mabeki wanapokuwa wamepitwa.
Vumilieni tu wakuu hakuna namna au mjipange tena mwakani au mkomae na FA tena muombe mkutane na Yanga ili mchukue inaonesha hiyo ndio timu mliojipanga isiwafunge kwa hali na mali mkasahau kwenye mashindano hakuna Yanga pekee.