Habari wadau,
Kama heading inavyojieleza hapo juu, nilikua napitia pitia ratiba za mechi za ligi kuu vpl zilizobaki kati ya simba na yanga nimekuja kugundua simba ana ratiba ngumu ikimsubiri mbele yake kuliko yanga.
Kila timu imebakisha mechi sita ili ligi kufikia ukingoni na simba ikiwa juu kwa tofauti ya point mbili.
Ukitazama kati ya mechi hizo 6, simba ana mechi 3 za ugenini dhidi ya kagera sugar, toto african na mbao fc. Unaweza kuona ni mechi rahisi lakini si rahisi kwa simba kuibuka na point zote 9 huko kanda ya ziwa japo ni jambo linalowezekana pia.
Pia simba ana mechi 3 ambazo atamalizia Dar dhidi ya Mwadui, stand na African lyon. Japo zinaonekana ni timu dhaifu lakn African lyon hawatabariki sometimes wanakua kama hamorapa kiboko ya mabishoo.
Ukirudi kwa hawa wamatopeni aka vyura almaarufu wa kimataifa ukipenda waite wazee wa arosto, wao wana mechi 5 nyumbani dhidi ya mbeya city, kagera, toto, prisons na azam fc.
Pamoja kuwa na mechi ngumu dhidi ya azam na mbeya city ila kucheza dar kunaweza kuwa catalyst kwao na kuweza kukusanya points nyingi kulinganisha Na simba aka wazee wa mchangani.
Sisemi Yanga ni lazima awe bingwa ila kwa kuangalia ratiba yake ilivyokaa ukiilinganisha na simba basi kama wakichanga karata zao vizuri watoto wajangwani wataibuka kidedea kwa msimu watatu mfulululizo.
Wazee wa mchangani na wazee wa arosto karibuni kutoa mapovu