Pamoja na Simba sc kuongoza ligi lakini Yanga wana nafasi kubwa ya kuwa bingwa

Pamoja na Simba sc kuongoza ligi lakini Yanga wana nafasi kubwa ya kuwa bingwa

Mpira Hauchezwi Kwa Hesabu Za Vidole....
Wekaga akiba ya maneno. Niliwapa equal chance ila based on fixtures Ukweli ndo huo niliouweka hapo. Labda ungejaribu kupiga hesabu zako na wewe tuzione.

By the way kumeitika huko kaitaba Wao 2 nyie 1
 
Habari wadau,

Kama heading inavyojieleza hapo juu, nilikua napitia pitia ratiba za mechi za ligi kuu vpl zilizobaki kati ya simba na yanga nimekuja kugundua simba ana ratiba ngumu ikimsubiri mbele yake kuliko yanga.

Kila timu imebakisha mechi sita ili ligi kufikia ukingoni na simba ikiwa juu kwa tofauti ya point mbili.

Ukitazama kati ya mechi hizo 6, simba ana mechi 3 za ugenini dhidi ya kagera sugar, toto african na mbao fc. Unaweza kuona ni mechi rahisi lakini si rahisi kwa simba kuibuka na point zote 9 huko kanda ya ziwa japo ni jambo linalowezekana pia.

Pia simba ana mechi 3 ambazo atamalizia Dar dhidi ya Mwadui, stand na African lyon. Japo zinaonekana ni timu dhaifu lakn African lyon hawatabariki sometimes wanakua kama hamorapa kiboko ya mabishoo.

Ukirudi kwa hawa wamatopeni aka vyura almaarufu wa kimataifa ukipenda waite wazee wa arosto, wao wana mechi 5 nyumbani dhidi ya mbeya city, kagera, toto, prisons na azam fc.

Pamoja kuwa na mechi ngumu dhidi ya azam na mbeya city ila kucheza dar kunaweza kuwa catalyst kwao na kuweza kukusanya points nyingi kulinganisha Na simba aka wazee wa mchangani.

Sisemi Yanga ni lazima awe bingwa ila kwa kuangalia ratiba yake ilivyokaa ukiilinganisha na simba basi kama wakichanga karata zao vizuri watoto wajangwani wataibuka kidedea kwa msimu watatu mfulululizo.

Wazee wa mchangani na wazee wa arosto karibuni kutoa mapovu
Acha ndoto za mchana
 
Wekaga akiba ya maneno. Niliwapa equal chance ila based on fixtures Ukweli ndo huo niliouweka hapo. Labda ungejaribu kupiga hesabu zako na wewe tuzione.

By the way kumeitika huko kaitaba Wao 2 nyie 1
Tartiiiibu yameanza kutumia. Kweli kabisa ni vyema kuweka akiba ya maneno or else kuyatumia kwa hekima.
 
single touch double manifestation, Yanga bingwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa, poleni sana wazeee wamchangani.
 
Tartiiiibu yameanza kutumia. Kweli kabisa ni vyema kuweka akiba ya maneno or else kuyatumia kwa hekima.
Well said mkuu, Tatizo hawa jamaa wa msimbazi walidhani nipo hapa kuwanyanyua watoto wa jangwani. Wao wanaongelea ushabaki na unazi. Ila ukweli utabaki kuwa ukweli. Simba ratiba yao imekaa vibaya na imeanza kuwahukumu sasa.

Pamoja Yanga kuwa na majeruhi wengi ila viwango vya wachezaji wao wa akiba bado vinaweza kumudu mechi zao zilizobaki.
 
single touch double manifestation, Yanga bingwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa, poleni sana wazeee wamchangani.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Mkuu pole pole basi usiongezee stress nyasi bado hazijalipiwa ujue.
 
Leo ndo nilidhani simba wangeambulia pointi 3 lakini kwa Mbao na Toto yetu masikio. Hata hivyo adui yako muombee njaa tu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Mkuu imebadilika siku hizi eti wanasema adui muombee maisha marefu aone mafanikio yako. [emoji23][emoji23][emoji23]
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] mkuu nawao pia watu usiwafanyie hivyo majirani
Simba wangetufanya tusilale leo kwa kelele zao.
Yanga wakija teleza na simba wakashinda tutakubali matokeo, but for now, nawaomba waseme maneno hayo matatu "YANGA BINGWA TENA"

C:\Users\user\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image002.jpg
 
mbona unaandika kutusifia sana wanajangwani kana kwamba wewe ni mmoja wetu, ila sio mbaya unakaribishwa chama la wananchi
 
mbona unaandika kutusifia sana wanajangwani kana kwamba wewe ni mmoja wetu, ila sio mbaya unakaribishwa chama la wananchi
Hahaha mkuu mi ni mmoja wao kati ya wa kimataifa.
 
Simba wangewekeza nguvu kwenye FA cup tu huku kwingine watausikia tu ubingwa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Mkuu usiwafanyie hivyo wenzio....BTW Azam na yeye anakutolea macho huko. Au kashatoka Azam?
 
Simba wangetufanya tusilale leo kwa kelele zao.
Yanga wakija teleza na simba wakashinda tutakubali matokeo, but for now, nawaomba waseme maneno hayo matatu "YANGA BINGWA TENA"

C:\Users\user\AppData\Local\Temp\msohtmlclip1\01\clip_image002.jpg
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Hiyo naitwa jino kwa jino. Naona hutaki ujirani mkuu
 
Bado mwanza mkuu,awatoamin watakachokutana nacho kanda ya ziwa

Sent from my LG-D858HK using JamiiForums mobile app
Wasi wasi wangu ni fitina za wale watu jangwani. Kama nawaona wanavyowatia ndimu Toto African kumrahisishia kazi Baba yao. Mkuu, hawa jamaa wa mchangani wasipokua makini wanaeza jikuta wanakunywa chai kwa uluzi.
 
Back
Top Bottom