Pamoja na ufaulu kupanda, shule za kata Dar hali ni mbaya, Division Zero ni nyingi sana, Afisa Elimu aondolewe

Pamoja na ufaulu kupanda, shule za kata Dar hali ni mbaya, Division Zero ni nyingi sana, Afisa Elimu aondolewe

Unaambiwa kulipa ada ni matumizi mabaya ya fedha. Eti "ufanye uwekezaji" huku mwanao analima miswaki na zero zisizohesabika, wewe unamnunulia vipande vya 20×20 eti chuo atakutana nao hao kina St. Francis.

Mwisho wa siku unakula za uso, anatoka anastahili fani ya uyaya na umamantilie posho alfu tano kwa siku😂
Huyo anayefika chuo anajitofautisha vipi na huyo aliyepata zero kwa sasa Tanzania ? Au kujitolea kufundisha bure ?
 
Afisa elimi ndio anasomea wanafunzi, tatizo mfumo wetu wa elimu ni mbovu kwanzia ngazi ya chini hadi juu mavyuoni, ni elimu ambayo ni pyramid.
 
Tatizo wanafunzi hawataki kusoma buzy wapo tiki toki kufanya challenge
 
  • Thanks
Reactions: K11
Hao Kitunda sekondari wanaenda chuo kikuu kuuza ubuyu au kitu gani?
Hao wanaoenda chuo kikuu wakitoka wanakuja kuuza ukwaju wa bakhresa na hao wa kitunda,kusajili laini na hao wa kitunda, kukimbiza boda boda na hao wa kitunda, kuwa wachekeshaji mitandaoni na hao wa kitunda au nakosea ?
 
Afisa elimi ndio anasomea wanafunzi, tatizo mfumo wetu wa elimu ni mbovu kwanzia ngazi ya chini hadi juu mavyuoni, ni elimu ambayo ni pyramid.
Hao wanafunzi wamefili sababu walimu wao wamegoma kuwafaulisha, elewa neno kuwafaulisha
 
matokeo ya form four kwa mwaka 2024 yametangazwa leo.
Kwa mujibu wa baraza la mitihani, ufaulu umepanda kwa asilimia tatu.

Ila huku kwenye shule za kata hali mbaya. Unakuta nusu ya wanafunzi wamefeli vibaya mno katika shule husika.

Mfano shule kama Kitunda hali ni mbaya, wanafunzi 249 wamepata division zero. Unajiuliza hii shule ina uongozi kweli? Afisa Elimu nae analipwa mshahara kabisa? Nini kifanyike wakuu?View attachment 3211475

View attachment 3211479

View attachment 3211481

View attachment 3211491

View attachment 3211492

Soma: NECTA yatangaza matokeo ya kidato cha nne 2024. Yatazame hapa!
Shuke za Kata mazingira ya kujifunzia ni mabaya.
Uwezi amini kuona wanafunzi wengi wanakaa Chini. Tembelea shuke hata za Mkoa wa Dar na Pwani ambazo viongo wa nchi wapo Karibu na huzipita mara kwa mara. Tuna safari ndefu kwakweli. Shule zingine wanafunzi waliochaguliwa kidato cha Kwanza Wazazi wanashauriwa kuwanunulia Viti na meza watoto wao.
 
Hao wanaoenda chuo kikuu wakitoka wanakuja kuuza ukwaju wa bakhresa na hao wa kitunda,kusajili laini na hao wa kitunda, kukimbiza boda boda na hao wa kitunda, kuwa wachekeshaji mitandaoni na hao wa kitunda au nakosea ?
Ajira hakuna na siku hizi ajira imegeuka kua bahati
 
Shule za kata hali ni mbaya. Imagine Tanzania tuna shule za kata zaidi ya 1000 alaf shule ya kata moja inatoa zero 100. So hapo madogo kama 100,000 wanakimbilia mtaani kwenye "survival of the fittest"
 
matokeo ya form four kwa mwaka 2024 yametangazwa leo.
Kwa mujibu wa baraza la mitihani, ufaulu umepanda kwa asilimia tatu.

Ila huku kwenye shule za kata hali mbaya. Unakuta nusu ya wanafunzi wamefeli vibaya mno katika shule husika.

Mfano shule kama Kitunda hali ni mbaya, wanafunzi 249 wamepata division zero. Unajiuliza hii shule ina uongozi kweli? Afisa Elimu nae analipwa mshahara kabisa? Nini kifanyike wakuu?View attachment 3211475

View attachment 3211479

View attachment 3211481

View attachment 3211491

View attachment 3211492

Soma: NECTA yatangaza matokeo ya kidato cha nne 2024. Yatazame hapa!
Hiyo kitunda ukiangalia uwingi wa wanafunzi,mazingira na vitendea kazi vya walimu,naipa points nyingi zaidi ya shule 10 bora,imagine ina wanafunzi zaidi ya 600,walimu awazidi 15 tena walimu wenye stress za mikopo wamepata 1 to 3 wanafunzi zaidi ya 80
 
Back
Top Bottom