Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndio, shule zote zinazoongoza kufaulu zina mabweni. Ukiona mwanafunzi anakaa bweni halafu kafeli basi huyo alipanga kufeli.Nakubalina na wewe mabweni yanaweza saidi kukuza elimu, sambamba na kukomesha utoro wa wanafunzi hasa kupenda kwenda kuogelea baharini wakati wa masomo
Naon upo kisiasaPale juu umesema walimu wanadharauliwa ila wanafanyaje?
Tofauti ni kwamba matokeo tumeyaona na wamelamba miswaki na zero.Hao wanaoenda chuo kikuu wakitoka wanakuja kuuza ukwaju wa bakhresa na hao wa kitunda,kusajili laini na hao wa kitunda, kukimbiza boda boda na hao wa kitunda, kuwa wachekeshaji mitandaoni na hao wa kitunda au nakosea ?
Hao waliopata division one na wale wa zero baada ya miaka michache mbeleni, wote watakutana kwenye kuendesha bodaboda. Trust me..Ndugu yangu LIKUD unaonaje hiyo shule ya Kitunda ni kayumba inayomfaa mwanao maana wewe hutaki EM schools.
Wakati mwanao anaambulia miswaki wewe unamfanyia "uwekezaji" ili usitumie hela bure kulipa ada. Akitoka hapo na zero, aje awashinde wale kina St. Francis kwenye ufaulu wa chuo cha ndotoni, maana kwa matokeo hayo chuo kikuu its likely atakisikia kwenye redio. Labda ianzishwe kozi ya uyaya.
Kwani mtoto anafaulu kwa kuadhibiwa?Kwani afisa elimu ndo kafanya mitihani kumbuka wingi wa shule za shule za serikali kuchangia kuleta matokeo mabovu watoto mchelemchele wakiguswa wazazi na walezi midomo juu walimu wafanye nn zaidi ya kukaa kimya mambo yajiendee
Kwani nani anajukumu la kuwaadabisha hao wacheza singeli na wavuta bangi?Yaani watu wanasikitika kuona machangu, wacheza singeli, maafisa ubashiri, wavuta bangi, walevi, n.k n.k wamekata sufuri.
Great Thinkers wa JF ya zama hizi bhana.
Walimu pokeeni matusi wiki hii.
Wanafunzi wa kike shule za sekondari nyingi Mtwara wanadanga na wazazi ni kama wamebariki kabisa
Ifike mahali sasa serikali ifanye uamuzi wa busara. 1. Ipunguze umri wa mwanamke kuruhusiwa kuingia katika ndoa kutoka miaka 18 hadi ( 14 & 15) kwa watu wa dini zote sio waislamu pekee maana sheria ya Ndoa ya mwaka 71 inasema kwamba mtoto wa kike Muumini wa dini ya kiislamu anaruhusiwa kuingia...www.jamiiforums.com
LIKUD yupo sahihi. Kuna graduates hata huo umamantilie wana ulilia bila mafanikio..Unaambiwa kulipa ada ni matumizi mabaya ya fedha. Eti "ufanye uwekezaji" huku mwanao analima miswaki na zero zisizohesabika, wewe unamnunulia vipande vya 20×20 eti chuo atakutana nao hao kina St. Francis.
Mwisho wa siku unakula za uso, anatoka anastahili fani ya uyaya na umamantilie posho alfu tano kwa siku😂
Una data?KAYUMBA schools za Likudi ndiyo chanzo Cha zero Kwa wanafunzi.Hakuna hata EMs Moja ambayo mwanafunzi wake hata mmoja ambaye amepata daraja la sifuri.
Hao divisions one wako, baada ya kumaliza chuo kikuu, utawakuta wanaendesha bodaboda kitaa..Hao Kitunda sekondari wanaenda chuo kikuu kuuza ubuyu au kitu gani?
Zero 249 Alafu niendelee kuhangaisha kichwa waangalie na ujuzi wa watu wasikae kuhangaisha vichwa zaidi for nothingmatokeo ya form four kwa mwaka 2024 yametangazwa leo.
Kwa mujibu wa baraza la mitihani, ufaulu umepanda kwa asilimia tatu.
Ila huku kwenye shule za kata hali mbaya. Unakuta nusu ya wanafunzi wamefeli vibaya mno katika shule husika.
Mfano shule kama Kitunda hali ni mbaya, wanafunzi 249 wamepata division zero. Unajiuliza hii shule ina uongozi kweli? Afisa Elimu nae analipwa mshahara kabisa? Nini kifanyike wakuu?View attachment 3211475
View attachment 3211479
View attachment 3211481
View attachment 3211491
View attachment 3211492
Soma: NECTA yatangaza matokeo ya kidato cha nne 2024. Yatazame hapa!
fatilia thread zake kwa umakini bila mahaba utamuelewa.KAYUMBA schools za Likudi ndiyo chanzo Cha zero Kwa wanafunzi.Hakuna hata EMs Moja ambayo mwanafunzi wake hata mmoja ambaye amepata daraja la sifuri.