Pamoja na ufaulu kupanda, shule za kata Dar hali ni mbaya, Division Zero ni nyingi sana, Afisa Elimu aondolewe

Pamoja na ufaulu kupanda, shule za kata Dar hali ni mbaya, Division Zero ni nyingi sana, Afisa Elimu aondolewe

Matokeo ya NECTA tumeyaona, miswaki tunaiona kwa kayumba.

Unayo matokeo ya wapika nyanya yanayosimamiwa na baraza lolote yanayoonyesha wamefanikiwa kuwashinda watu kama wa St. Francis????
Mbona wapo madogo waliosoma kayumba na wameondoka na 1.7.
 
  • Thanks
Reactions: K11
Uzi hauna la maana kabisaa Afisa Elimu anahusikaje hapo. Huenda kuna mambo mengi hapo, huenda wazazi hawajali, miundo mbinu na vifaa wezeshi havitoshi kutokana na umaskini, wanafunzi wengi kuliko idadi ya watu. Kusimamia taasisi kama huna uwezeshaji (facilities ni zero).
Wewe ni mchonganishi na unakoekekea utakuwa mchawi Poor Brain To yeye Evelyn Salt
 
Faida atakayokuwa nayo aliyepata zero ni kuijua mitaa mapema na jinsi watu wana hustle. So hata aliyepata one akaenda chuo akamaliza halafu akaiingia mtaani yule aliyepata 0 atakuwa na uhakika wa kusurvive kuliko huyu aliyepata 1 labda kama aajiriwe.
Juma Nature kazaliwa uswahilini na anaijua vizuri mitaa. Ni hilo group la Miswaki FC, aliishia elimu ya chini sana na alikuwa na muda mwingi kuijua mitaa na kupata umaarufu usio na nguvu ya elimu nyuma.

Fred Ngajiro "Vunjabei" ni mshamba wa kutoka kwa wauza mbao mkoani uko, hajui lolote kuhusu jiji na ana elimu ya juu (Master's) na alikuwa na ufaulu wa Division 1 kama sio 2.
Juma Nature anamzidi Vunjabei kimaisha??
 
Mbona wapo madogo waliosoma kayumba na wameondoka na 1.7.
Pia hospitalini kuna waliokunywa sumu ila wakatibiwa wakapona, na hapo utasema basi sumu kiwe kinywaji na kitozwe kodi.

Exceptions za mtu mmoja kati ya elfu 10 hazitoi mwongozo wa maisha yawe vipi.
 
Division one bila connections za maana ni sawa na takataka..
Mwenye Division 1 kashaipata ndio hivyo hata umuue haifutiki, mwenye Mswaki ndio hivyo ashaupata hata awe na connectio au hana.

Kama vipi mpeleke huyo kilaza mwenye sifuri ya Form 4 na connection awe hata Afisa Habari wa Vodacom uone kama connection uchwara zitamsaidia.
 
Juma Nature kazaliwa uswahilini na anaijua vizuri mitaa. Ni hilo group la Miswaki FC, aliishia elimu ya chini sana na alikuwa na muda mwingi kuijua mitaa na kupata umaarufu usio na nguvu ya elimu nyuma.

Fred Ngajiro "Vunjabei" ni mshamba wa kutoka kwa wauza mbao mkoani uko, hajui lolote kuhusu jiji na ana elimu ya juu (Master's) na alikuwa na ufaulu wa Division 1 kaka sio 2.
Juma Nature anamzidi Vunjabei kimaisha??
Sijasema mtu mwenye 0 atampita mwenye 1 kimaisha. Namaanisha pale mwenye 1 kamaliza chuo halaf kakosa ajira.
Balidi swali dogo kati ya Diamond na Vunjabei nani kasoma? Na nani kamzidi mwenzake kimaisha?
 
matokeo ya form four kwa mwaka 2024 yametangazwa leo.
Kwa mujibu wa baraza la mitihani, ufaulu umepanda kwa asilimia tatu.

Ila huku kwenye shule za kata hali mbaya. Unakuta nusu ya wanafunzi wamefeli vibaya mno katika shule husika.

Mfano shule kama Kitunda hali ni mbaya, wanafunzi 249 wamepata division zero. Unajiuliza hii shule ina uongozi kweli? Afisa Elimu nae analipwa mshahara kabisa? Nini kifanyike wakuu?View attachment 3211475

View attachment 3211479

View attachment 3211481

View attachment 3211491

View attachment 3211492

Soma: NECTA yatangaza matokeo ya kidato cha nne 2024. Yatazame hapa!
Lucas Mwashambwa Mama amewafikia wengi na machozi yanambubujika Kwa furaha. Elimu Bure na sera ya Ccm ya quantity isiyozingatia quality. Elimu ambayo watunga sera wanaogopa hata kuwapeleka watoto wao huko
 
Pia hospitalini kuna waliokunywa sumu ila wakatibiwa wakapona, na hapo utasema basi sumu kiwe kinywaji na kitozwe kodi.

Exceptions za mtu mmoja kati ya elfu 10 hazitoi mwongozo wa maisha yawe vipi.
Sijasema pia shule za kayumba ni bora kuliko za private.
 
Wakati wengine wanalia na zero, St francis wanafunzi wote 92 Wana division one point 7,
Kumbe ni 92 cream, nilidhani ni 600+.
Hivi mnalinganisha msjina ya shule au mfumo wa shule kwa ujumla.
Hata huko Kitunda kuna waliofaulu
 
  • Thanks
Reactions: K11
Uzi hauna la maana kabisaa Afisa Elimu anahusikaje hapo. Huenda kuna mambo mengi hapo, huenda wazazi hawajali, miundo mbinu na vifaa wezeshi havitoshi kutokana na umaskini, wanafunzi wengi kuliko idadi ya watu. Kusimamia taasisi kama huna uwezeshaji (facilities ni zero).
Wewe ni mchonganishi na unakoekekea utakuwa mchawi Poor Brain To yeye Evelyn Salt
❤️🥱🙏
 
Nitajia shule ya EM ambayo mwanafunzi wake kapata daraja la nne ambalo ni la mwisho
S0493 AL-HARAMAIN ISLAMIC SEMINARY

S1407 ARCH BISHOP KAHURANANGA SECONDARY SCHOOL

S0622 KUNDUCHI GIRLS' ISLAMIC HIGH SCHOOL

S0176 LUSANGI MORAVIAN JUNIOR SEMINARY

S1067 BISHOP ALPHA MEMORIAL HIGH SCHOOL

Pitia matokeo ya hizo shule kwa uchache kisha urudie kauli yako
 
Lucas Mwashambwa Mama amewafikia wengi na machozi yanambubujika Kwa furaha. Elimu Bure na sera ya Ccm ya quantity isiyozingatia quality. Elimu ambayo watunga sera wanaogopa hata kuwapeleka watoto wao huko
Wewe kama Mzazi pia una wajibu wa kutoa hamasa na kumsisitiza mwanao kusoma kwa bidii na siyo kuachia kazi hiyo kwa walimu pekee. Timiza wajibu wako vyema.
 
Sijasema mtu mwenye 0 atampita mwenye 1 kimaisha. Namaanisha pale mwenye 1 kamaliza chuo halaf kakosa ajira.
Hao madogo waliopata matokeo leo nani kakosa ajira mpaka uanze kusema mwenye zero amempita mwenye 1 kimaisha?

Mpaka sasa data zilizopo ni matokeo ya mtihani, wote walifanya mtihani uleule na huyu kapata 1 huyu kapata zero. Hayo mengineyo ya atafeli kimaisha ni sawa na maskini anavyojifariji kuwa "hata tajiri atakufa, hatozikwa na mali zake".
Balidi swali dogo kati ya Diamond na Vunjabei nani kasoma? Na nani kamzidi mwenzake kimaisha?
Diamond ana mtoto anayesoma kayumba, ili aje afanikiwa kwa kuimba kama yeye? Kama kayumba ni muhimu ungekutana na watoto wa Diamond wakienda chekechea za Tandale.

Hao waliopata miswaki wote hawatoimba kama Diamond, kipaji cha sanaa ni nadra kuliko elimu ya kufundishwa.

Mastaa waliokuwa wanahit miaka ya 2005 na wenye mafanikio sasa hivi ni wa kuhesabu. Naibu Waziri Mwana FA ana Masters, P Funk sio zero yule na ana maisha, Prof. Jay sio kilaza unamuona, Sugu sio mbumbumbu yule hajaishia Form IV wala kupata zero.
Aya upande mwingine wale design ya Kitunda sekondari unawaona kina Nature, Chid Benz.
 
matokeo ya form four kwa mwaka 2024 yametangazwa leo.
Kwa mujibu wa baraza la mitihani, ufaulu umepanda kwa asilimia tatu.

Ila huku kwenye shule za kata hali mbaya. Unakuta nusu ya wanafunzi wamefeli vibaya mno katika shule husika.

Mfano shule kama Kitunda hali ni mbaya, wanafunzi 249 wamepata division zero. Unajiuliza hii shule ina uongozi kweli? Afisa Elimu nae analipwa mshahara kabisa? Nini kifanyike wakuu?View attachment 3211475

View attachment 3211479

View attachment 3211481

View attachment 3211491

View attachment 3211492

Soma: NECTA yatangaza matokeo ya kidato cha nne 2024. Yatazame hapa!
Kwan afisa elimu ndo kafanya mitian? Na ndo mdau pekee wa elimu?? Bas kamuondoe 😍
 
Back
Top Bottom