Wale wenye dini zenu mtaashuhudia viongozi wenu wa dini au wengine mnawaita wa kiroho watakavyojazana kwenye uapisho wake kumuombea na kuwaaminisha kwamba yeye ni chaguo au mpango wa mango pamoja na yote tuliyoshuhudia kwa macho yetu na tuliyopitia kama nchi huku Ulimwengu mzima nao ukishuhudia maigizo yaliyoitwa uchaguzi ambao hata nayo hayakufanyika kabisa bali yaliishia kuharibika tu.
Nchi zote zimeona hakukua na uchaguzi wowote ,
SADC, EU, SA, wote hao walikuwa upande wa Wananchi, hata CCM wenyewe wameona hakuna kitu kama uchaguzi umefanyika, bado mtu anajitangaza ameshinda kwa kura M 32, kama sio ujuha ni nini, nina uhakika hata robo ya waliotakiwa kupiga kura hawakupiga, maana yake hawakutaki, unajua kabisa watu wamehudhulia kampeni zako kwa kulazimishwa kupanda malori kutoka maeneo mengine, lakini bado unalazimisha kuwa Rais,
Ni kwamba una matatizo ya akili au?
Hukuzaliwa uwe Rais, huna hekima na busara ya kiuongozi, bado unataka uwe Rais, ni nini hiki, ndugu zangu Watanganyika, kuna kitu Mungu ametuandalia au?
Najiuliza tu!!.
Sasa kinachofuatia ni nini, miaka minne yote tumeona uongozi ulivyokuwa, tutegemee nini, kwamba mambo yatakuwa tofauti, sasa wanaotakiwa kufa si wameongezeka idadi, maana kinachofuatia ni kulipa kisasi tu, kwa walioandama, tunafanyanye kuwalimda vijana wetu,
Hivi Mafwele anaendelea kuwapo, Mwiguku na matusi yake anaendelea kuwapo, Mchengelwa na kufokea Watanzania anaendelea kuwapo. Mungu tusaidie Watanzania