Pamoja na yote, Magufuli aachwe amalize vipindi vyake viwili vya Urais

Mkuu.. Ni kweli.. Busara za kawaida zinakataza kutafuta kinyozi mpya siku ya harusi yako hata kama unataka kunyoa upara.. Unashauriwa kumtumia kinyozi ambaye umemzoea na una uhakika atakunyoa vizuri ukapendeza siku ya harusi yako..
Nchi yetu ime invest nguvu nyingi kwa Magufuli.. Si busara nguvu hii tuliyo invest ikapotea.. Wacha tuendelee kuvuna kwa Magufuli ili nchi yetu ipate faida ya uwekezaji huu!
Kuna makubwa mengi ambayo Magufuli ameyaanzisha.. Busara inatutaka watanzania tumwongeze kipindi kingine aweze kuyakamilisha.
 
hoja ya kipumbavu, mwambie apambane awezavyo ila hatoboi mwaka huu!
 
Disillusioned na Mikakati ya Mzee.....Sijui anawaza nini? 10 years?

kama Mungu akipenda sababu jinsi katiba ya nchi inavyokanyangwa ili kufit nini anataka Kuanzia Bungeni hadi vyombo vya dola....Hashindwi kanyaga aendelee pengine

Lakini Historia itasema Haki itapatikana....Subira na Uvumilivu



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na ametuletea heshima kubwa sana nje ya nchi hakuna mfano

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo unaona kuongea kiingereza fasaha ndio maendeleo? Hizo ni colonial mindset. Hivi nchi zote ambazo raia wake wanaongea kiingereza zimeendelea kwa sababu tu wanaongea kiingereza? Au nchi ambazo hazizungumzi kiingereza hawana maendeleo?. Siyo lazima rais ajue kuongea kiingereza ndiyo alete maendeleo kama ndi hivyo basi nitawashauri hawa nao waongee kiingereza ili nchi zao zipate maendeleo kama uingereza: Putin, Angela Merkel, Xi Jinping, Emmanuel Macron, Shinzo Abe na wengine wengi.
 
Hiyo miradi haikuanza leo na itaendelea tu hata kama nchi haitakuwa na rais. Aondoke October 2020.
 
inawezekana kwa maslahi yako binafsi amekuudhi lakini angalia na upande wa pili miradi ya kitaifa inayotekelezwa katka hii awamu ya 5 ambayo hata wewe na familia yako mtanufaika nayo. TANZANIA FIRST MENGINE KILA MTU APAMBANE NA HALI YAKE TU.
Kama ikionekana tija haiwezi simama
Ila kumrudisha huyo ni kurudisha mateso kwa watz
 
Hata akipewa 20yrs Hakuna chance ya hio miradi kukamilika,
Kama miaka 5 sgr haijafika hata moro Ina maana kila mkoa to mkoa ni 5 yrs
 
Endeleeni kubweka mpaka 2025 na baada ya hapo mtamkumbuka.
 
Kwann tung'ang'anie soda iliyoisha nguvu Hali kwenye friji ziko nyingi
 
Ukisha pata umeme wa uhakika bei ya umeme itashuka na viwanda ni lazima vitaongezeka.
Hilo li la dhahiri.
Sasa thamani ya maisha utaikosaje?
Ule mradi mkubwa saana saana aisee usichukulie masihara na bado hawajaanza kuchimba hata bwawa moja bado wapo katika mataarisho mungu akitupa uhai na mradi huo ukiisha watanzania kiukweli watakua hatuna shida ya umeme

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa sasa nchi haina Rais...
Kama yupo mwambieni ajitokeze aendelee na ziara zake au arejea kwenye makazi rasmi ya Rais Ikulu!
 
Sitaki kukujibu kwa papara kwa haya uliyoweka hapa pamoja na kwamba mengi yake siyaafiki na hapo ndipo lilipo tatizo.
You sound a bit sincere, but then incredibly conflicted? How can this be?

Naomba unisome baadae ikiwezekana. Nitarudi kukujibu kwa utulivu zaidi.
 
Shida ya umeme iko pale pale...
Tena at the expanse of very serious environmental degradations!!
 
Kuna wakati Ronald Reagan , Rais wa Marekani aliwahi kusema “ read my lips”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…