Panya 100 Wafuzu, waenda Ughaibuni kufanya kazi

Dalton Elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
968
Reaction score
1,978
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amesema kupitia mradi wa kufundisha wanyama (APOPO) hususan Panyabuku wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo(SUA), panya 100 wamefundishwa na kufuzu na kupelekwa nchi mbalimbali.

Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 2025/26, Prof.Mkenda amesema panya hao wamepelekwa Angola (13), Azerbaijan (11), Cambodia (58) na Ethiopia sita (6) kwa ajili kutambua mabomu yaliyotegwa ardhini pamoja na utambuzi wa vimelea vya kifua kikuu.

Aidha, amesema panya 12 wamepelekwa nchini Marekani kama panya wa maonesho (mabalozi) kwenye shamba la wanyama.
“Utekelezaji wa mradi huo umeendelea kuijengea sifa na kuitangaza Tanzania Kimataifa ambapo panya wa Kitanzania ajulikanaye kwa jina la Ronin amevunja rekodi ya dunia kwa kutambua mabomu 109 yaliyotegwa ardhini nchini Cambodia akivunja rekodi ya panya wa Kitanzania Magawa ambaye alitambua mabomu 71 yaliyotengwa ardhini,”amesema.
 
Tunatakiwa kuachana na huu mradi. Sasa hivi mabomu yanarushwa mlipuaji akiwa kwao. Sasa sisi bado tunatafiti technology ya miaka ya 80. Tuangalie na kuvumbua panya wanao weza nusa kuwa bomu linakuja tujikinge na wanaoweza kugundua kama kuna tetemeko la ardhi watu wajiandae kujiokoa
 
Ndio maana wamepelekwa nje ya nchi ikiwemo US.
 
Kila la heri panya wetu,

Mkatuwakilishe vyema huko ughaibuni.

Mkirudi mje na zawadi.

Napenda kuiomba serikali yangu sikivu, ifuatilie kwa ukaribu mishahara yao, na kuhakikisha wanapata marupurupu yao , pindi wakistaafu viinua mgongo vyao wapate kwa wakati.
 
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amesema kupitia mradi wa kufundisha wanyama (APOPO) hususan Panyabuku wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo(SUA), panya 100 wamefundishwa na kufuzu na kupelekwa nchi mbalimbali.

Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 2025/26, Prof.Mkenda amesema panya hao wamepelekwa Angola (13), Azerbaijan (11), Cambodia (58) na Ethiopia sita (6) kwa ajili kutambua mabomu yaliyotegwa ardhini pamoja na utambuzi wa vimelea vya kifua kikuu.

Aidha, amesema panya 12 wamepelekwa nchini Marekani kama panya wa maonesho (mabalozi) kwenye shamba la wanyama.

Duuu, ona sasa wenzetu waliosoma wanavyokata mipaka ya nchi na mabara
 
Kwahiyo watu Kama watu imeshindikana kufuzu kwenda ughaibuni.
Mitano tena
 
Tunatakiwa kuachana na huu mradi. Sasa hivi mabomu yanarushwa mlipuaji akiwa kwao. Sasa sisi bado tunatafiti technology ya miaka ya 80. Tuangalie na kuvumbua panya wanao weza nusa kuwa bomu linakuja tujikinge na wanaoweza kugundua kama kuna tetemeko la ardhi watu wajiandae kujiokoa

Land mines bado ni tatizo la nchi nyingi duniani. Ukienda Angola, Msumbiji, Cambodia, nk bado watu wanafanywa vilema au kuuawa na mabomu hayo. Kuna maeneo kabisa yametengwa kama maeneo ya kifo, mtu haruhusiwi kwenda kwa sababu ya mabomu, licha ya kuwa ni maeneo ambayo yako location nzuri
 
Bora hata hao panya wasomi wenye akili waende kupeperusha bendera ya nchi huko ughaibuni kuliko wasomi wetu wanaokimbilia ccm na kuwa machawa

Mitano tena kwa mama, anaupiga mwingi
 
Tunatakiwa kuachana na huu mradi. Sasa hivi mabomu yanarushwa mlipuaji akiwa kwao. Sasa sisi bado tunatafiti technology ya miaka ya 80. Tuangalie na kuvumbua panya wanao weza nusa kuwa bomu linakuja tujikinge na wanaoweza kugundua kama kuna tetemeko la ardhi watu wajiandae kujiokoa
Mabomu yanayoteguliwa ni ya miaka mingi iliyopita, mabomu hayo bado yanaleta madhara kwa binaadamu mpaka sasa.
 
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amesema kupitia mradi wa kufundisha wanyama (APOPO) hususan Panyabuku wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo(SUA), panya 100 wamefundishwa na kufuzu na kupelekwa nchi mbalimbali.

Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 2025/26, Prof.Mkenda amesema panya hao wamepelekwa Angola (13), Azerbaijan (11), Cambodia (58) na Ethiopia sita (6) kwa ajili kutambua mabomu yaliyotegwa ardhini pamoja na utambuzi wa vimelea vya kifua kikuu.

Aidha, amesema panya 12 wamepelekwa nchini Marekani kama panya wa maonesho (mabalozi) kwenye shamba la wanyama.
Kumbe panya wana akili na manufaa kuliko chawa!!!
 
Back
Top Bottom