Tresor Mandala
JF-Expert Member
- Aug 20, 2010
- 47,397
- 101,204
Kusoma raha sana,
Kusoma kuzuriKumbe panya wana akili na manufaa kuliko chawa!!!
Wakufunzi wa hao panya ni watanzania ..😂😂😂
Panya wa mamaPanya wa Tanzania, wana akili na vipaji kuliko Watanzania 😆
Maana kutoka Tanzania wanaopata fursa za kwenda mataifa ya nje kufanya kazi ni Panya
Kama panya buku kila wakihitimu wanalamba ajira fasta namna hiyo-tena nje ya nchi- naishauri SUA iachane na biashara kichaa ya kufyatua graduate ambao hawaajiriki.Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amesema kupitia mradi wa kufundisha wanyama (APOPO) hususan Panyabuku wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo(SUA), panya 100 wamefundishwa na kufuzu na kupelekwa nchi mbalimbali.
Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 2025/26, Prof.Mkenda amesema panya hao wamepelekwa Angola (13), Azerbaijan (11), Cambodia (58) na Ethiopia sita (6) kwa ajili kutambua mabomu yaliyotegwa ardhini pamoja na utambuzi wa vimelea vya kifua kikuu.
Aidha, amesema panya 12 wamepelekwa nchini Marekani kama panya wa maonesho (mabalozi) kwenye shamba la wanyama.
Hao Kustaafu Hadi KifoKila la heri panya wetu,
Mkatuwakilishe vyema huko ughaibuni.
Mkirudi mje na zawadi.
Napenda kuiomba serikali yangu sikivu, ifuatilie kwa ukaribu mishahara yao, na kuhakikisha wanapata marupurupu yao , pindi wakistaafu viinua mgongo vyao wapate kwa wakati.