Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 15,835
- 23,776
Watoto walio zaliwa jana waitwe MAGAWA.Panya wa Tanzania mwenye sifa ya kufichua mabomu kimataifa astaafu Cambodia Magawa (panya) aliyejishindia tuzo kwa ushujaa wake anastaafu katika kazi yake ya kufichua mabomu yaliotegwa ardhini.
Kila ugunduzi alioufanya ulipunguza hatari ya kuumia au kifo kwa watu wa Kambodia. Katika kazi ya miaka mitano aliyofanya Hadi leo Magawa amefanikiwa kugundua mabomu 71 yaliotegwa ardhini pamoja na vilipuzi kadhaa nchini Cambodia na kumfanya kuwa HeroRAT aliyefanikiwa zaidi wa APOPO
Wasimamizi wake wanasema kwamba panya huyo mwenye umri wa miaka saba ameanza kupunguza kasi yake akielekea kuwa mzee na anahitaji kuheshimu mahitaji yake
Magawa ni panya mkubwa wa kijeshi wa kiafrika aliyezaliwa nchini Tanzania mnamo Novemba 2014. Alikulia katika kituo cha Mafunzo na Utafiti cha APOPO nchini Tanzania ambapo alijifunza jinsi ya kupata vilipuzi kwa kutumia hisia zake za ajabu za kunusa. Magawa kisha alihamia Siem Reap huko Cambodia mnamo 2016, ambapo alianza kazi yake yenye mafanikio.
View attachment 1808755
PILI, serikali impe BENZI LAKE na kumjengea nyumba.