Panya Magawa astaafu kazi ya kufichua mabomu kimataifa

Panya Magawa astaafu kazi ya kufichua mabomu kimataifa

#UNAAMBIWA: Panya wa kiume kutoka Tanzania, Magawa ambaye mwaka jana alitunukiwa nishani ya dhahabu kutokana na uwezo wake wa kubaini mabomu ya kutegwa ardhini Cambodia, anastaafu Mwezi huu.

Magawa alizaliwa Tanzania Nov 5,2014 akiwa na uzani wa KG 1.2 na urefu wa Sentimita 70, alipewa mafunzo na Shirika lisilo la Kiserikali la Apopo kutoka Ubelgiji lenye Makao yake Morogoro Tanzania na alipewa nishani ya dhahabu kutokana na uwezo wake wa kubaini mabomu ya kutegwa ardhini.

Wasimamizi wake wanasema Magawa mwenye umri wa miaka saba kwa sasa ameanza kupunguza kasi yake ya kutegua mabomu kwakuwa amezeeka na ni wakati wake wa kupumzika.

Shirika la Matibabu ya Wanyama la Uingereza lisilokuwa la kiserikali PDSA lilimtunza medali ya dhahabu kwa kujitolea kwake kuokoa maisha kupitia kazi yake ya kubaini mabomu hatari yaliyotegwa ardhini Cambodia, inadhaniwa huenda kuna hadi mabomu Milioni sita ya kutegwa ardhini katika Nchi hiyo ya kusini mashariki mwa bara Asia.

Screenshot_20210605_193558.jpg
 
Hahahahah...!apunguze misongamano...naskia panya wanpenda misongamano
Ishu kwake ni mapori
Kajenga eneo ambalo halijajengwa sana so unakuta kuna viwanja vya wengine mpaka waje kuvisafisha ni miezi.ndani ya Yale machaka mazitomazito ndo nyumba za panya.
Mapanya ni manene makubwa,kama ni mmakonde hukosi mboga
 
Haya maisha nyie.....panya anamiliki dhahabu mie binadamu sina 😂😂
 
Wasisahau kumjengea hekalu kama wengine.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]aaahhhh this is JF

Mwanangu umenichekesha sanaaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Jf iwe pahala pa kurefresh na kufurah daima
 
Panya wa Tanzania mwenye sifa ya kufichua mabomu kimataifa astaafu Cambodia Magawa (panya) aliyejishindia tuzo kwa ushujaa wake anastaafu katika kazi yake ya kufichua mabomu yaliotegwa ardhini.

Kila ugunduzi alioufanya ulipunguza hatari ya kuumia au kifo kwa watu wa Kambodia. Katika kazi ya miaka mitano aliyofanya Hadi leo Magawa amefanikiwa kugundua mabomu 71 yaliotegwa ardhini pamoja na vilipuzi kadhaa nchini Cambodia na kumfanya kuwa HeroRAT aliyefanikiwa zaidi wa APOPO

Wasimamizi wake wanasema kwamba panya huyo mwenye umri wa miaka saba ameanza kupunguza kasi yake akielekea kuwa mzee na anahitaji kuheshimu mahitaji yake

Magawa ni panya mkubwa wa kijeshi wa kiafrika aliyezaliwa nchini Tanzania mnamo Novemba 2014. Alikulia katika kituo cha Mafunzo na Utafiti cha APOPO nchini Tanzania ambapo alijifunza jinsi ya kupata vilipuzi kwa kutumia hisia zake za ajabu za kunusa. Magawa kisha alihamia Siem Reap huko Cambodia mnamo 2016, ambapo alianza kazi yake yenye mafanikio.

View attachment 1808755
Kama ana akili hizo pesa zake akanunue uwanja huko mbweni ajenge aanzishe familia yake aachane na tabia ya kwenda kukaa kwenye madari ya nyumba za watu.
 
We jamaa boya sana,nimekaa na sista du siti moja najiandaa kupiga swaga ghafla nasoma comment yako nkajikuta nacheka kiboya nimepoteza points zote nkaonekana mshamba kisenge.
Bora hujatongoza mkuu...ila tuseme ukwel...masuala ya kuumwa na panya ujue huna net,unalala na masalia ya msos,unalala room 1 na mavyombo na manguo! Yaan room yako ni chafu balaa...
Mm huo nauterm kama umaskini wa level ya mwisho kbs
 
Na mm mbwa wangu aitwae CHUKI ameanza kupunguza kubweka toka January ameifanya Kaz yake kwa muda wa miaka Kumi bila kuchoka

Bahat mbaya sina cha kumpa Zaid ya ugal nao mpa kila siku

HONGERA KWA MAGAWA

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom