Panya Magawa astaafu kazi ya kufichua mabomu kimataifa

Panya Magawa astaafu kazi ya kufichua mabomu kimataifa

Kwa hiyo panya inalipwa mafao ? halafu kuna vijana hawana ajira toka wamemaliza chuo...si muwape hao vijana hata fursa za kutegua mabomu🐀💣
 
Wanasheria
Msaada tafadhali maana ndugu yetu magawa tunayetoka ukoo mmoja.
Kwa kazi aliyofanya mataifa mbalimbali ya kutegua mabomu tunaomba msaada wa kisheria ili mafao yake tuweze kuyapata.
Ni ndugu yetu kabisa tena tunatoka ukoo mmoja msaada tafadhali.
 
Ukiona unaumwa na panya jua uko level ya mwisho ya umaskini mkuu!
Huwajui panya mkuu, waulize Australia mwaka huu kilichowakuta.
Hawabagui, New York yenyewe ina panya.
Tuulize wakulima Kilosa, Ifakara, Lushoto, Kilindi, kuna miaka tunapatwa na janga la panya.
Hata mwaka huu nafikiri watakuwepo, maana mvua zilikuwa chache.

Namuheshimu panya aweza kukutia umaskini in seconds.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Panya wa Tanzania mwenye sifa ya kufichua mabomu kimataifa astaafu Cambodia Magawa (panya) aliyejishindia tuzo kwa ushujaa wake anastaafu katika kazi yake ya kufichua mabomu yaliotegwa ardhini.

Kila ugunduzi alioufanya ulipunguza hatari ya kuumia au kifo kwa watu wa Kambodia. Katika kazi ya miaka mitano aliyofanya Hadi leo Magawa amefanikiwa kugundua mabomu 71 yaliotegwa ardhini pamoja na vilipuzi kadhaa nchini Cambodia na kumfanya kuwa HeroRAT aliyefanikiwa zaidi wa APOPO

Wasimamizi wake wanasema kwamba panya huyo mwenye umri wa miaka saba ameanza kupunguza kasi yake akielekea kuwa mzee na anahitaji kuheshimu mahitaji yake

Magawa ni panya mkubwa wa kijeshi wa kiafrika aliyezaliwa nchini Tanzania mnamo Novemba 2014. Alikulia katika kituo cha Mafunzo na Utafiti cha APOPO nchini Tanzania ambapo alijifunza jinsi ya kupata vilipuzi kwa kutumia hisia zake za ajabu za kunusa. Magawa kisha alihamia Siem Reap huko Cambodia mnamo 2016, ambapo alianza kazi yake yenye mafanikio.

View attachment 1808755
Bila Shaka Huyu Magawa panya asili yake Dodoma .
 
Panya anajulikana na ana boardguard ila hata hajulikani
 
Huwajui panya mkuu, waulize Australia mwaka huu kilichowakuta.
Hawabagui, New York yenyewe ina panya.
Tuulize wakulima Kilosa, Ifakara, Lushoto, Kilindi, kuna miaka tunapatwa na janga la panya.
Hata mwaka huu nafikiri watakuwepo, maana mvua zilikuwa chache.

Namuheshimu panya aweza kukutia umaskini in seconds.

Everyday is Saturday............................... 😎
Wakulima wanawafata hom? Kwetu ifakara sijakutana na panya aisee!
 
Back
Top Bottom