Panya Magawa astaafu kazi ya kufichua mabomu kimataifa

Watoto walio zaliwa jana waitwe MAGAWA.

PILI, serikali impe BENZI LAKE na kumjengea nyumba.
 
Nianze kwa kupongeza juhudi za SUA mpaka walipofikia na mradi huu wa Panya.

Kwani mpaka sasa wanaweza kutambua vimelea wa TB, kutegua mabomu ya aridhini n.k.

Pamoja na hayo ningetamani kusikia Panya hawa hata wameanza na shughuli nyingine tofauti tofauti.

Kwa mfano wangewezeshwa waweze kukusanya taka za plastiki, hasa hivi vya nailoni.

Ifike mahali kila Kata nchini iwe inakodisha idadi kadhaa ya Panya kwa mwezi au mwaka kwa ajili ya shughuli hizo.
 
SUA na tafiti za haja na uhakika. UDSM na tafiti za robot la mabati
 
Fahamu Panya Mtanzania Magawa ambaye amestaafu kazi ya kutegua mabomu baada ya kufanya kazi hiyo mataifa mbalimbali kwa weledi mkubwa ambapo mpaka anastaafu ametegua mabomu zaidi 109.

Magawa ameshinda medali ya dhahabu kwa uwezo wake wa kazi. inaelezwa kuwa kwa sasa ataendelea kusalia Cambodia baada ya kustaafu kutokana na kuhofia afya yake wakati wakusafiri. Lakini chumba chake na sebule kikiwa na CCTV- Camera pamoja na feni kipo.

Jina la panya magawa ambalo ni jina la rafiki yake babake Pendo Msegu (Mkufunzi) likimaanisha Mtoaji, amestaafu akiwa na umri wa miaka 7. Mkufunzi Pendo anaeleza kuwa Magawa alikuwa wa kiume lakini hakuwa kwenye mahusiano (alikuwa single) , licha ya kuwa single hakuwa na mtoto pia . Lakini anawadogo zake ambao pia wanaendelea na mafunzo hadi sasa.

[emoji232][emoji232][emoji242][emoji242][emoji242][emoji242]

 
Magawa katutoka,asante kwa utumishi uliotukuka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…