Bushmaster
JF-Expert Member
- Jan 18, 2022
- 583
- 1,265
Hao panya road nawatafuta sana,walimpiga dogo panga la usoni,ukiwaona tena popote pale nishtue nije nipige hata jiwe
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona wanaokula kodi zetu huwaambii kuwa hawako juu ya sheriaHii nchi ina mfumo wa sheria na hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria, leo hii wamemuua kijana wa watu inakuwaje kesho wakamuua mtu mwingine ambaye anashukiwa tu kuwa ni mwizi. Serikali,
Hilo nalo jizi tu unafikaje hapa eti umeguswa na kifo cha panya road na mbaya zaidi kaja na uthibitisho kuwa alikwapua sasa sijui alitaka wamfanye nini?RC mwenyewe katangaza kuwa wakutwe au wakatafutwe Mwaisela kama mna shida naoUnapoandika suala zito kama hili la panya road, usiegemee upande wowote, kuwa huru, jiweke kati kati.
Vinginevyo nawe utaonekana ni panya road tu ama mnufaika.
Kuna binti kauawa mitaa ya Dar na hao panya road na mpaka muda huu kuna taharuki kubwa sana kitaifa na msiba mkubwa familia ikiomboleza na kusaga meno!
Sasa sijasikia popote ukianza kwanza kulaani kuuawa kwa huyo raia mwema asiye na hatia ama kutoa pole kwa familia iliyouliwa familia yao na hao vibaka.
Unamtetea panya road mwenzio sio !! Wao wakijeruhi, wakiua, wakipora ni Sawa ?! Wauawe tuu hawana faida katika nchi hii. Povu ruksa [emoji1787][emoji1787][emoji1787]Habari za Jioni,
Kuna jambo la kusikitisha sana ambalo limenifanya niwaze sana mda huu. Jioni hii saa moja kuna kijana ambaye ni panya road amechomwa moto barabara ya kutokea sweet corner kuelekea Manzese darajani (karibu na machine za kusaga). Kijana huyo ambaye alimpora mtu kwa kutumia silaha amepigwa na kuchomwa moto.
Kilichonisikitisha ni kuwa sikutegemea kama kuna watu wenye hulka za kuchukua sheria mkononi. Hii nchi ina mfumo wa sheria na hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria, leo hii wamemuua kijana wa watu inakuwaje kesho wakamuua mtu mwingine ambaye anashukiwa tu kuwa ni mwizi. Serikali, wadau wa haki za binadamu na jeshi la polisi linatakiwa liangalie hili swala kwa jicho la tatu.
Nakumbuka kuna kijana nilisoma nae form two alikiwa anaitwa James Nyoni, huyu kijana alikuwa anapenda maisha mazuri tu ya kujionyesha onyesha. Nakumbuka alichukua pamba za mtu gheto akazitinga jamaa mwenye pamba zake akakutana nae mitaa ya Ubungo.
Ilikuwa mwaka 2010, yule mwenye pamba akamwitia rafiki yake mwizi na watu walimpiga na kumchoma James Nyoni moto. Hili ni moja ya tukio ambalo liliniachia simanzi kubwa sana kwa sababu ya nguo jamaa akachomwa moto.
I am very sad about this. We are not savages we are real people and we should be civilized. People should not take the law at their own hands, and tonight I believe Panya Road will retaliate. My house is in the street of Manzese no one will be safe, begging the Police and the street watchmen to guard the innocent people and their families.
We endelea kukaba tu siku zako zinahesabikaPunguza ujinga ndugu.haki za binadamu zinahusu wale wenye dhamana na mamlaka yakulinda usalama wa binadamu.sasa panya road ana mamlaka gani.inasemwa hivyo ili kusiwe na matumizi mabaya ya mamlaka kwasababu mamlaka ikiamua inaweza kuswaga wananchi wote kama mbuzi na msihoji chochote.vibaka wakifanya uhuni kuna vyombo vyenye mamlaka vyakuwachukulia hatua je siku ikitokea mamlaka ndio iliyovunja sheria ni nani wakuiwajibisha?.Ndo maana wenye akili wanaweka hizo haki na maangalizo.
Kampe mke wako hadithi za kijinga hiziSio mazingira yote yanaweza kua hivyo.Kuna kijiji kibaka aliiba gunia la maindi akakimbizwa ilikua usiku akaingia kwenye nyumba ya mtu akajificha mwenye nyumba akahisi kuna mtu kaingia wakati anajipanga kuangalia ni nini wanakijiji wakafika wakidai mwizi wao mzee wawatu kutoka ili awaambie sio yeye na mwizi yuko ndani kajificha wakampiga mapanga.mambo mengine tusiyachukulie kirahisi kwakua halijakukuta.
Ile story ya yule jamaa ilisikitisha sana.. yule dada ana ticket ya motoni kabisa kwa alichokifanyaIlitokea SAUT Mwanza mtu kagombana na demu wake alivyoenda kumtembelea hostel yule demu akamuitia mwizi. Wakampiga mpaka anakata roho ndio sauti za jamani msimpige sio mwizi zinasikika kutoka kwa huyo mdada
Mzee kna sehemu inaitwa msisiriWatu wa Manzese wana sifa na uthubutu kama watu wa Rchuga bravo bravo.
Choma vibaka wote.
Na sahvi wanawambia betting,kamari ni ajira wacheze tuTumegeukia uchuuzi Kama suluhisho la kudumu la kuukosekana ajira...
.bora kupanua fursa kwenye kilimo, ufugaji au uvuvi maana kuna mahitaji ya hizo bidhaa kila siku huko duniani.
KUCHUKUA SHERIA MKONONI HAIJAANZA LEO WALA JANABad very bad
Kuna mwamba aliweka uzi hapa kuwa alimkopesha demu elfu 50, kwenda kudai yule demu akamwitia mwizi. Jamaa alikimbia kuokoa maisha yake, inakuwaje kama watu wangejichukulia sheria mkononi. Angeweza poteza maisha na hakuwa na hatia. WE HAVE TO OBSERVE RULE OF LAW, WE ARE NOT ANIMALS. .
Atakuwa alionekana kuwa na macho juu juu
Inshu sio panya road, wala nani, bali ninachokizungumzia ni kujichukulia sheria mkononi, ndio maana nikasema kama kuna uthibitisho wa alichokiiba sawa, lakini haya ya kusema tu huyo mwizi, ni hatari sana kwenye jamii, ni wangapi wameuawa kwa kuitiwa wezi kumbe jamaa ana ugomvi na demu wake, akaamua kuitiwa mwizi na akauawa, tukio kama hili lilitokea ubungo mwaka juzi!!jamaa amekwenda kwa demu wake, akamkuta yupo na jamaa ndani, ikatokea fujo demu akamuitia mwizi, wana nzego wakamuua jamaa, badaye inakuja kujulikana mbona ni mpenzi wake!!hadi leo demu yuko ndani!!!japo mifumo yetu ya sheria ina matatizo lakini kujichukulia sheria mkononi ni hatari sana!!ndio maana hiyo huwezi kuikuta kwenye jamii ya watu walioendeleaDuuuh kumbe watetezi wa panyaroad mpo wengi hivi?
Yaan wewe watu kupingwa mapanga na kuuliwa na hao panyaroad unaona ni sawa tu kwako ila panyaroad wakishugurikiwa unaanza kupaza sauti? Tutawanyoosha na nyinyi watetezi wao endeleeni tu
Sawa mkuu umeeleweka...Inshu sio panya road, wala nani, bali ninachokizungumzia ni kujichukulia sheria mkononi, ndio maana nikasema kama kuna uthibitisho wa alichokiiba sawa, lakini haya ya kusema tu huyo mwizi, ni hatari sana kwenye jamii, ni wangapi wameuawa kwa kuitiwa wezi kumbe jamaa ana ugomvi na demu wake, akaamua kuitiwa mwizi na akauawa, tukio kama hili lilitokea ubungo mwaka juzi!!jamaa amekwenda kwa demu wake, akamkuta yupo na jamaa ndani, ikatokea fujo demu akamuitia mwizi, wana nzego wakamuua jamaa, badaye inakuja kujulikana mbona ni mpenzi wake!!hadi leo demu yuko ndani!!!japo mifumo yetu ya sheria ina matatizo lakini kujichukulia sheria mkononi ni hatari sana!!ndio maana hiyo huwezi kuikuta kwenye jamii ya watu walioendelea