Panya Road achomwa moto Manzese

Panya Road achomwa moto Manzese

Hao panya road nawatafuta sana,walimpiga dogo panga la usoni,ukiwaona tena popote pale nishtue nije nipige hata jiwe
 
Mtoa mada unaumia kwa kuwa aliyeuawa ni classmate wako. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787]
 
Hii nchi ina mfumo wa sheria na hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria, leo hii wamemuua kijana wa watu inakuwaje kesho wakamuua mtu mwingine ambaye anashukiwa tu kuwa ni mwizi. Serikali,
Mbona wanaokula kodi zetu huwaambii kuwa hawako juu ya sheria
 
Unapoandika suala zito kama hili la panya road, usiegemee upande wowote, kuwa huru, jiweke kati kati.

Vinginevyo nawe utaonekana ni panya road tu ama mnufaika.

Kuna binti kauawa mitaa ya Dar na hao panya road na mpaka muda huu kuna taharuki kubwa sana kitaifa na msiba mkubwa familia ikiomboleza na kusaga meno!

Sasa sijasikia popote ukianza kwanza kulaani kuuawa kwa huyo raia mwema asiye na hatia ama kutoa pole kwa familia iliyouliwa familia yao na hao vibaka.
Hilo nalo jizi tu unafikaje hapa eti umeguswa na kifo cha panya road na mbaya zaidi kaja na uthibitisho kuwa alikwapua sasa sijui alitaka wamfanye nini?RC mwenyewe katangaza kuwa wakutwe au wakatafutwe Mwaisela kama mna shida nao

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Habari za Jioni,

Kuna jambo la kusikitisha sana ambalo limenifanya niwaze sana mda huu. Jioni hii saa moja kuna kijana ambaye ni panya road amechomwa moto barabara ya kutokea sweet corner kuelekea Manzese darajani (karibu na machine za kusaga). Kijana huyo ambaye alimpora mtu kwa kutumia silaha amepigwa na kuchomwa moto.

Kilichonisikitisha ni kuwa sikutegemea kama kuna watu wenye hulka za kuchukua sheria mkononi. Hii nchi ina mfumo wa sheria na hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria, leo hii wamemuua kijana wa watu inakuwaje kesho wakamuua mtu mwingine ambaye anashukiwa tu kuwa ni mwizi. Serikali, wadau wa haki za binadamu na jeshi la polisi linatakiwa liangalie hili swala kwa jicho la tatu.

Nakumbuka kuna kijana nilisoma nae form two alikiwa anaitwa James Nyoni, huyu kijana alikuwa anapenda maisha mazuri tu ya kujionyesha onyesha. Nakumbuka alichukua pamba za mtu gheto akazitinga jamaa mwenye pamba zake akakutana nae mitaa ya Ubungo.

Ilikuwa mwaka 2010, yule mwenye pamba akamwitia rafiki yake mwizi na watu walimpiga na kumchoma James Nyoni moto. Hili ni moja ya tukio ambalo liliniachia simanzi kubwa sana kwa sababu ya nguo jamaa akachomwa moto.

I am very sad about this. We are not savages we are real people and we should be civilized. People should not take the law at their own hands, and tonight I believe Panya Road will retaliate. My house is in the street of Manzese no one will be safe, begging the Police and the street watchmen to guard the innocent people and their families.
Unamtetea panya road mwenzio sio !! Wao wakijeruhi, wakiua, wakipora ni Sawa ?! Wauawe tuu hawana faida katika nchi hii. Povu ruksa [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Punguza ujinga ndugu.haki za binadamu zinahusu wale wenye dhamana na mamlaka yakulinda usalama wa binadamu.sasa panya road ana mamlaka gani.inasemwa hivyo ili kusiwe na matumizi mabaya ya mamlaka kwasababu mamlaka ikiamua inaweza kuswaga wananchi wote kama mbuzi na msihoji chochote.vibaka wakifanya uhuni kuna vyombo vyenye mamlaka vyakuwachukulia hatua je siku ikitokea mamlaka ndio iliyovunja sheria ni nani wakuiwajibisha?.Ndo maana wenye akili wanaweka hizo haki na maangalizo.
We endelea kukaba tu siku zako zinahesabika
 
Sio mazingira yote yanaweza kua hivyo.Kuna kijiji kibaka aliiba gunia la maindi akakimbizwa ilikua usiku akaingia kwenye nyumba ya mtu akajificha mwenye nyumba akahisi kuna mtu kaingia wakati anajipanga kuangalia ni nini wanakijiji wakafika wakidai mwizi wao mzee wawatu kutoka ili awaambie sio yeye na mwizi yuko ndani kajificha wakampiga mapanga.mambo mengine tusiyachukulie kirahisi kwakua halijakukuta.
Kampe mke wako hadithi za kijinga hizi
 
Kiubinadamu upo sawa, ila mkuu ushawahi kuingia anga za vibaka, wezi au panya road? Sali sana yasije kukukuta wewe au mpendwa wako. Au nenda kwa yule mzee aliyeuliwa binti yake umwambie hizi habari ulizoandika hapa
 
Ilitokea SAUT Mwanza mtu kagombana na demu wake alivyoenda kumtembelea hostel yule demu akamuitia mwizi. Wakampiga mpaka anakata roho ndio sauti za jamani msimpige sio mwizi zinasikika kutoka kwa huyo mdada
Ile story ya yule jamaa ilisikitisha sana.. yule dada ana ticket ya motoni kabisa kwa alichokifanya
 
Tumegeukia uchuuzi Kama suluhisho la kudumu la kuukosekana ajira...

.bora kupanua fursa kwenye kilimo, ufugaji au uvuvi maana kuna mahitaji ya hizo bidhaa kila siku huko duniani.
Na sahvi wanawambia betting,kamari ni ajira wacheze tu

Ova
 
Bad very bad
Kuna mwamba aliweka uzi hapa kuwa alimkopesha demu elfu 50, kwenda kudai yule demu akamwitia mwizi. Jamaa alikimbia kuokoa maisha yake, inakuwaje kama watu wangejichukulia sheria mkononi. Angeweza poteza maisha na hakuwa na hatia. WE HAVE TO OBSERVE RULE OF LAW, WE ARE NOT ANIMALS. .
KUCHUKUA SHERIA MKONONI HAIJAANZA LEO WALA JANA
KUNA WATU AMBAO NI WATUKUTU NA WATU WA MATUKIO KUNA WAKATI INAFIKA JAMII INAWACHOKA,SERIKALI INAWACHOKA...SOLUTION YAO NI MOJA KUWAONDOA DUNIANI
HAYA MATUKIO YA KUWAONDOA YANAFANYIKAGA SANA,SIKU RAIA WAKIAMUA NA KWA TAARIFA YAKO RAIA HAWAAMUI TU WAO,KUNA BARAKA WANAPEWA TOKA JUU

KUNA WAKATI FULANI KUNA WAKABAJI AMBAO WALIKUWA WANASUMBUA SANA SEHEMU ZA KINONDONI,NAKUMBUKA WALIPEWA
ONYO SANA MPAKA KWA WAZAZ WAO WAWAKANYE WATOTO ZAO WAACHE...LAKN MWISHONI WATOTO
WALE WALIKUWA WANAJIFANYA MANUNDA HAWASIKI
KUNA TEAM ILIPITA MAKWAO NA KUWACHKUA MKONONI MWA WAZAZ WAO WENGINE WAKIWA MAGHETONI MWAO
WALIPELEKWA BIAFRA UWANJANI PEMBENI,WALIPIGWA NA KUMALIZWA WOTE HAPO HAPO

OVA
 
Mkuu ujasikia walichofnaya hao panya road cku mbili hizi mpaka kukuuwa mwanafunzi wa chuo

Sasa kufa uwo panya road mmoja unalalamika kweli bob!! Hawo panya wapigwe mpaka wakufee
 
Hawa panya wameleta taharuki katika jamii. Wanatakiwa kushughulikiwa kisawasawa. Hawafai na hawakiwi kuonewa huruma hata kidogo.Bila hivo wataendelea kuiumiza jamii mzima. Wananchi inabidi waungane kuwatokomeza. Hali sio shwari mitaani Dar. Hawawezi kuachwa wajitawale na kuumiza watu. Hawafai kabisa hawa jamaa.
 
Duuuh kumbe watetezi wa panyaroad mpo wengi hivi?

Yaan wewe watu kupingwa mapanga na kuuliwa na hao panyaroad unaona ni sawa tu kwako ila panyaroad wakishugurikiwa unaanza kupaza sauti? Tutawanyoosha na nyinyi watetezi wao endeleeni tu
Inshu sio panya road, wala nani, bali ninachokizungumzia ni kujichukulia sheria mkononi, ndio maana nikasema kama kuna uthibitisho wa alichokiiba sawa, lakini haya ya kusema tu huyo mwizi, ni hatari sana kwenye jamii, ni wangapi wameuawa kwa kuitiwa wezi kumbe jamaa ana ugomvi na demu wake, akaamua kuitiwa mwizi na akauawa, tukio kama hili lilitokea ubungo mwaka juzi!!jamaa amekwenda kwa demu wake, akamkuta yupo na jamaa ndani, ikatokea fujo demu akamuitia mwizi, wana nzego wakamuua jamaa, badaye inakuja kujulikana mbona ni mpenzi wake!!hadi leo demu yuko ndani!!!japo mifumo yetu ya sheria ina matatizo lakini kujichukulia sheria mkononi ni hatari sana!!ndio maana hiyo huwezi kuikuta kwenye jamii ya watu walioendelea
 
Inshu sio panya road, wala nani, bali ninachokizungumzia ni kujichukulia sheria mkononi, ndio maana nikasema kama kuna uthibitisho wa alichokiiba sawa, lakini haya ya kusema tu huyo mwizi, ni hatari sana kwenye jamii, ni wangapi wameuawa kwa kuitiwa wezi kumbe jamaa ana ugomvi na demu wake, akaamua kuitiwa mwizi na akauawa, tukio kama hili lilitokea ubungo mwaka juzi!!jamaa amekwenda kwa demu wake, akamkuta yupo na jamaa ndani, ikatokea fujo demu akamuitia mwizi, wana nzego wakamuua jamaa, badaye inakuja kujulikana mbona ni mpenzi wake!!hadi leo demu yuko ndani!!!japo mifumo yetu ya sheria ina matatizo lakini kujichukulia sheria mkononi ni hatari sana!!ndio maana hiyo huwezi kuikuta kwenye jamii ya watu walioendelea
Sawa mkuu umeeleweka...
 
Watu wa Dar wacharuka! Wazima Panya Road Mmoja. Je Panya Road Wengine Watasitisha Uhalifu? (Natamani kichwa cha thread kingekuwa hivyo)
 
Katika hili la panya road watakufa wengi watafungwa wengi vila hatia. Hii ni vita siku zote vita haina macho
 
Back
Top Bottom