Habari za Jioni
Kuna jambo la kusikitisha sana ambalo limenifanya niwaze sana mda huu. Jioni hii saa moja kuna kijana ambaye ni panya road amechomwa moto barabara ya kutokea sweet corner kuelekea Manzese darajani (karibu na machine za kusaga). Kijana huyo ambaye alimpora mtu kwa kutumia silaha amepigwa na kuchomwa moto. .
Kilichonisikitisha ni kuwa sikutegemea kama kuna watu wenye hulka za kuchukua sheria mkononi. Hii nchi ina mfumo wa sheria na hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria, leoo hii wamemuua kijana wa watu inakuwaje kesho wakamuua mtu mwingine ambaye anashukiwa tu kuwa ni mwizi. Serikali, wadau wa haki za binadamu na jeshi la polisi linatakiwa liangalie hili swala kwa jicho la tatu. .
Nakumbuka kuna kijana nilisoma nae form two alikiwa anaitwa James Nyoni, huyu kijana alikuwa anapenda maisha mazuri tu ya kujionyesha onyesha. Nakumbuka alichukua pamba za mtu gheto akazitinga jamaa mwenye pamba zake akakutana nae mitaa ya Ubungo. Ilikuwa mwaka 2010, yule mwenye pamba akamwitia rafiki yake mwizi na watu walimpiga na kumchoma James Nyoni moto. Hili ni moja ya tukio ambalo liliniachia simanzi kubwa sana kwa sababu ya nguo jamaa akachomwa moto. .
Am very sad about this. We are not savages we are really people and we should be civilized. People should take law at their own hands, and tonight I believe Panya Roads will retaliate. My house being in street of Manzese no one will be safe, begging the Police and the street watchmen to guard the innocent people and their families. .