Panya Road achomwa moto Manzese

Panya Road achomwa moto Manzese

Mtu ambaye bado anafikiria kuua mwenzake kwa visababu vidogo vidogo ni Hayawani tu huyo.

Kumwua mtu kwa kumhisi hakumtofautishi mwuaji na panya road halisi ambao tungependa sote kuwapiga vita.

Tuwapige vita panya road kwa mujibu wa sheria.
 
Habari za Jioni
Kuna jambo la kusikitisha sana ambalo limenifanya niwaze sana mda huu. Jioni hii saa moja kuna kijana ambaye ni panya road amechomwa moto barabara ya kutokea sweet corner kuelekea Manzese darajani (karibu na machine za kusaga). Kijana huyo ambaye alimpora mtu kwa kutumia silaha amepigwa na kuchomwa moto. .

Kilichonisikitisha ni kuwa sikutegemea kama kuna watu wenye hulka za kuchukua sheria mkononi. Hii nchi ina mfumo wa sheria na hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria, leoo hii wamemuua kijana wa watu inakuwaje kesho wakamuua mtu mwingine ambaye anashukiwa tu kuwa ni mwizi. Serikali, wadau wa haki za binadamu na jeshi la polisi linatakiwa liangalie hili swala kwa jicho la tatu. .

Nakumbuka kuna kijana nilisoma nae form two alikiwa anaitwa James Nyoni, huyu kijana alikuwa anapenda maisha mazuri tu ya kujionyesha onyesha. Nakumbuka alichukua pamba za mtu gheto akazitinga jamaa mwenye pamba zake akakutana nae mitaa ya Ubungo. Ilikuwa mwaka 2010, yule mwenye pamba akamwitia rafiki yake mwizi na watu walimpiga na kumchoma James Nyoni moto. Hili ni moja ya tukio ambalo liliniachia simanzi kubwa sana kwa sababu ya nguo jamaa akachomwa moto. .

Am very sad about this. We are not savages we are really people and we should be civilized. People should take law at their own hands, and tonight I believe Panya Roads will retaliate. My house being in street of Manzese no one will be safe, begging the Police and the street watchmen to guard the innocent people and their families. .
Watachomwa moto sana na hata wewe unastahili kuchomwa moto sio huu TU mpaka wa Jehanam mana ni Mnafiki .
Wanafiki ni watu hatari kuliko panya road.

Mwanyekiti Mungu alishusha mpaka Aya ya wanafiki ili kuwaonya.

Wale wanaojiita Watu wa Haki za Binadamu nao pia Wana unafiki.

Polisi wakikamata watu mnlia Lia . Wakiwaacha mnalialia .
Watu wameamua kupambana wenyewe na Wahalifu mnalialia mnataka Nini? Jamii ndiyo inayowafahamu Wahalifu. Mkuu wa mkoa amesema wakamtwe mnalialia.Jamii yetu imejaa Wahalifu na wanafiki wote wanastahili kuchomwa moto .

Ili kuepukana na Moto jamiii nzima irejee Kwa Mwenyezi Mungu.
Watu watubu dhambi zao.
Watu waache njia zao mbaya.
Jamii yetu watu wengi wameumizwa na matendo mabaya ya watu wengine.

Kuna watu wengi wanafanya maovu makubwa Tena Kwa kushindana. Rushwa ,wizi wa Mali za umma ,zinaa kila Kona, uporaji, watu wanauza bidhaa feki, matapeli ,biashara HARAMU , watu wanauza mafuta yaliyochakachuliwa, madereva hawafuati SHERIA, Polisi hawafuati SHERIA , wakubwa wa mihimili hawafuati katiba , watu wanaibiwa kila Kona ,wafugaji hawafuati SHERIA . Maofisi yamejaa Wazinzi ,washirikina ,walevi na wapiga dili.
Wote hao adhabu yao ni moto.
Wakizuia moto wa mitaani hawatazuia ule wa Jehanam..

Wote tunapaswa kumrudia Mwenyezi Mungu.
Wote tumesababisha Vijana wetu kuwa Panya road.
Wote tunastahili kuchomwa moto .
Wote tunastahili kureje kwenye misingi ya katiba. Wote wanastahili kuomba msamaha. Waliochoma moto binadamu mwenzao ni mwanzo TU wa kutufanya tutafakari maovu yetu wenyewe sio ya wengine.
 
Ni kweli ila watu watatumia mwaya wa kuchukua sheria mkononi hata kwa wasio na hatia
Thats how it goes.
Wote wanahatia kwani wote wametenda dhambi.
Dawa ni Watu wote turejee Kwa Mwanyezi Mungu.
Nchi yenye utajiri mkubwa aliouumba Mungu na sio mtu yeyote au Chama chochote Bali ni asili TU Mungu ameweka. Ni aibu kuwa na Vijana mamilioni wanaranda randa mitaani wakiuza pipi za kichina na midoli. Yaani mtu Amekaa mjini ana bidhaa ambayo mtaji wake hauzidi Elfu 20 halafu yupo katikati ya watu wanaoishi maisha ya anasa kila siku Kwa sababu TU yupo kwenye nafasi ya kusimamia rasilimali alizoziumba Mwenyezi Mungu. Sio sawa. Kuna mahali kama Jamii tumekosea wote. Wote tunastahili kuchomwa moto mpaka ule wa Jehanam.
 
Ndio maana kuna utawala wa sheria
Kwa hiyo wewe unashauri kama mtu kakuibia auliwe
Kuna mtu kanidhulumu elfu 20 nikamuue?
Ingetakiwa afikishwe kwenye sheria
Hivi umewahi kutafakari juu ya aina ya watu wanaotunga Sheria na wale walioko nyuma ya Kwa karibu. Ukatafakari uadilifu wao ,matendo yao,kauli zao, mitizamo yao juu ya waliko chini yao.

Angalia hata SHERIA za kimataifa mataifa yanayoweka mashinikizo ya kutunga SHERIA hizo ni mataifa ambayo ni mihimili ya uovu .

Wabunge waliochaguliwa Kwa wizi ,na rushwa hawana uhalali kiroho na kimwili kutunga SHERIA ya Haki. Hata wakitunga HAWAWEZI kusimamia watendaji wao ili kutenda haki.
Zao la uovu haliwezi kutenda haki Wala kusimamia haki.
Leo hii wanaotumia muda Mwingi kuwalaumu ,kuwadhalilisha na kuwatukana Polisi ni wale walioshirikiana na Polisi hao hao kuzuia jamii ili wasichague wawakilishi watakaotunga SHERIA za haki Kwa wote.

SHERIA haijali haki za hao Vijana waliokosa fursa.Zaidi Sasa inawataka wawe na namba ya mlipa Kodi ili walipe Kodi bila kuwa na vipato vinavyoeleweka.
 
NInakazia:

"Lawama zote ni kws serikali iliyoshindwa kuwadhibiti hawa watoto matokeo yake ndio haya....kuua na kuawa."
Mengine tunaibebesha Serikali bure, tuanzie kwa wazazi wa hawa vijana.
 
Napita ila kama kweli amepora mtu kwa silaha huyo ni panya road na hali yao inaeleweka. Huyo nyoni kama alichukua nguo bila idhini ya mwenyewe, alikuwa mwizi. KUHUSU UTAWALA WA SHERIA, KAMA UPO SIDHANI PANGEKUWEPO PANYA ROAD. Ni wa kufikirika.
 
Hujawahi kujeruhiwa au ndugu yako kupoteza maisha kwa kwa kupigwq na panda Road ndiyo maana unaongea hivyo.
 
Bad very bad
Kuna mwamba aliweka uzi hapa kuwa alimkopesha demu elfu 50, kwenda kudai yule demu akamwitia mwizi. Jamaa alikimbia kuokoa maisha yake, inakuwaje kama watu wangejichukulia sheria mkononi. Angeweza poteza maisha na hakuwa na hatia. WE HAVE TO OBSERVE RULE OF LAW, WE ARE NOT ANIMALS. .
Kama ni Panya road kweli acha auwawe.

Hao panya road wanafuata rule of law? Are they beast or human beings?
 
Ndio maana kuna utawala wa sheria
Kwa hiyo wewe unashauri kama mtu kakuibia auliwe
Kuna mtu kanidhulumu elfu 20 nikamuue?
Ingetakiwa afikishwe kwenye sheria
Hiyo sheria ndio haimshughulikii mhalifu ipasavyo
 
Habari za Jioni
Kuna jambo la kusikitisha sana ambalo limenifanya niwaze sana mda huu. Jioni hii saa moja kuna kijana ambaye ni panya road amechomwa moto barabara ya kutokea sweet corner kuelekea Manzese darajani (karibu na machine za kusaga). Kijana huyo ambaye alimpora mtu kwa kutumia silaha amepigwa na kuchomwa moto. .

Kilichonisikitisha ni kuwa sikutegemea kama kuna watu wenye hulka za kuchukua sheria mkononi. Hii nchi ina mfumo wa sheria na hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria, leoo hii wamemuua kijana wa watu inakuwaje kesho wakamuua mtu mwingine ambaye anashukiwa tu kuwa ni mwizi. Serikali, wadau wa haki za binadamu na jeshi la polisi linatakiwa liangalie hili swala kwa jicho la tatu. .

Nakumbuka kuna kijana nilisoma nae form two alikiwa anaitwa James Nyoni, huyu kijana alikuwa anapenda maisha mazuri tu ya kujionyesha onyesha. Nakumbuka alichukua pamba za mtu gheto akazitinga jamaa mwenye pamba zake akakutana nae mitaa ya Ubungo. Ilikuwa mwaka 2010, yule mwenye pamba akamwitia rafiki yake mwizi na watu walimpiga na kumchoma James Nyoni moto. Hili ni moja ya tukio ambalo liliniachia simanzi kubwa sana kwa sababu ya nguo jamaa akachomwa moto. .

Am very sad about this. We are not savages we are really people and we should be civilized. People should take law at their own hands, and tonight I believe Panya Roads will retaliate. My house being in street of Manzese no one will be safe, begging the Police and the street watchmen to guard the innocent people and their families. .
Wao hao panya road wanapojichukulia Sheria mkononi wa kutukata mapanga na kutuibia vitu vyetu tulivyovitolea jasho haki inasemaje hapo?? Wachomwe tu ilimradi amethibitika amepora kwanini apore??
 
Unapoandika suala zito kama hili la panya road, usiegemee upande wowote, kuwa huru, jiweke kati kati.

Vinginevyo nawe utaonekana ni panya road tu ama mnufaika.

Kuna binti kauawa mitaa ya Dar na hao panya road na mpaka muda huu kuna taharuki kubwa sana kitaifa na msiba mkubwa familia ikiomboleza na kusaga meno!

Sasa sijasikia popote ukianza kwanza kulaani kuuawa kwa huyo raia mwema asiye na hatia ama kutoa pole kwa familia iliyouliwa familia yao na hao vibaka.
Ndio mambo yao wanaojifanya kupigania haki za binadamu, mtu kakamatwa kafungwa miez sita amerudi kafanya uharifu wa kuua naye anapaswa kuuawa ili aone tamu ya kuua
 
Unasikitika watu kuchukua sheria mkononi huku wao panya rodi walivyokua wakijichukulia sheria mkononi hauskitiki

Wakati huo huo polisi wamewashindwa sasa wewe unataka wananchi wasishugulike nao wao wenyewe

Wabongo mmerogwa? mnatakeje sasa
 
Nilikua nawaonea huruma kama wewe ila kwa matukio ya kikatili wanayofanya hiyo dhambi ya wakiomba mafuta ya petroli mimi naweza kutoa ulifanyika ukatili iwambi mbeya kwa mama mjane tena walirudia kuiba mara tatu siku na miezi tofauti hapo kawe nimesoma juzi taarifa kuwa wamevunja nyumba wapangaji wote wamewaibia na kumuua dada mmoja maumivu yake hapo sio ya kitoto...mbaya zaidi wao ndio wanaamua wakuachie uhai au laa na wana siraha za kuua hawabahatishi kabisa hao ni wanyama mimi sio mnafiki eti wauaji wakiuawa niumie hapana kwa kweli..mbeya waliwahi mpiga nondo dogo mmoja kafika nyumbani nje anagonga wahuni wakamvamia saa mbili tuu usiku wakamuua na kuondoka na vitu ambavyo hata ukiambiwa kuwa wameua utudhunika maisha yako yote..
 
Uliwahi kusikia ule semi wa umdhanaye siye ....?

Hudhani hii yaweza kuwa nafasi nzuri ku settle personal vendetta?

Kama kuwahisi tu watu inatosha, mahakama za nini basi?

Wahenga hao hao walisema lisemwalo lipo.

Kama unadhaniwa tu kuwa wewe ni mmoja wa panyaroad basi character yako ina walakini.

Watu hawatoki out of the blue kusema wewe ni panyaroad au mwizi au punda wa ngada etc etc.

Yeyote anahusishwa na uhalifu asurubiwe barabara hakuna namna.
 
Back
Top Bottom