Panya Road achomwa moto Manzese

Panya Road achomwa moto Manzese

Watu wameshavurugwa,wamechoka na panya road
Hata kama ni hivyo, haya mambo ya kuchukua sheria mkononi, yana madhara makubwa sana!!kwani ni watu wenhi wamepoteza maisha kwa chuki yu, mtu una ugomvi naye anakuitia mwizi, tayari!!na kibaya zaidi hao wanaoshambulia huwa haya hawanaha muda wakufuatilia ninkweli wao ni kutoa kipigo tu!!labda kungekuwa na vigezo fulani vya kuangalia labda mtuhumiwa amekutwa na mali aliyoiiba, hapo kidogo sawa.
 
Habari za Jioni
Kuna jambo la kusikitisha sana ambalo limenifanya niwaze sana mda huu. Jioni hii saa moja kuna kijana ambaye ni panya road amechomwa moto barabara ya kutokea sweet corner kuelekea Manzese darajani (karibu na machine za kusaga). Kijana huyo ambaye alimpora mtu kwa kutumia silaha amepigwa na kuchomwa moto. .

Kilichonisikitisha ni kuwa sikutegemea kama kuna watu wenye hulka za kuchukua sheria mkononi. Hii nchi ina mfumo wa sheria na hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria, leoo hii wamemuua kijana wa watu inakuwaje kesho wakamuua mtu mwingine ambaye anashukiwa tu kuwa ni mwizi. Serikali, wadau wa haki za binadamu na jeshi la polisi linatakiwa liangalie hili swala kwa jicho la tatu. .

Nakumbuka kuna kijana nilisoma nae form two alikiwa anaitwa James Nyoni, huyu kijana alikuwa anapenda maisha mazuri tu ya kujionyesha onyesha. Nakumbuka alichukua pamba za mtu gheto akazitinga jamaa mwenye pamba zake akakutana nae mitaa ya Ubungo. Ilikuwa mwaka 2010, yule mwenye pamba akamwitia rafiki yake mwizi na watu walimpiga na kumchoma James Nyoni moto. Hili ni moja ya tukio ambalo liliniachia simanzi kubwa sana kwa sababu ya nguo jamaa akachomwa moto. .

Am very sad about this. We are not savages we are really people and we should be civilized. People should take law at their own hands, and tonight I believe Panya Roads will retaliate. My house being in street of Manzese no one will be safe, begging the Police and the street watchmen to guard the innocent people and their families. .
Ingekuwa inawezekana wapigwe risasi
 
Hata kama ni hivyo, haya mambo ya kuchukua sheria mkononi, yana madhara makubwa sana!!kwani ni watu wenhi wamepoteza maisha kwa chuki yu, mtu una ugomvi naye anakuitia mwizi, tayari!!na kibaya zaidi hao wanaoshambulia huwa haya hawanaha muda wakufuatilia ninkweli wao ni kutoa kipigo tu!!labda kungilekuwaa vigezo fulani vya kuangalia labda mtuhumiwa amekutwa na mali aliyoiiba, hapo kidogo sawa.
Duuuh kumbe watetezi wa panyaroad mpo wengi hivi?

Yaan wewe watu kupingwa mapanga na kuuliwa na hao panyaroad unaona ni sawa tu kwako ila panyaroad wakishugurikiwa unaanza kupaza sauti? Tutawanyoosha na nyinyi watetezi wao endeleeni tu
 
Ndio maana kuna utawala wa sheria
Kwa hiyo wewe unashauri kama mtu kakuibia auliwe
Kuna mtu kanidhulumu elfu 20 nikamuue?
Ingetakiwa afikishwe kwenye sheria

[mention]Gily [/mention] unajua kaka sheria zipo na wanaokiuka izo sheria pia ndo tatizo binafsi nikimkuta wanamchoma moto naenda nitamwokoa kwa kumtoa pale ila nitampeleka sehemu nimkate mikono tuu yote miwili baas af namwacha, ila suala ka kuua kama unauwezo fanya kweli maana mi babu yangu juzi hapa kapigwa na vyuma kichwani nusu hadi akazilai sa sijui walijua wamehua ndo wakamsachi wakachukua tu kiswaswadu imajine sim ambayo thaman yake haifikii ata ghalama tulizotumia kwa nauli kumpeleka hospitali acha kishonwa na kumuuguza! Unayesema ivo hayajawahi kukutokea yakikutokea ndo utajua

alafu watu wanachekesha sana yani mtu aje na panga ama kisu na anakuchoma bila kujali kama utapona au lah kisa kuchukua kitu ulichotafuta kwa jasho lako huenda ela wanazotaka kuchukua maybe nizamkopo ulokopa iliufanye biashara familia yako isilale njaa them ye ukimkamata ukamkata na ilo ilo panga we ndo unakua mbaya na nikulize ni mwizi hau kibaka gani ushaskia anapelekwa polisi et akajiskia vibaya? Wao ukiwapeleka polisi ni sawasawa nakuwaokoa ila kwenye kifo ndo huwafundisha kua malipo ya walitendalo ni umauti na inasadia reference angalia kipindi cha MWENDAZAKE yule mkeukaji wa haki za vibaka.
 
Kwenye kuwashughulikia mnajuwaje huyu ndiye na huyu siye?

Shughulikia yeyote yule anayehusishwa nao. Easy fix

Mtu makini hawezi kuhusishwa nao kwa namna yeyote ile.
 
wewe unajua damage ya panya Road ama unakuja kuandika hapa?
Kaka elewa maana ya utawala wa sheria vp kaka ,mdogo,au baba yako awe na uhasama na mtu alafu yule mtu amuitie mwizi auwawe kwa kuchomwa moto utajisikiaje hasa ukija kujua kuwa amewawa kwa kosa asilo stahili?
Mm binafsi nilitokea kuchukia mchozo huo mwaka 2012 alipo uwa mwanafunzi wa kidato cha 4 majira ya saa 9 usiku alikuwa ametoka kujisomea raia walikuwa wamemkurupusha mwizi wao dogo akatokea kwa mbele akauwawa na kulipo kucha ikafahamika dhahiri kuwa dogo hakuhusika na tukio la wizi
Sasa imagine upo sehemu mfano kkoo anatokea mtu ambae ana uhasama na ww anakupigia yowe la mwiziiiiii simu yangu unadhani wanao jichukulia sheria mikononi watapata wasaa wa kukusikikiza au itakua ni kifo? Tafakari ndugu
 
Punguza ujinga ndugu.haki za binadamu zinahusu wale wenye dhamana na mamlaka yakulinda usalama wa binadamu.sasa panya road ana mamlaka gani.inasemwa hivyo ili kusiwe na matumizi mabaya ya mamlaka kwasababu mamlaka ikiamua inaweza kuswaga wananchi wote kama mbuzi na msihoji chochote.vibaka wakifanya uhuni kuna vyombo vyenye mamlaka vyakuwachukulia hatua je siku ikitokea mamlaka ndio iliyovunja sheria ni nani wakuiwajibisha?.Ndo maana wenye akili wanaweka hizo haki na maangalizo.

Panya road wasurubiwe barabara stop this haki za binadamu BS. Victims wa panya road wana haki zao as well.
 
Kaka elewa maana ya utawala wa sheria vp kaka ,mdogo,au baba yako awe na uhasama na mtu alafu yule mtu amuitie mwizi auwawe kwa kuchomwa moto utajisikiaje hasa ukija kujua kuwa amewawa kwa kosa asilo stahili?
Mm binafsi nilitokea kuchukia mchozo huo mwaka 2012 alipo uwa mwanafunzi wa kidato cha 4 majira ya saa 9 usiku alikuwa ametoka kujisomea raia walikuwa wamemkurupusha mwizi wao dogo akatokea kwa mbele akauwawa na kulipo kucha ikafahamika dhahiri kuwa dogo hakuhusika na tukio la wizi
Sasa imagine upo sehemu mfano kkoo anatokea mtu ambae ana uhasama na ww anakupigia yowe la mwiziiiiii simu yangu unadhani wanao jichukulia sheria mikononi watapata wasaa wa kukusikikiza au itakua ni kifo? Tafakari ndugu
Mmeanza kujitetea mmeanza mnateteana labda tusiwadake.. unaleta simulizi za 2012 tupo 2012 hapa? Tena msituchezee akili waambie bado tuna hasira
 
Acha kuwatetea Hawa pNya buku mkuu mwenywe wa mkoa kashasema Kama mwanao au nfdug yako apatikani bas njoni kituoni ama hospitalini hvyo sasa HV Ni mwendo wa kutumia elimination method tu

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Mmeanza kujitetea mmeanza mnateteana labda tusiwadake.. unaleta simulizi za 2012 tupo 2012 hapa? Tena msituchezee akili waambie na wenzako bado tuna hasira
Rejea hoja zangu hapo juu kwa upeo huru bila jazba mm nimetoa mifano na athari juu ya athali zinazo weza kutokea kwa kujichukulia sheria mikononi maana tabia hiyo ikishamiri sana inaweza kuhatarisha usalama wa raia wema na panya road pia
 
Acha iwe mlianza sisi tunamaliza.. yaan Mimi mtu anaewatetea panyaroad na yeye namuona panyaroad tu hamna tofauti.. wewe sheria gan inayokuruhusu kubeba panga na kuwakata raia unazijua sheria wewe? Unazijua sheria wewe? Wakati mnakata watu mapanga mlijua kuhusu sheria nyinyi? Wakati mnaua mlijua kuhusu sheria? tena unabahati na utadakwa tu
 
Habari za Jioni
Kuna jambo la kusikitisha sana ambalo limenifanya niwaze sana mda huu. Jioni hii saa moja kuna kijana ambaye ni panya road amechomwa moto barabara ya kutokea sweet corner kuelekea Manzese darajani (karibu na machine za kusaga). Kijana huyo ambaye alimpora mtu kwa kutumia silaha amepigwa na kuchomwa moto. .

Kilichonisikitisha ni kuwa sikutegemea kama kuna watu wenye hulka za kuchukua sheria mkononi. Hii nchi ina mfumo wa sheria na hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria, leoo hii wamemuua kijana wa watu inakuwaje kesho wakamuua mtu mwingine ambaye anashukiwa tu kuwa ni mwizi. Serikali, wadau wa haki za binadamu na jeshi la polisi linatakiwa liangalie hili swala kwa jicho la tatu. .

Nakumbuka kuna kijana nilisoma nae form two alikiwa anaitwa James Nyoni, huyu kijana alikuwa anapenda maisha mazuri tu ya kujionyesha onyesha. Nakumbuka alichukua pamba za mtu gheto akazitinga jamaa mwenye pamba zake akakutana nae mitaa ya Ubungo. Ilikuwa mwaka 2010, yule mwenye pamba akamwitia rafiki yake mwizi na watu walimpiga na kumchoma James Nyoni moto. Hili ni moja ya tukio ambalo liliniachia simanzi kubwa sana kwa sababu ya nguo jamaa akachomwa moto. .

Am very sad about this. We are not savages we are really people and we should be civilized. People should take law at their own hands, and tonight I believe Panya Roads will retaliate. My house being in street of Manzese no one will be safe, begging the Police and the street watchmen to guard the innocent people and their families. .
Wewe Kaka unazungumzia sheria zipi? Mfumo upi wa haki hapa Tanzania ambao uko organized kwa ajili ya kubambikia kesi wapinzani? Hakuna kitu hicho hapa bongo.

Tuombe Mungu tu
 
Shughulikia yeyote yule anayehusishwa nao. Easy fix

Mtu makini hawezi kuhusishwa nao kwa namna yeyote ile.

Uliwahi kusikia ule semi wa umdhanaye siye ....?

Hudhani hii yaweza kuwa nafasi nzuri ku settle personal vendetta?

Kama kuwahisi tu watu inatosha, mahakama za nini basi?
 
Wewe Kaka unazungumzia sheria zipi? Mfumo upi wa haki hapa Tanzania ambao uko organized kwa ajili ya kubambikia kesi wapinzani? Hakuna kitu hicho hapa bongo.

Tuombe Mungu tu

Si wapinzani tu.

Nakazia: Kubambikizia watu kesi.
 
Ndugu kuna watu wanajionaga watakatifu sana bila kujua huo utakatifu wao unalindwa na sheria.siku kukiwa hakuna hizo sheria yoyote anaweza kuhukimiwa bila kupata muda wakusikilizwa au kuthibitishwa.

Ndiyo maana tuko hapa tulipo na mkwamo wa katiba mpya.

Watu hawajui haki za kila mtu hazina majadiliano. Tuna magenge ya wajinga.

Waliona mbali sana Ulimwengu, FAM, Lissu, Maria, Fatma na wenzao kwa kuyasema hadharani:

IMG_20220914_180443_804.jpg

Cc: Countrywide
 
Ndiyo maana tuko hapa tulipo na mkwamo wa katiba mpya.

Watu hawajui haki za kila mtu hazina majadiliano. Tuna magenge ya wajinga.

Waliona mbali sana Ulimwengu, FAM, Lissu, Maria, Fatma na wenzao kwa kuyasema hadharani:

View attachment 2359209

Cc: Countrywide
Mtu ambaye bado anafikiria kuua mwenzake kwa visababu vidogo vidogo ni Hayawani tu huyo.
 
Back
Top Bottom