Habari za Jioni
Kuna jambo la kusikitisha sana ambalo limenifanya niwaze sana mda huu. Jioni hii saa moja kuna kijana ambaye ni panya road amechomwa moto barabara ya kutokea sweet corner kuelekea Manzese darajani (karibu na machine za kusaga). Kijana huyo ambaye alimpora mtu kwa kutumia silaha amepigwa na kuchomwa moto. .
Kilichonisikitisha ni kuwa sikutegemea kama kuna watu wenye hulka za kuchukua sheria mkononi. Hii nchi ina mfumo wa sheria na hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria, leoo hii wamemuua kijana wa watu inakuwaje kesho wakamuua mtu mwingine ambaye anashukiwa tu kuwa ni mwizi. Serikali, wadau wa haki za binadamu na jeshi la polisi linatakiwa liangalie hili swala kwa jicho la tatu. .
Nakumbuka kuna kijana nilisoma nae form two alikiwa anaitwa James Nyoni, huyu kijana alikuwa anapenda maisha mazuri tu ya kujionyesha onyesha. Nakumbuka alichukua pamba za mtu gheto akazitinga jamaa mwenye pamba zake akakutana nae mitaa ya Ubungo. Ilikuwa mwaka 2010, yule mwenye pamba akamwitia rafiki yake mwizi na watu walimpiga na kumchoma James Nyoni moto. Hili ni moja ya tukio ambalo liliniachia simanzi kubwa sana kwa sababu ya nguo jamaa akachomwa moto. .
Am very sad about this. We are not savages we are really people and we should be civilized. People should take law at their own hands, and tonight I believe Panya Roads will retaliate. My house being in street of Manzese no one will be safe, begging the Police and the street watchmen to guard the innocent people and their families. .
Watachomwa moto sana na hata wewe unastahili kuchomwa moto sio huu TU mpaka wa Jehanam mana ni Mnafiki .
Wanafiki ni watu hatari kuliko panya road.
Mwanyekiti Mungu alishusha mpaka Aya ya wanafiki ili kuwaonya.
Wale wanaojiita Watu wa Haki za Binadamu nao pia Wana unafiki.
Polisi wakikamata watu mnlia Lia . Wakiwaacha mnalialia .
Watu wameamua kupambana wenyewe na Wahalifu mnalialia mnataka Nini? Jamii ndiyo inayowafahamu Wahalifu. Mkuu wa mkoa amesema wakamtwe mnalialia.Jamii yetu imejaa Wahalifu na wanafiki wote wanastahili kuchomwa moto .
Ili kuepukana na Moto jamiii nzima irejee Kwa Mwenyezi Mungu.
Watu watubu dhambi zao.
Watu waache njia zao mbaya.
Jamii yetu watu wengi wameumizwa na matendo mabaya ya watu wengine.
Kuna watu wengi wanafanya maovu makubwa Tena Kwa kushindana. Rushwa ,wizi wa Mali za umma ,zinaa kila Kona, uporaji, watu wanauza bidhaa feki, matapeli ,biashara HARAMU , watu wanauza mafuta yaliyochakachuliwa, madereva hawafuati SHERIA, Polisi hawafuati SHERIA , wakubwa wa mihimili hawafuati katiba , watu wanaibiwa kila Kona ,wafugaji hawafuati SHERIA . Maofisi yamejaa Wazinzi ,washirikina ,walevi na wapiga dili.
Wote hao adhabu yao ni moto.
Wakizuia moto wa mitaani hawatazuia ule wa Jehanam..
Wote tunapaswa kumrudia Mwenyezi Mungu.
Wote tumesababisha Vijana wetu kuwa Panya road.
Wote tunastahili kuchomwa moto .
Wote tunastahili kureje kwenye misingi ya katiba. Wote wanastahili kuomba msamaha. Waliochoma moto binadamu mwenzao ni mwanzo TU wa kutufanya tutafakari maovu yetu wenyewe sio ya wengine.