Panya road wanauawa kwa risas. Je, wezi wa mabilioni ya kodi za Watanzania wanabakije salama?

Utamaliza vijana wewe.
Mkuu nilikuwa namjibu huyo

Nilimaanisha ikiwa yeye anaona ni sahihi panya road kuuawa na wabadhirifu wa mali za umma nao wauawe kama ambavyo wanawafanyia panya road, wanafuatwa majumbani mfano aliesema billion ni vijisenti pyupyupyu nae inamuhusu hapo nami ndipo ntakubaliana Kwa sheria na katiba kutokufuatwa
 
Panya road wanaua na kudhuru mwili,mbadhirifu anamuua nani na anamdhuru mwili nani?
Hawa panya road wameua wangapi kwa mwaka huu tuu ?

Hao wabadhirifu wameua mamilioni ya watu ,ni wangapi wamepoteza maisha kwa kukosa huduma ya afya ? Wangapi wamepoteza maisha kwa kukosekana huduma ya mama mjamzito karibu na makazi yao ?

Kwenye afya tuu mkuu ni wengi saana lakini sisi muda wote tunawaimbia mapambio hao wabadhirifu na panya road tunawaona makatili kweli
 
Wengi Sana
 
Mkuu una kichwa kigumu sana, hajatetea panya rodi bali kasema ni lini wezi wa mabilioni wanaosababisha watu kufa kwa kukosa huduma muhimu watapewa adhabu kama wanazopata panya rodi?
 
Nimeamini nchi hii ina wajinga wwngi mmoja wao ndio wewe. Kwa hio unataka panya road waachiwe tu ee?
Kwa hii coment yako wewe ndiye mjinga, hajasema waachiwe kasema wezi wa mali ya umma nao wapewe adhabu kama za panya rodi, mbona china wanatoa adhabu za panya rodi kwa wezi wa mali ya umma
 
Wengi Sana
Hao wengi sana wepi waliouawa na panya road au waliopoteza maisha sababu ya kukosa huduma za afya ?
Kwa hiyo panya road wameanza mwaka huu au? Wameanza kukata watu mwaka huu au?

I wish waje wakunyooshe one day ili ukome kuandika ujinga.
 
Wewe ni punguani,hao wezi si ndio mliokua mnawatetea wakati JPM anawaadabisha
Kwa hii coment yako wewe ndiye mjinga, hajasema waachiwe kasema wezi wa mali ya umma nao wapewe adhabu kama za panya rodi, mbona china wanatoa adhabu za panya rodi kwa wezi wa mali ya umma
 
Wakati wanaongezwa wanaolawiti watoto basi waongezwe na wezi wa mali ya umma
 
Wewe ni punguani,hao wezi si ndio mliokua mnawatetea wakati JPM anawaadabisha
Acha uongo lini JPM aliwapiga chuma wezi wa mali ya umma? Ndio kwanza matrilioni yalipotea alivyokuwa rais
 
Hakuna anaewatetea polisi wao wanapambana na panya road na sisi Wananchi kama tunaumizwa na hawa viongozi tuandamane, tuwazomee kilawanapopita, wasipojirekebisha tupige mawe gari zao mwisho kabisa kama awajabadilika adhabu ya kifo inawahusu kutoka kwetu Wananchi
 
wa ubelgiji si huwa mnasema alipigwa chuma na JPM ama mmesahau?na aliowarundika jela umewasahau. Wabongo kwa kujisahaulisha mpo vizuri. Panyaroad tulia polisi wakushughulikie
Acha uongo lini JPM aliwapiga chuma wezi wa mali ya umma? Ndio kwanza matrilioni yalipotea alivyokuwa rais
 
Tunataka panya rodi waendelee kupata wanachokipata sasa kutoka kwa polisi ila na wezi wa mali ya umma nao waongezwe kwenye list ya panya rodi nao wale chuma
 
Wezi wa mabilioni awaondoshwi madarakani na polisi wanaondolewa madarakani na sisi Wananchi kama hawa viongozi awatufai ni sisi Wananchi ndio tunatakiwa kuchukua hatua na wala sio polisi
 
wa ubelgiji si huwa mnasema alipigwa chuma na JPM ama mmesahau?na aliowarundika jela umewasahau. Wabongo kwa kujisahaulisha mpo vizuri. Panyaroad tulia polisi wakushughulikie
Sasa huyo wa ubeligiji alikula lini mali ya umma?
 

Tuwe na sheria kama China. Kesi iendeshwe, halafu hukumu. Suala la kuwafuata nyumbani, tunaweza kupoteza hata wasio na hatia.
 
Kinachonisgaza, ni kupigwa shaba wezi wadogo badala ya kukamatwa wakajibu na kuachwa majizi papa yakiendelea kuiba kila uchwao,

Wore wanapaswa wale shaba tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…