Panya road wanauawa kwa risas. Je, wezi wa mabilioni ya kodi za Watanzania wanabakije salama?

Panya road wanauawa kwa risas. Je, wezi wa mabilioni ya kodi za Watanzania wanabakije salama?

Kundi la vijana wanaojulikana kama Panya road' limekuwa ni tishio kwa wananchi kwa siku za hivi karibuni!

Vijana hawa wamekuwa wakitishia usalama wa jamii na hata kufanya mauwaji mbalimbali kwa lengo LA kuiba na kupora kila kilicho mbele ya macho yao!

Tunapenda kulishukuru Jeshi la police kwa kuanza kudhibiti hawa vijana na kuanza kurudisha amani katika mitaa iliyokuwa ikivamiwa Mara kwa Mara kwa kuwakamata hawa vijana alimarufu kwa jina la Panya road

Mbali na kuwakamata, wengine wamekuwa wakipigwa risasi na kufa papo hapo, adhabu hii ndiyo inayopelekea kuuliza juu ya wezi wa Mabilion ya fedha za kodi za wananchi

Wezi hawa wa kodi zetu, ndio wauwaji wakubwa wa watu wanaokufa kwa kukosa huduma mahospitalini!

Watu wanaokufa kwa kukosa gari la wagonjwa ili tu kuwahi huduma katika hospital zetu kuu!

Wajawazito wanakufa kutokana na mtu mmoja tu kuiba kodi ambazo zingeondoa kero hiyo, halafu police wetu wana ng'aa ng'aa sharubu badala ya kutandika risasi liuwaji kama hilo

Badala yake, anauliwa kijana mwenye njaa tuu, kaiba kuku ili akale na wanae, anatandikwa risasi badala ya kukamatwa ili akajibu makosa yake

Ni lini yataanza kupigwa risasi majizi na mauwaji ya wananchi haya yanayoiba kodi zetu ambapo zingewezesha upatikanaji wa huduma nzuri mahospitalini na kuweza kupatiwa bima kwa watanzania wote?

La hatutaki kuwashuti hawa wezi wa mabilioni yetu, tusiwauwe na hawa wanaoiba Mchele ili wakakidhi njaa zao
The approach is reciprocal to the type /modality of the crime. You can't come up with a typical insurgency approach and we react to the panyavibwengo with lunacy like birthday celebrations. This time we have opted for military way bcoz in any case we don't know who is behind this un imaginable peace threats within our communities.

You plant seeds of insurgency type we go military procedurally and this hasn't been police own decisions but the command of national security committee bcoz there has been repetitions of such deadly vibakaz.

This is a typical protrusion prototype of insurgency cases.


Please kindly, we the general public should heavily support this police approach of eliminating such rats.


POLICE: I thank you and commend you vehemently and all the time. 🙏🙏🙏
 
Mkuu temeke iyo niliwahi poteza viatu na simu baada ya kukutana na kundi la vijana kati 6/7.

Binafsi sina la kulishauri jeshi la polisi . Waachwe waendelee tu na mkakati wao mpaka mwisho
Pole boss. Ukute hapo hivyo vitu hata wakigawana hawapati pesa ya kula wiki ila walitaka kukutoa uhai.
 
Badala yake, anauliwa kijana mwenye njaa tuu, kaiba kuku ili akale na wanae, anatandikwa risasi badala ya kukamatwa ili akajibu makosa yake
Panya road haibi Kuku ,Panya road ni wauaji ,ni sawa na majambazi ,siwezi kuwatetea Panya road ,DAWA YA PANYA ROAD NA MAJAMBAZI NI KULA VYUMA TU.
 
Mkuu samahani kwako wewe wezi wa mabilioni wapo sahihi na wala wizi wao hauna madhara ?

Nchi hii kweli nimeamini wananchi wake wamejaa roho mbaya saana ,unawezaje kuhalalisha wizi wa mabilioni ambayo ilikuwa inaweza kwenda kujenga vituo vya afya ama kununua madawa hospitalini.

Hujawahi kujiuliza vifo vinavyosababishwa na ukosefu wa huduma kuwa mbali ama ukosefu wa dawa vipi vingapi ?
Hajahalalisha mkuu. Panya road hauawi kwasababu ya kuwa yeye ni mwizi. Panya road anauawa kwasababu anadhuru mwili na anaua watu katika huo wizi wanaofanya. Licha ya kukuibia mali yako halali bado anakudhuru na mwili kabisa, tena kwa asilimia kubwa hawa panya road wanawaibia na kuwadhuru watu masikini na wale wa kipato cha kati. Akithibitishwa wacha hatma yake impate tu.

Kwa upande wa watuhumiwa wa wizi wa mabilioni ya umma na wao pia washughulikiwe. Lkn kwa kuwa hawajamdhuru yeyote kwa silaha basi wao wafilisiwe wala wasiuawe. Anayedhuru kwa upanga na adhuriwe kwa upanga au chochote chenye ncha kali
 
Bokoboko mabapa mixer mabanzi ila pilau kwa kua lina viungo vingi unakatwakatwa .Jamaa yangu alikutana nao akachagua pilau aisee usiombe.Halafu hawa chupi sijui wanasema nini hawa.
Hatari sana aisee
 
Acheni kutetea ujinga, hao wezi wa mabilioni wamemshikia nani panga, hao wezi wa mabilioni wamembaka nani?? Hujasiki mama na mtoto wakibakwa na hao panya road??.. pesa zinatafutwa lakini uhai wa mtu haupatikan popote ukishapotea, hao unaosema wezi wa mabilioni si unaona wanakufa na kuyaacha tunaanza kung'ang'aniana Tena. Panya road wafe TU hao wezi wa mabilioni tutajua namna ya kudili nao tu
Naunga mkono hoja, auwae kwa panga au nyembe naye amalizwe kwa bastola tu. Kama
tadin tudan! Al Qisasl haq
 
Wanauliwa kwa Sumu kidogo kidogo huku wakishangilia.
Watu wanakufa kwa UTI, typhoid, UKIMWI, kifua kikuu kwasababu ya umaskini ulioletwa na wanasiasa
Mpuuzi wewe.

Endelea kutetea hawa Panya road siku wakiichakata Tigo yako akili zitakukaa sawa

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Labda wewe huelewi

Kuna kitu kinaitwa post hoc fallacy, cause effects relationship. Unachotaka kusema ni kwamba kwa sababu wezi wa mamilioni wameachwa (sidhani kama una ushahidi wowote kuwa fulani kaiba ngawila hizi hajapelekwa mahakamani) basi na panya rodi nao waachwe waendelee kuleta taharuki mitaani. Ni vitu viwili ambavyo unalazimisha viwe na uhusiano, lakini kimsingi havina.
 
Kuna kitu kinaitwa post hoc fallacy, cause effects relationship. Unachotaka kusema ni kwamba kwa sababu wezi wa mamilioni wameachwa (sidhani kama una ushahidi wowote kuwa fulani kaiba ngawila hizi hajapelekwa mahakamani) basi na panya rodi nao waachwe waendelee kuleta taharuki mitaani. Ni vitu viwili ambavyo unalazimisha viwe na uhusiano, lakini kimsingi havina.

Hapa inshu sio waachwe bali wote pyupyupyu iwahusu si ndio utaratibu mpya tumeuanzisha kwa wavunja sheria na katiba
 
Back
Top Bottom